Sunday, November 11, 2018

DC. MOHAMEDI UTALY AWAONYA WAFUGAJI.

MKUU wa Wilaya ya Mvomero Mkoa wa Morogoro Mohamed Utaly, akizungumza na wafugaji kijiji cha Sokoine kata ya Dakawa wilayani Mvomero.
.........................................................
 
Na Omary Mngindo, Mvomero

MKUU wa Wilaya ya Mvomero Mkoa wa Morogoro Mohamed Utaly, amewataka jamii ya Wafugaji wilayani humo kuacha tabia ya kutaka kushindana na Dola, kwani hatua hiyo ni ya hatari kwa maisha yao.

Utaly ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wafugaji wanaounda umoja wao Kanda ya Mashariki, kwenye Mkutano uliofanyika Kijiji cha Sokoine, Kata ya Dakawa wilayani hapa, ambapo alisema kuwa baadhi ya wafugaji hawaiheshimu dola.

Wafugaji wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Morogoro Shamba Lingido, Naibu Katibu Mkuu wa chama cha wafugaji Taifa Joshua Lugosi na Olnjurie Marigwa Mwenyekiti wa wafugaji Mkoa wa Pwani, Utaly amewataka viongozi wa jamii hiyo kuwaonya vijana wao.

Alieleza kuwa siku moja mfugaji jamii ya Morani, alikatazwa asiingize mifugo kwenye shamba, ambapo baada ya hatua hiyo alitaka kupambana na askari Polisi aliyekuwa na siraha, tukio ambalo askari alimtaka mfugaji huyo atulie, lakini cha kusikitisha hakutii amri hiyo.

"Nampongeze askari aliyekutwa na tukuo hilo, alimzuia amsimfuate kwa kuwa alikuwa siraha mkononi, cha kusikitisha Morani huyo akiwa na mkuki mkononi, alikuwa anakwenda kwa kasi akimfuata askari lengo kutaka kumnyang'anya siraha," alisema Utaly.

Akaongeza kuwa askari baada ya kumuona Morani huyo hatii amri, akapiga risasi moja juu kama kumtisha, lakini hakutii, huku akimfuata kwa kasia, kaongeza nyingine mbili ndipo yeye na wenzake wakageuka na kuanza kukimbia.

Nae Inspekta Emmanuel Mphuru Msaidizi wa Mkuu wa Kituo aliyemwakilisha Mkuu wa Polisi wilaya (OCD) alisema kuwa kitendo cha jamii hiyo kupuuza amri za polisi no kujitakia matatizo, hivyo ni vema wakatii amri.

Akizungumzia tukio hilo, Lingindo amesema kuwa wamesikitishwa kuwepo kwa tukio hilo, na kwamba watakaa na viongozi wao kuona ni namna gani wanavyoweza kulizungumza kwa lengo laondoa hali hiyo.

Watumishi waliofutana na Mkuu wa wilaya wakifuatilia mazungumo ya mkutano huo.

Wafugaji wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Mohamed Utaly

Mwenyekiti wa Wafugaji Mkoa wa Pwani, (kulia) akifuatilia mkutano huo kwa kunukuu mambo muhimu yaliyokuwa yakizungumzwa.


Pichani kutoka kushoto Mwenyekiti wa Time, Veronica Ndetiai Kindeti, letoni Leboi Mwenyekiti wa Wafugaji Kanda na Shamba kubwa Mwenyekiti wa Wafugaji Mkoa wa Morogoro, Picha zote na Omary Mngindo.

MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 11, 2018.

DAWASA YAWAVUTIA MAMIA KUREJESHEWA HUDUMA YA MAJI

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) imefanikiwa kuvutia mamia ya Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuomba kurejeshewa huduma ya maji safi baada ya huduma hiyo kusitishwa hapo awali kutokana na wateja hao kushindwa kulipa madeni ya  ankara za maji kwa kipindi kilichopita.

Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa wananchi wote waliokatiwa  maji kwa muda mrefu kufika katika Ofisi za DAWASA zilizopo katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na Viunga vyake pamoja na Kibaha na Bagamoyo Mkoani Pwani ili taratibu za kuwarejeshea maji zifanyike.

Akizungumzia lengo la Mamlaka hiyo Mhandisi Luhemeja amesema kuwa ni kuhakikisha kuwa inaongeza wateja  na pia kuwarejesha wale waliokatiwa maji kwa muda mrefu baada ya kushindwa kulipa bili zao ambapo sasa wataingia makubaliano maalum na Mamlaka hiyo yatakayowawezesha kupata huduma ya maji na kuendelea kulipa deni  kidogo kidogo kulingana na makubaliano hadi watakapomaliza madeni yao.

Hatua zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo katika kuboresha huduma zake ni pamoja na kuvutia wateja wapya na kurejesha wale waliokatiwa maji kwa muda mrefu.

Sehemu ya Taarifa ya Mamlaka hiyo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Tweeter  inasema kuwa wananchi wameonesha mwitikio mkubwa katika maeneo yote yanayohudumiwa na DAWASA hasa kwa kuwasilisha maombi ya kurejeshewa huduma hiyo.

“ Kutoka mkoa wa Kinondoni wateja zaidi ya 50 wamejitokeza kuomba kurejeshewa huduma ya maji safi na salama hivyo ni mwanzo mzuri kutokana na mwitikio huu ambao umeonesha wazi kuwa wananchi wanaunga mkono juhudi za Serikali kuhakikisha wanafikiwa na huduma bora”; inasisitiza sehemu ya taarifa ya Mamlaka hiyo.

Hatua  nyingine zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo ni pamoja na kudhibiti mivujo ya maji, kufikisha huduma ya maji maeneo ya pembezoni na pia kuhakikisha kuwa maeneo ya viwanda yanafikiwa na huduma hiyo ili kuchochea uchumi wa viwanda.

DAWASA imekuwa ikitekeleza miradi yakimkakati inayolenga kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafikiwa na huduma ya majisafi na salama katika Jiji la Dar es Salaam na Pwani tangu Mamlaka hiyo ilipoundwa upya baada kuvunjwa kwa DAWASCO hivi karibuni na majukumu yake kuhamishiwa DAWASA.