Monday, February 25, 2019

HALI YA UPATIKANAJI WA UMEME KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM

Februari 25, 2019
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi Wateja wake wa Mkoa wa Dar es salaam kwa kukosa huduma ya umeme kwa siku za hivi karibuni kutokana na maboresho makubwa yanayohusisha matengenezo kinga ya mashine 3 za Kituo cha Ubungo II, pamoja na uwekaji wa transfoma kubwa la MVA 300 kwenye Kituo cha kupoza umeme cha Ubungo ili kukiongezea uwezo na kwenda sambamba na ukuaji wa mahitaji ya jiji la Dar es Salaam.
 Kabla ya matengenezo kuanza mnamo Januari 2019 Kituo hiki cha kupoza umeme cha Ubungo kimekuwa kinapokea umeme kutoka katika vituo vya Uzalishaji umeme vilivyopo upande wa msongo wa kilovolti 220 kupitia transfoma mbili zenye uwezo wa MVA 150 kila moja, zenye kupokea umeme wa msongo wa Kilovolti  220 na kuushusha hadi kuwa msongo wa Kilovolti 132  katika transforma namba sita na namba  saba za kituo cha Ubungo na  vituo vya uzalishaji umeme vilivyoungwa kwenye msongo wa kilovolti 132 ambavyo vimeungwa moja kwa moja kwenye mfumo mkuu wa usambazaji umeme  kwa Dar es Salaam na Zanzibar.
Kutokana na matengenezo yanayoendelea vituo vya uzalishaji umeme vilivyoungwa kwenye msongo wa kilovoti 132 na 33 vimekuwa nguzo kubwa ya upatikanaji wa umeme. Vituo hivyo ni Ubungo II na Tegeta.
Shirika kupitia wataalamu wake tayari limefanya jitihada kubwa za kupunguza athari za upungufu wa upatikanaji wa umeme kwa wakaazi wa Dar es salaam na Zanzibar kwa kufanya yafuatayo: 
Mosi, Kufungua laini ya msongo wa kilovoti 132 kati ya Kilimanjaro na Hale: Hili hufanyika ili kutoruhusu umeme wa kutoka Dar es Salaam na Morogoro kwenda Kilimanjaro hivyo Mkoa huu kuchukulia kwenye upande wa msongo wa kilovolti 220 kutoka Arusha.
Pili , Kuwezesha upatikanaji wa umeme katika baadhi ya  maeneo ya Mkoa wa Dar es salaam, kwa kuunga baadhi ya njia za Usafirishaji  umeme kutoka Kituo cha Kinyerezi, Gongolamboto hadi Mbagala ili kuwezesha maeneo hayo kupata umeme bila kupitia kituo cha Ubungo  ambacho kipo katika matengenezo.
Tatu, Kufungua njia ya umeme ya kilovolti 132 itokayo Kituo cha Kunduchi   hadi Mlandizi na kuunga maeneo hayo katika njia ya umeme ya kilovolti 132 itokayo Morogoro ili kuwezesha jiji la Dar es salaam kuwa na umeme wa uhakika.
Nne, Kufungua laini ya msongo wa kilovolti 132 kati ya Ubungo na Chalinze upande wa Ubungo ili kutozihusisha transfoma za Ubungo kwenye mzigo wa mikoa mingine na hivyo kutumika kuhudumia  wateja wa  Dar es Salaam na Zanzibar pekee.
 Tunatarajia matengenezo haya yanayokwenda kwa awamu yatakamilika ifikapo mwezi Juni 2019.
TANESCO itaendelea kutoa taarifa ya Maendeleo ya kazi ya matengenezo ya kituo cha Ubungo yenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika Dar es salaam na Zanzibar kwa siku zijazo 
Kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100
Tovuti: www.tanesco.co.tz, 
Mitandao ya kijamii
Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,
 Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/
IMETOLEWA NA:
OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU

NCHI 50 BORA ZENYE MIFUMO IMARA YA UDHIBITI UBORA WA BIDHAA ZA VYAKULA NA DAWA

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akisema jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wataalam wa udhibiti ubora wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA na Wakala wa Chakula, Dawa na vipodozi Zanzibar (ZDFA) Jijini Dar Es Salaam.

Picha ya Pamoja wajumbe wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula (aliyeketi wa tatu kulia)

Na WAMJW- Dar es Salaam

TANZANIA yatajwa miongoni mwa nchi 50 kati ya 194 duniani zenye mifumo imara na madhubuti ya udhibiti wa ubora wa bidhaa za vyakula, dawa na vipodozi. 

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula leo wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano kwa wataalam wa udhibiti ubora wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi (ZDFA) na wenzao kutoka nchi ya Malawi. 

Mafunzo hayo maalum yameandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO-Tanzania) kwa lengo la kuwaongezea mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kuimarisha nchi hizo kuongeza nguvu ya udhibiti wa bidhaa hizo. 

“WHO imetutambua na imetupa level (daraja) la tatu, hii ni hatua nzuri, TFDA imefanya kazi kubwa, hii inamaanisha mifumo ya udhibiti tanzania inatambulika duniani kote na kwamba misingi ya udhibiti ya mamlaka yetu imefikia ngazi ya kimataifa". Amesema Dkt. Chaula na kuongeza “Lakini pamoja na hatua hiyo lazima iendelee kujiimarisha ili ikiwezekana tupande daraja tufikie level 4 ambayo ndiyo kiwango cha juu zaidi". 

“Ili tuweze kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi, mamlaka yetu inapaswa kutengeneza mifumo ya ufuatiliaji ubora na usalama wa bidhaa kuanzia viwandani hadi kwa mtumiaji, ili kuhakikisha hakuna dawa bandia zinaingia nchini mwetu”. 

Akiwasilisha mada Dkt. Alireza Khadem Broojerdi kutoka WHO amesema ili kuongeza nguvu ya udhibiti nchi zinapaswa kushirikiana kwa ukaribu. 

“Tunayo malengo 17 ya kidunia (SDGs), lengo namba tatu linasisitiza juu ya afya bora kwa wote, tunayo pia malengo ya mwaka 2019- 2030, mpaka sasa nchi 50 ikiwamo Tanzania sawa na asilimia 26 zimefikia daraja la tatu na nne. Nchi 45 sawa na asilimia 23 zipo daraja la pili, nchi 96 zimefikia daraja la kwanza na zingine zilizobaki bado hazijafikia viwango hivyo,” amesema Dkt. Khademu. 

Awali akizungumza Kaimu Mkurugenzi wa TFDA, Dkt. Candida Shirima amesema kupitia semina hiyo iliyoandaliwa na WHO watajifunza mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kuweza kufikia malengo waliyojiwekea katika kuendelea kuimarisha mifumo ya udhibiti wa bidhaa hizo.

TGNP YAZNDUA KAMPENI YA ULINZI WA MTOTO DHIDI YA UKATILI WA KINGONO- “1-5-5 NAMLINDA”

Anna Sangai akzungumza na waandishi wa habari kuhusu kampeni ya Ukatili dhidi ya watoto

Sehemu ya wageni waliohudhuria mkutano wa kampeni ya ulinzi wa mtoto dhidi ya ukatili wa Kingono

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

25 February 2019

KAMPENI YA ULINZI WA MTOTO DHIDI YA UKATILI WA KINGONO- “1-5-5 NAMLINDA”

Mlinde mtoto afurahie utoto wake, ujana wake na uzee wake”

Ukatili dhidi ya watoto umekuwa ni sehemu ya maisha ya  watoto wengi nchini. Mojawapo ya aina za ukatili unaokumba kundi hili  ni ukatili wa kingono.   

Mnamo mwaka 2011, nchi yetu ilitoa taarifa ya utafiti uliofanyika kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto, utafiti huo uligundua kuwa karibia mmoja kati ya wasichana watatu na mmoja kati ya wavulana saba wamekutana na ukatili wa kingono kabla ya kutimiza miaka 18. 

Hata hivyo, kulingana na utafiti huo, wengi wa watoto  hawatoi taarifa juu ya vitendo hivyo, wachache wanatafuta huduma  na wachache zaidi wanafanikiwa kupata matibabu au msaada wanapotoa taarifa ya matukio hayo. 

Pia, ripoti iliyotolewa na Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) zinaonyesha kuwa matukio ya ukatili wa kingono miongoni mwa watoto  yanaongezeka nchini. 

Kulingana na ripoti hiyo iliyotolewa Juni 2018, wastani wa watoto 394 wamebakwa kila mwezi katika maeneo mbalimbali Tanzania bara, huku ulawiti wa watoto ukiongezeka kutoka  matukio 12 kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2017 hadi matukio 533 kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2018, na mikoa inayoongoza kwa matukio hayo ni Dar es salaam na Iringa. 

Vitendo hivi havikubaliki katika jamii kwani ni kinyume cha haki za binadamu na mikataba mbalimbali ya kimataifa, na kikanda iliyoridhiwa na serikali juu ya ulinzi wa mtoto dhidi ya aina zote za ukatili wa kijinsia. Mikataba hiyo ni pamoja na Mkataba wa haki za mtoto wa mwaka 1989, tamko la Afrika juu ya haki na ustawi wa mtoto la mwaka 1990.

Vitendo hivi vinarudisha nyuma maendeleo ya mtoto na taifa kwa ujumla. Miongoni mwa athari zitokanazo na ukatili wa kingono dhidi ya watoto ni pamoja na watoto kuathirika kisaikolojia, maambukizi ya magonjwa ya zinaa na UKIMWI, mimba za utotoni, na kubwa zaidi ni kuhatarisha ustawi wa taifa na kuchochea uongezeko la vitendo hivi katika jamii.

Kutokana na takwimu hizo, hali ya tatizo ni kubwa sana, jambo ambalo limesukuma TGNP Mtandao kuja na kampeni ya ulinzi wa mtoto iitwayo 1-5-5 Namlinda. Kampeni hii inachangia katika jitihada za serikali kutokomeza aina zote za ukatili dhidi ya watoto kupitia Mpango wa Taifa wa Kutokomeza dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) unaolenga kupunguza ukatili dhidi ya wanawake na watoti kwa asilimia 50 ifikapo 2022.

Kampeni hii inalenga kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya athari za ukatili wa kingono kwa watoto na umuhimu wa kuwalinda dhidi aina hiyo ya ukatili, kutathmini na kuibua mijadala katika jamii juu ya hali halisi ya ukatili wa kingono, kuhamasisha jamii kuzuia vitendo hivi visitokee na kutoa taarifa mara  waonapo matukio hayo ya ukatili wa kingono kwa watoto ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua stahiki.

Kampeni hii pia inalenga kujenga nguvu za pamoja na wadau mbalimbali nchini katika kuweka mikakati ya pamoja ya ulinzi wa mtoto dhidi ya ukatili wa kingono na kuhakikisha kila mtu katika jamii anajisikia kuwajibika kumlinda mtoto. Hivyo, kampeni hii imelenga kuwafikia wanawake, wasichana, wavulana, wanaume, viongozi wa dini, serikali, jamii, vyombo vya habari, madawati ya jinsia polisi, asasi za kiraia, wadau wa maendeleo, makungwi, watoa huduma za afya,wanaharakati, watoa huduma za usafiri wa umma kama bodabodaa na daladala pamoja na wabunge, na wanasiasa.

Kampeni hii inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 27 Februari 2019 ambapo wawakilishi wa wadau mbalimbali ambao ni walengwa wa kampeni watashiriki  ili kupitishwa katika kampeni hii na kujadiliana kwa pamoja wajibu wa kila kundi katika ulinzi wa mtoto. Kampeni hii inatarajiwa kuzinduliwa rasmi na  mkuu wa jeshi la polisi Tanzania-IGP Saimoni Sirro.

Jamii inawajibu wa kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia. Hii ni kwa mujibu wa sheria ya mtoto na. 21 ya mwaka 2009 na mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto. 

TGNP Mtandao, inaamini kuwa  ikiwa kila mtu katika jamii atatimiza wajibu wake vizuri wa kumlinda mtoto, Tanzania billa ukatili wa kingono kwa watoto inawezekana. Pia, TGNP inaamini kuwa ikiwa watoto watakuwa huru dhidi ya aina zote za ukatili wa kijinsia, tutakuwa na taifa imara lenye viongozi bora, nguvukazi iliyo na afya njema na tutaweza kufikia malengo ya dunia ya maendeleo endelevu. Madai yetu katika kampeni hii ni pamoja na:- 

*      Kuitaka jamii kuguswa na tatizo la ukatili wa kigono kwa watoto wakiwa nje na ndani ya shule

*      Jamii ichukue hatua za kumlinda mtoto popote alipo. Kila mmoja alipo asimamie ulinzi wa mtoto 

*      vyombo vya habari vitoe elimu kwa wingi juu ya athari za ukatili wa kingono kwa watoto, faida ya kuwalinda watoto na kuendelea kukemea vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya watoto. 

*      Serikali kuu, serikali za mitaa na vyombo vya dola visimamie kikamilifu sheria ya kudhibiti uchawi na. 12 ya mwaka 1998(The Witchcraft Act). Ambayo imeainisha adhabu kwa watu wanaoendesha vitendo vya kishirikiana vinavyoweza kuwadhuru watoto na kuongeza vitendo vya ukatili wa kingono kama ubakaji. 

*      Tunatoa rai kwa jeshi la polisi  na vyombo vingine vya dola kama wadau wa kutekeleza MTAKUWAA (NPA) kuhakikisha watoto wanakuwa salama kwa kuimarisha ulinzi katika maeneo yote yanayotajwa kuwa sio salama kwa watoto nchini. 

*      Kupitia kampeni hii jamii yote, kupitia mtu mmoja mmoja na kikundi inapaswa kumlinda na kuhakikisha ustawi wa mtoto. 

*      Tunaitaka serikali na wadau kuzijengea uwezo kamati za ulinzi wa watoto ili waweze kutimiza majukumu yao ikiwemo kubaini maeneo hatarishi katika kijiji/ mtaa na kupanga mikakati ya kupunguza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Imetolewa na

Lilian Liundi

Mkurugenzi Mtendaji

TGNP Mtandao.

Kwa mawasiliano:Wasiliana nasi kupitia idara ya mawasiliano na habari

1.      Monica John

Simu: 0652 267 611 Email: monica.john@tgnp.org

2.      Jackson Malangalila

Simu: 0657 479 490 Email: Jackson. malangalila@tgnp.org

Saturday, February 23, 2019

Wanafunzi wenye mahitaji maalum wapewa misaada Lindi

https://i1.wp.com/dar24.com/wp-content/uploads/2019/02/mJUMBE.jpg?resize=1140%2C640

Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama cha mapinduzi CCM Manispaa ya Lindi, Hamida Abdala

 Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama cha mapinduzi CCM Manispaa ya Lindi, Hamida Abdala, ametoa msaada kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Mpilipili iliyopo Lindi Mjini.

Ametoa msaada wa viroba 3 vya unga, kiroba 1cha Sabuni, Maharage, Maziwa na Madaftari kwa wanafunzi wenye uhitaji maalumu ikiwa ni njia mojawapo ya kuwapa moyo wa kujiona wapo sawa na wanafunzi wengine na kuwapa moyo wa kupenda shule bila kujali mazingira wanayoishi.

Aidha Mbunge huyo amesikitishwa na uchakavu wa jengo linalotumiwa na wanafunzi hao na kusema atakutana na Mkurugenzi wa Manispaa waweze kuweka mazingira mazuri na kuahidi kuongeza madawati wanafunzi hao.

“Nasikitika kuona uchakavu wa darasa licha ya kuwa ni moja ambalo tumeshindwa kulisimamia na naahidi nitakutana na Mkurugenzi wa Manispaa ili tuweke katika hali nzuri na yenye usalama kwa maendeleo yenu kitaaluma,” amesema Mbunge huyo .

Ametaja changamoto nyingine ya upungufu wa madawati na ameahidi kuitatua na amewaomba viongozi wengine wawe na hali ya kutembelea mashule mbalimbali ili waweze kugundua changamoto zinazowakabili wanafunzi ili zitatuliwe na wanafunzi wapate matokeo mazuri kwenye mitihani yao.

Kwa upande wake mwl. Fadhili Saidi Mtitima ametoa pongezi kwa Mbunge wa viti maalumu kwa kuwapatia zawadi licha ya kusahaulika kwa kundi hilo lenye uhitaji maalumu na ametaja idadi ya wanafunzi hao jumla ni 32 huku wasichana wakiwa 10, wavulana 22 na hali ya kitaaluma wapo vizuri hivyo ameomba wazazi wawapeleke watoto wao wasiwafiche majumbani waende wakapate elimu yao ya msingi

MAKAMU WA RAIS ASEMA WAFANYABIASHARA NDOGO WASIOTAKA KUCHUKUA VITAMBULISHO WATAHESABIKA KAMA WAFANYABIASHARA WANAOPASWA KULIPA KODI

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amewataka wafanyabiashara wadogo kulipia na kuchukua vitambulisho maalumu vilivyotolewa na Serikali kwa ajili yao vinginevyo vitahesabika kuwa ni wafanyabiashara wakubwa wanaopaswa kulipia kodi.

Hatua itasaidia kuwatambua na kuepusha usumbufu wakati wa kufanya shughuli zao za kujiletea maendeleo.

Makamu wa Rais alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara katika  uwanja wa TASAF wilayani Sikonge ikiwa ni siku tatu ya ziara yake mkoani Tabora.

Alisema mfanyabiashara ndogo ndogo asiyetaka kulipia shilingi 20,000/- za kitambulisho maalumu atahesabika kuwa yeye anapaswa kukata leseni na kulipa kodi kama walivyo wafanyabiashara wakubwa.

Makamu wa Rais aliongeza kuwa kama shilingi 20,000/- zinaonekana ni nyingi kwa baadhi ya wafanyabiashara wadogo kulipa kwa mkupuo, uongozi wa Mkoa, Wilaya unaweza kuweka utaratibu ambao utawawezesha kulipa kwa awamu.

Alisema mfanyabiashara huyo anaweza kulipa kwa awamu mbili au tatu na akishamaliza malipo anakabidhiwa kitambulisho chake.

Aidha Makamu wa Rais alitoa angalizo kwa viongozi wa Mamlaka ya Mikoa na Serikali za Mitaa kuhakikisha hakuna Mfanyabiashara atakayepewa kitambulisho kabla ya kumaliza malipo yote kuwa upo uwezekano wa kutoroka na kwenda Mkoa mwingine na kuendesha shughuli zake kwa kutumia kitambulisho ambacho bado anadaiwa.