Thursday, March 14, 2019

KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI (PAC) YAKAGUA UBORA WA BARABARA

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akikagua barabara ili kujiridhisha na ubora wake, Kamati hiyo ilipotembelea  na kukagua mradi wa ujenzi wa barabara Kuu ya kutoka Afrika Kusini mpaka Misri kipande cha Dodoma – Iringa Kilomita 260 maeneo ya Mlowa mkoani Dodoma  hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
 

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akiwaongoza wajumbe wa Kamati hiyo kukagua barabara maeneo ya Mlowa Mkoani Dodoma ili kujiridhisha na ubora wake, Kamati hiyo ilipokagua mradi wa ujenzi wa barabara kuu kutoka Afrika Kusini mpaka Misri kipande cha Dodoma – Iringa Kilomita 260 hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)

Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mheshimiwa Dkt. Haji Mponda akiuliza jambo kwa Mkurugenzi wa barabara Mhandisi John Ngowi (wa kwanza kushoto), Kamati hiyo ilipotembelea  na kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Dodoma – Iringa Kilomita 260 maeneo ya Mlowa  hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Moshi Selemani Kakoso, akisisitiza jambo kwa Naibu Mawaziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kwandikwa na Mhe. Atashasta Nditiye, wakati kamati hiyo ilipokagua ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma.
 
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati kamati hiyo ilipokagua ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Moshi Selemani Kakoso.

Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma, Bi. Bertha Bankwa, akielezea mkakati wa uboreshaji wa kiwanja hicho kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati kamati hiyo ilipokikagua.

Muonekano wa barabara ya kuruka na kutua ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma. Barabara hiyo imerefushwa kutoka mita 2,000 hadi mita 2,500.

Mhandisi Kedrick Chawe kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS), akionesha ramani ya Kiwanja cha Ndege cha Msalato kitakavyokuwa mara baada ya awamu ya kwanza ya ujenzi wake kukamilika kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati kamati hiyo ilipokagua eneo ambalo kiwanja hicho kitajengwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akisoma taarifa ya mradi wa barabara ya Iringa-Dodoma (Km 260) kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma, leo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Naghenjwa Kaboyoka, akikagua ubora wa lami katika eneo la Nkulabi, barabara ya Iringa-Dodoma (Km 260), wakati kamati hiyo ilipokagua barabara hiyo leo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi John Ngowi, akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), walipokagua barabara ya Iringa-Dodoma (Km 260).

Muonekano wa Barabara ya Iringa -Dodoma (Km 260) sehemu ya Migori- Fufu (Km 93.80) ambayo ujenzi wake umekamilika kwa kiwango cha lami.

TAA YASAIDIA MADRASAT ISTIQAAMA MISAHAFU.

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhandisi na Huduma za Ufundi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Mbila Mdemu (kushoto), akimkabidhi Katibu wa Madrasat-ul-Istiqama, Ustaadh Hemed Suleiman misahafu 29, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa wa Mamlaka hiyo, Richard Mayongela.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakishughudia Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhandisi na Huduma za Ufundi, Mhandisi Mbila Mdemu (kushoto) akikabidhi Katibu wa Madrasa ya Istiqama ya Buguruni, Ghana, Ustaadh Hemed Suleiman moja ya misahafu 29 waliyotoa msaada.
....................................


Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA  ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), leo imetoa vitabu vya dini aina ya misahafu 29 kwa Madrasat-ul-Istiqama ya Buguruni, Mtaa wa Ghana, kwa ajili ya watoto wanaosoma elimu ya dini ya Kiislam.


Akikabidhi vitabu hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Kaimu Mkurugenzi wa Uhandisi na Huduma za Ufundi, Mhandisi Mbila Mdemu amesema mbali na kazi za kuendesha, kusimamia na kuendeleza Viwanja vya Ndege Tanzania Bara, TAA imekuwa ikishirikiana na jamii katika masuala mbalimbali yanayohusu jamii.


Mhandisi Mdemu amesema pamoja na kwamba Madrasat hiyo ina watoto takribani 230, lakini anaamini wataweza kupokezana vitabu hivi na kupata mafunzo yaliyo sahihi, yatakayowajengea malezi bora yenye msingi wa amani na mshikamano.


Amesema msaada huu wa vitabu vya dini utasaidia kuanza kuwaandaa watoto hao, ambao baadaye wakiwa wakubwa wanakuwa ni sehemu ya jumuiya na sehemu ya Mamlaka na jamii nzima ya Kitanzania, ambapo watakuwa waadilifu na wenye maadili mema kwa taifa kwa kuwa wamepata msingi mzuri wa elimu ya dini, ambao ndio chimbuko la uadilifu na amani.


“Hii ni kawaida ya Mamlaka kutoa misaada kwa jamii, na ninaamini msaada huu pia utasaidia kufanya kitu kikubwa katika jamii yetu, kwa kuwa watoto hawa ndio watakuja kuwa watumishi wa miaka ijayo, hivyo watakuwa mfano wa kuigwa katika jamii,” alisema Mhandisi Mdemu.


Pia Mhandisi, amewakaribisha kutembelea TAA kwa ajili ya kujifunza na kuwa na ari ya kufanya kazi na Taasisi hii, ambayo ipo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi).


Naye Katibu wa Madrasat hiyo, Hemed Suleiman ameishukuru TAA kwa kujitoa kwao kwa kutoa msaada huo, ambao ni moja ya vitu muhimu kwao.


“Nawashukuru sana tena sana kwa msaada huu, hatuna cha kuwalipa ila Mungu awazidishie pale mlipotoa, muendelee kuwasaidia watu zaidi ya sisi” ameshukuru Bw. Suleiman.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS YOWERI MUSEVENI JIJINI KAMPALA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Africa Now Summit 2019 katika hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort mjini Kampala, Uganda. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MAGAZETI YA LEO MACHI 14, 2019