Thursday, March 14, 2019

SERIKALI YAOKOA BILION 3.4 KWENYE MATIBABU YA UGONJWA WA FIGO

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo wakati akitoa tamko la Siku ya Figo Duniani, lililotolewa leo katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma.
.............................


Na WAMJW-DOM.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali imefanukiwa kuokoa kiasi cha Shilingi Bilion 3.4 ambacho kingetumika katika matibabu kwa Wagonjwa wa Figo nje ya Nchi.


Dkt. Ndugulile ameyasema hayo leo Machi 14 wakati akiongea na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma ikiwa ni Siku ya Figo Duniani ambayo inaongozwa na kauli mbiu ya Afya ya figo kwa kila mmoja kila.


Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeokoa kiasi cha shilingi bilioni 4.2 ambacho kingetumika katika matibabu ya wagonjwa 80 mpaka 100 ambao wangepelekwa nje ya nchi kwaajili ya matibabu.


“Wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 42, kama tungewapeleka  wagonjwa nje ya nchi ingegharimu serikali kiasi cha shilingi bilioni 4.2 kwa idadi hiyo ya wagonjwa.  80 mpaka 100, wakati huduma hii hapa nchini inagharimu kiasi cha shilingingi milioni 21 kwa kila mgonjwa.” Alisema Dkt. Ndugulile.


Aidha, Dkt, Ndugulile amesema kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia magonjwa ya figo ni pamoja na uzito wa kupindukia (obesity), matumizi makubwa ya sigara, unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara,kutokufanya mazoezi na kunywa madawa kiholela hasa dawa za kupunguza maumivu.


Aliendelea kusema kuwa, magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu ni magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha matatizo ya figo, magonjwa haya yakitambuliwa mapema yanaweza kudhibitiwa kwa matibabu na kuepusha madhara kwenye figo.


Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile amesema kuwa Kufikia Desemba mwaka 2018, jumla ya vituo 28 vyenye jumla ya wagonjwa 1050 vilikuwa vikitoa huduma ya usafishaji damu katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro na Dodoma.


Mbali na hayo, Dkt. Ndugulile amesema Serikali imepiga hatua kubwa ya kuanzisha huduma za kupandikiza figo hapa nchini katika hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Figo nchini Dkt. Onesmo Kisanga amesema kuwa Ugonjwa wa Figo ni tatizo kubwa nchini huku wananchi wengi wakiwa na uelewa mdogo juu ya athari na visababishi vya ugonjwa huo.


Aidha Dkt. Onesmo amewataka wananchi kuacha tabia ya kunywa dawa bila kupata ushauri wa kitaalamu hivyo kuepuka kuzalisha sumu mwilini na kupelekea ugonjwa wa figo.


Hata hivyo Dkt. Onesmo Kisanga ameishukuru Serikali kwa kuwaendeleza kimasomo wataalam kwenye upande wa matibabu ya figo ambao sasa wamesambazwa sehemu mbali mbali ndani ya nchi kutoa huduma za matibabu.


Naye Dkt. Grace Maghembe Kaimu Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya amesema ungojwa huu umekuwa ukiwaathiri zaidi wakazi wa mijini kuliko vijijini kutoka na mfumo wa maisha uliopo sasa ambapo watu wengi wamekuwa hawazingatii mtindo bora wa maisha kwa kutofanya mazoezi pamoja na kula chakula bora.


Dkt. Maghembe amesema bado ipo changamoto kwenye matumizi ya dawa za mitishamba ambazo bado hazijatambuliwa na kuthibitishwa huku akiwataka wananchi kuwa waangalifu pia kwenye matumizi ya dawa hizo.


“Serikali inatambua umuhimu wa tiba mbadala pamoja na matibabu ya tiba za asili na ndio maana zipo taasisi za serikali zinazohusika kuzitambua dawa hizo ni zipi na zina vitu gani na unatakiwa kutumia kwa kiwango gani” amesema Dkt Maghembe nakuwataka watengenezaji wa dawa hizo kufuata taratibu zilizopo ili kuthibitisha na kusajili dawa zao.
 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye picha) wakati akitoa tamko la Siku ya Figo Duniani, lililotolewa leo katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma. Wakwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe na wamwisho ni Mwenyekiti wa Chama cha Magonjwa ya Figo nchini Dkt. Kisanga

Waandishi wa Habari waliojitokeza kumsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akitoa tamko la Siku ya Figo Duniani, lililotolewa leo katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma.

MTAMBO WA KUCHAKATA ASALI WAFUNGWA MANYONI

 Mtendaji Mkuu wa TFS Profesa Dos Sontos Silayo akiangalia mitambo ya kuchakata asali iliyofungwa wilayani Manyoni mkoani Singida.

 Mitambo ya kuchakata asali ambayo imefungwa katika kiwanda cha TFS wilayani Manyoni,mkoani Singida
.........................


WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umefunga mtambo wa kuchakata asali wilayani Manyoni mkoani Singida.


Akizungumza leo Machi 14,2019 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TFS Tulizo Kilaga amesema mtambo  huo wa kisasa una uwezo wa kuchakata lita 500 kwa siku.


Amesema kuwa mtambo huo umegharimu Sh.milioni 80 na unatarajiwa kuondoa changamoto ya uwepo wa asali yenye kiwango duni cha ubora katika ukanda huo na maeneo maeneo ya jirani.


“Mtambo huu umefungwa katika kiwanda cha TFS na utatumiwa na wafugaji wa nyuki wa ndani pamoja na nje wote wataruhusiwa kuchakata mazao yao,”amesema Kilaga.


Ameongeza kuwa kiwanda hiko kwa kiasi kikubwa kitategemea mali ghafi toka kwenye msitu wa Aghondi uliopo eneo la Itigi na uwepo wa mtambo huo pia utasaidia kutunza mazingira kwani watakuwa na uhakika wa soko la asali yao.

 
Pia amesema katika uvunaji wa awali wamefanikiwa kuvuna mizinga 459 kati ya 729 na kupata asali kilo  6,175 sawa na tani 6.175 wastani kilo 13.45 kwa mzinga.


Akizungumzia mtambo huo, Meneja wa TFS wilayani Manyoni Juma Mambo amesema utasaidia kupatikana kwa asali bora na hivyo kuwa na uhakika wa soko la ndani na nje ambalo litawafanya wadau kujiongezea kipato.


JOSHUA NASSARI AVULIWA UBUNGE.