Wednesday, November 7, 2018

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” jijini Dodoma.
...............................


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo kwa kila Mkuu wa Mkoa aifanye afya ya uzazi na mtoto kuwa ajenda ya kudumu katika vikao vya ushauri vya Mkoa (RCC).

Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” ya Kuongeza kasi ya Uwajibikaji Kupunguza Vifo Vitokanavyo na Uzazi na Watoto Wachanga.

“Ili kuhakikisha suala la kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto katika nchi yetu linapewa kipaumbele cha juu katika shughuli za Serikali za kila siku” alisema Makamu wa Rais

Tafiti zilizofanyika mwaka 2015/2016 zinaonyesha kuwa, kiwango cha vifo vitokanavyo na uzazi ni 556 kwa kila vizazi hai 100,000 ambayo ni sawa na vifo 11,000 kila mwaka ambayo ni sawa na wanawake 30 hufariki kila siku, kutokana na matatizo yatokanayo na uzazi na kwa uapnde wa watoto wachanga ni 25 kwa kila vizazi hai 1000 .

Makamu wa Rais amesema jamii ina jukumu zito la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kwa kuhakikisha kuwa inajiwekea mpango mahsusi wa rufaa wakati wa dharura na utambuzi wa dalili hatarishi kwa mama na mtoto mchanga.

“Nitoe rai kwa wananchi, wanawake na wanaume na vijana kujitokeza kuchangia damu mara kwa mara kwa kuwa wakifanya hivi wanaokoa maisha ya mama mjamzito na watoto.” Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 80 ya damu salama inatumika kwa wakina mama wajawazito na watoto alisema Makamu wa Rais.

Kauli mbiu ya kampeni hii “Jiongeze: Tuwavushe Salama” inaaminika inaaminika italeta matokeo chanya katika kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga nchini.

Kwa Upande mwingine Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  alimshukuru Makamu wa Rais kwa kukubali kuwa mlezi wa kampeni hiyo ambayo itatekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja, pia alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa kipaumbele kwa afya ya Mtanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionesha taarifa inavyoonyesha hali halisi ilivyo sasa katika masuala yanayohusu uzazi salama wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi vitendea kazi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
  
Sehemu ya Wageni kutoka Taasisi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi vitendea kazi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Binilith Mahenge  (kushoto) mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” jijini Dodoma.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

ARUMERU YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YAANZA KUONEKANA*

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru *Mhe. Jery Muro* amejitolea  kuwasadia kuandika Maandiko ya kibiashara wananchi wanaotaka kufanya Kilimo na Ufugaji wa Kibiashara ili waweze *KUKOPESHEKA* na taasisi za Kifedha ambazo kabla ya kutoa msaada au mkopo huitaji mchanganuo au Andiko la kibiashara kwanza kabla ya kuwawezesha wananchi ambao wanataka kuanza kilimo au ufugaji wa kibiashara.

Mhe Muro amefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwepo Kwa *VIKWAZO* vya maandiko ya Mradi katika hatua za awali Pinda *wananchi* wenye nia ya kuanzisha kilimo na ufugaji wa kibiashara wanapoanza safari ya kutimiza *ndoto* zao za kuwekeza katika sekta hizo, ambapo baada ya kubaini uwepo wa *vikwazo* hivyo aliamua kujiongeza Kwa kutafuta wadau ambao atashirikiana nao katika kuwasaidia *wananchi* kuondoa Vikwazo hivyo.

Mhe Muro amesema *tayari* kampuni Binafsi ya Wawezeshaji wa wakulima *( PASS)* Private Agricultural Sector Support imekubalKuwaandalia na kugharamikia Mpango Kazi wa kibiashara *( Bussiness Planning )* zitakazowasaidia Wakulima na Wafugaji katika kupata Mkopo katika Taasisi za Kifedha hali ambayo itawasaidia katika uendelezaji wa Kilimo chenye tija na ufugaji wa kibiashara. 

Hatua hiyo imefikiwa mara baada ya Mhe Muro kufunga *MAONYESHO YA JUKWAA LA WAKULIMA MERU* ambayo yamefanyika Kwa siku tatu na kuwaleta pamoja wakulima, wafugaji na wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo na mifugo ambapo pamoja na kukubali kutoa msaada wa BURE katika kuandaa na kuandika maandiko ya mchanganuo wa kibiashara pia amewapatia chumba Cha ofisi ya kuratibu na kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji *JUKWAA LA WAKULIMA MERU* ili kuwawezesha kufanya kazi zao Kwa Haraka zaidi, na kuhaidi kuwatafutia Computer Kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu Za taarifa za wakulima na wafugaji.

Kwa upande Meneja wa Tawi la kampuni ya *( PASS)* amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru MHE Jerry Muro Kwa kuonyesha kuwajali wakulima na wafugaji ambapo amewataka wananchi hao Kujitokeza kwa wingi ili waweze kunufaika kupitia na Taasisi hiyo. 

*Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru*