Tuesday, March 26, 2019

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA SITA WA UMOJA WA MAAFISA ELIMU WA MIKOA NA HALMASHAURI

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua   Mkutano Mkuu wa Sita wa Maafisa  Elimu wa Mikoa na Halmashauri (REDOA) kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma, Machi 26, 2019.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Sita wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri (REDOA) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Mkutano huo kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma, Machi 26, 2019.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo baada ya kufungua  Mkutano Mkuu wa Sita wa Maafisa Elimu  wa Mikoa na Halmashuri (REDOA) kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma, Machi 26, 2019. Kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako, wa pili kulia ni Mwenyekiti wa REDOA, Germana Mung’aho.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na Mwenyekiti wa Umoja wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri  (REDOA), German Mung’aho baada ya kufungua Mkutano  Mkuu wa Sita wa REDOA kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma, Machi 26, 2019.  Wa pili kulia ni  Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako, kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jafo na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

MAWAZIRI WA AFRIKA WAKUTANA MOROCCO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Morocco, Mhe. Nasser Bourita,  baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mkutano.


Dkt. Mnyepe amemwakilisha Mhe.
Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika kuhusu maamuzi ya Umoja wa Afrika (AU) kuunga mkono jitihada za usuluhishi wa mgogoro wa eneo la Sahara Magharibi kati ya Morocco na Saharawi uliofanyika jijini Marrakech, Morocco tarehe 25 Machi, 2019.

Katibu Mkuu, wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Mnyepe akifuatilia
mazungumzo na michango ya wajumbe kutoka nchi mbalimbali wakati wa mkutano
huo.

Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe wa tatu kutoka kushoto, mstari wa nyuma, akiwa katika picha ya pamoja ya Mawaziri na Wawakilishi wa Mawaziri walioshiriki mkutano huo.