Friday, February 9, 2018

JESHI LA POLISI LATAKIWA KUZIACHIA PIKIPIKI ZILIZOSHIKILIWA KWA MUDA MREFU.



 WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba akikagua pikipiki ambazo zimeshikiliwakatika kituo cha polisi pangani. ameagiza polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa mda mrefu na zina makosa madogo waziachie na wasikae nazo kwa mda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu.
…………………………………………
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amelitaka jeshi la polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa mda mrefu na zina makosa madogo waziachie na wasikae nazo kwa mda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu.

Dk Mwigulu amesema yale yenye makosa makubwa kama uhalifu wa kivita, madawa ya kulevya, na wale wanaotelekeza wabaki nazo na wafanye utaratibu wa kuwapeleka mahakani au kuziteketeza na zenye makosa madogo wazitatua haraka na kuwarudishia na kuwapa elimu wamekosea wapi.

“Wapeni masomo wamekosea wapi walekezeni na waliowabishi waelekebisheni lakini tusirundike tukatengeza vyuma chakavu kwa hivi vitu ambavyo utatuzi wake tunawo, tutumie huu mkono wakutatua kwa yale ambayo yapo ndani ya mamlaka yetu” alisema Dk Mwigulu

Alisema kuwa ipo haja ya vijana sasa kufundishwa zaidi kuhusu sheria ya usalama barabarani ili kupunguza ajali ya pikipiki na mlundikano wa pikipiki katika vituo vya polisi nchini kwani kila napopita kita vituo vya polisi hukuta pikipiki ni nyingi na makosa yao ni madogomadogo.


Tuesday, February 6, 2018

RAIS MAGUFULI AZINDUA KITUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI BAGAMOYO.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani. 

Wa kwanza kushoto anayevuta utepe ni Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mafunzo kutoka tume Kuu ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian. Februari 6,2018.


RAIS DKT. SHEIN AFUNGUA MAHAKAMA YA WILAYA YA MWANAKWEREKWE.



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kulifungua jengo jipya la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Unguja,kushoto Waziri Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria na Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Haroun Ali Suleiman na kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Makungu na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akitowa maelezo wakati wa uzinduzi huo ya jengo jipya la mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Unguja.
BAADHI ya Majaji na Mahakimu wa Mahakama za Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa jengo hilo

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Zanzibar.

JAJI Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo jipya la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Zanzibar kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,kuhutubia hadhara hiyo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jengo la Mahakama ya Wilaya Mwamakwerekwe Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe Zanzibar baada ya uzinduzi wa jengo hilo.(Picha na Ikulu

RC NDIKILO AIAGIZA CBT KUMLIPA MALIPO YA AWALI MKANDARASI WA GHALA LA KOROSHO MKURANGA



MKUU wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo,(kulia)akielekeza jambo baada ya kuonyeshwa ramani ya ghala  la  korosho  ambapo linatarajia kujengwa huko Mkuranga, wakati alipokwenda kutembelea ujenzi wa  ghala hilo .
.............................................

Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga
MKUU wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameiagiza bodi ya Korosho Tanzania (CBT) kuhakikisha inamlipa ,malipo ya awali kiasi cha sh.bilioni 1.6, mkandarasi wa ghala la kuhifadhia korosho wilayani Mkuranga.

Alitoa agizo hilo ,wilayani Mkuranga alipotembelea ujenzi wa ghala hilo linalojengwa na kampuni ya BQ Contractors Ltd .

Alieleza kabla ya ujenzi waliingia mkataba wa kulipa asilimia 30 ya malipo ya awali ya ujenzi wa ghala hilo la kisasa ambalo litagharimu kiasi cha shilingi bilioni 5.5 hadi kukamilika kwake.

Aidha Ndikilo alisema, kampuni hiyo ilitoa malalamiko kuwa zimepita siku 52 wakiwa hawajapewa hata shilingi moja kwa ajili ya ujenzi huo hali ambayo inasababisha ujenzi huo kuwa mashakani kukamilika kwa wakati.

“CBT ihakikishe inatoa fedha hizo ndani ya wiki hii, bodi ya korosho ambao ndiyo wamiliki wa ghala hilo na endapo watashindwa kufanya hivyo atawapeleka kwa Waziri Mkuu kwa ajili ya hatua zaidi”;
“Mkurugenzi wa bodi hiyo itabidi wakutane Dodoma kwa ajili ya kueleza ni sababu gani inawafanya washindwe kumlipa mkandarasi huyo,” alisema Ndikilo.

Alisema serikali kwa kushirikiana na bodi ya korosho walikubaliana kujenga ghala hilo ili kuwe na ghala moja kwa kila wilaya tatu za Mkuranga, Kibaha na Rufiji ambako ndiko zinalimwa korosho nyingi.
Ndikilo alieleza lengo la  kuwa na ghala la  uhakika ni kufanikisha mfumo wa stakabadhi ghalani.

“Kuanzia msimu ujao korosho zote zitauzwa kwenye ghala moja kubwa badala ya kutumia maghala ya watu binafsi ama ya vyama vya msingi vya ushirika ambao wanaonekana kufanya hujuma kwa kuweka korosho ambazo hazina viwango ,:;ambapo kwa msimu huu tatizo lilikuwa kubwa sana,” alifafanua Ndikilo.

Hata hivyo ,alieleza kutotolewa fedha hizo kutasababisha ujenzi huo kutokamilika kwa wakati kutokana na hali ya mvua za masika unaokuja ambazo zitasababisha ujenzi huo kushindwa kufanyika katika kipindi lengwa.

Nae mwakilishi wa bodi ya korosho Japhari Matata alikiri kucheleweshwa kwa fedha hizo .

Alisema kwasasa taratibu za kuzipata fedha hizo zinaendelea ili kumpatia mkandarasi huyo.

Matata alisema atalifikisha suala hilo kwa wahusika kwa ajili ya kuhakikisha  linafanikiwa ili ujenzi huo ukamilike mwezi wa  nane  kipindi ambacho ndicho ilipangwa ukamilike.

Awali akitoa taarifa kuhusu ujenzi huo, meneja wa maendeleo ya biashara wa kampuni hiyo Hilu Bura, alisema changamoto kubwa ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya ujenzi huo ambao ulianza Oktoba mwaka jana.

Alitaja changamoto nyingine ni eneo hilo kuwa na maji kwa wingi hivyo endapo fedha zitachelewa kutasababisha kujenga kipindi cha mvua za masika ambacho kinakaribia kuanza.

Bura alimuomba mkuu wa mkoa huyo wa Pwani kuwasaidia ili waweze kupatiwa fedha za awali.

CCM BAGAMOYO IMEUFUTA WARAKA UNAOWAKATAZA WASIHOJI WATENDAJI WA SERIKALI



MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)wilayani Bagamoyo,alhaj Abdul Sharif ,akizungumza na wanachama wa chama hicho na baadhi ya wananchi (hawapo pichani) huko kata ya Miono wilaya Bagamoyo.
......................................

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Bagamoyo,alhaj Abdul Sharifu amefuta waraka uliotolewa wilayani hapo, ambao unakataza viongozi wa chama kutokuwa na fursa ya kuwahoji watendaji wa serikali.   
   
Aliyasema hayo baada ya kufanyika sherehe za miaka 41 ya CCM katika kata za Mbwewe, Miono na Lugoba .

Alhaj Sharifu alisema waraka huo unasababisha baadhi ya watendaji kutowajibika ipasavyo kwa wananchi.

Alielezea waraka huo unaonekana una maslahi ya watu binafsi ambao unakwenda kinyume na maslahi ya wananchi hivyo hauna manufaa yoyote zaidi ya kuwakandamiza wananchi.

“Naufuta maana haiwezekani watendaji wa serikali waachwe wafanye wanavyotaka hata wakiharibu tusiwahoji ,wakati chama kina wajibu wa watendaji wa serikali ,” alisema Sharifu.

Aidha Sharifu alisema,baadhi ya mambo yamekuwa hayaendi kutokana na watendaji hao kujisahau na kushindwa kutekeleza majukumu yao kwani hakuna watu wa kuwahoji.

“Kila siku Rais anasisitiza chama ndiyo kimeunda serikali hivyo watendaji wake lazima wasimamiwe na chama ,hatuwezi kuona mambo yanaharibika halafu tukae kimya ikifika nyakati za uchaguzi tunaonekana hatujafanya lolote,Hili halikubaliki,” alisema Sharifu.

Alisema ilani inayotekelezwa ni ya CCM hivyo lazima viongozi wa CCM wasimamie watendaji na hata ikiwezekana kuwaondoa wale ambao wanashindwa kuwajibika kwenye nafasi zao.

Nae mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Abubakary Mlawa alisema wamejipanga vizuri kuhakikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi inakamilika kwa muda uliopangwa.

Mlawa alisema kuwa jumuiya zote za chama zimeungana kuhakikisha zinawatumikia wananchi kwa kuhamasisha masuala ya maendeleo na kuibua miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na elimu, afya, maji, barabara, kilimo na mifugo.

Friday, February 2, 2018

JUMUIYA YA KOREA YATOA MSAADA WA KISIMA KEREGE BAGAMOYO.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wa Korea kusini, mama Lee Hae Meng, (kulia) mwenye kofia pembeni yake ni Diwani viti maalum Magomeni, Shumina Rashidi wakizindua kisima cha maji shule ya msingi Kerege wilayani Bagamoyo.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wa Korea kusini, mama Lee Hae Meng, akiwa na viongozi waandaamizi wa jumuiya hiyo wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kisima cha maji kilichochimbwa Shule ya Msingi Kerege.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wa Korea kusini, mama Lee Hae Meng, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kisima kilichochimbwa kwa msaada wa jumuiya ya watu wa korea kusini katika shule ya msingi Kerege.
.............................................

Jumuiya ya watu wa korea kusini waishio Tanzania na Afrika kwa ujumla wametoa msaada wa visima katika shule za msingi Kerege na Mapinga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, mam Lee Hae Meng ambae ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alisema wamefikia uamuzi huo ili kusaidia maeneo yenye shida ya maji hasa katika maeneo ya shule.

Alisema wameguswa na mazingira ya shule msingi Kerege na hivyo kuamua kujitolea katika kusaidia kisima cha maji ili wanafunzi katika shule hiyo waondokane na adha ya kutafuta maji.

Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kerege Ester Afia Awino alisema wanaishukuru jumuiya hiyo kwa msaada huo wa maji kwani ni miongoni mwa matatizo yaliyokuwa yanaikabili shule hiyo.

Alisema pamoja na kupata maji bado shule hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa ambapo alisema kwa sasa shule hiyo yenye wanafunzi 1,129 ina upungufu wa vyumba vya madarasa sita.

Alisema hali hiyo imetokana na ongezeko la wanafunzi waliojitokeza kuandikishwa shule katika kipindi hiki ambacho serikali imetangaza Elimu bure.

Akizungumzia hali ya taaluma ya shule hiyo, Kaimu Afisa Elimu Msingi, Alex Mwakawago alisema shule hiyo ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri kitaaluma hivyo kuindolea changamoto ni kuisaidia katika kuku taaluma.

Alisema upatikanaji wa maji katika shule hiyo kutaongeza ari kwa wananfunzi na kupata muda mzuri wa masomo na hatimae kuongeza kiwango cha taaluma.

Nae Diwani wa kata ya Kerege ambae pia ni Makamo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Saidi Ngatipula lisema anaishukuru jumuiya hiyo ya watu wa korea kusini kwa msaada wa visima ambapo umepunguza adha ya maji katika eneo la Kerege.

Alisema Jumuiya hiyo kwa sasa imechimba visima vitatu ndani ya kata ya Kerege ambapo ni shule ya msingi Kerege, Shule ya Msingi Mapinga na Shule ya Sekondari Kerege.

Aidha, alisema kuwa, wanathamini msaada huo na kwamba watavitunza visima hivyo ili waendelee kufaidika navyo kwa sku nyingi zaidi.
Diwani wa kata ya Kerege ambae pia ni Makamo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Saidi Ngatipula, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuzindua kisima shule ya msingi Kerege wilayani Bagamoyo.
 Kutoka kulia ni Diwani wa kata ya Kerege ambae pia ni Makamo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Saidi Ngatipula, katikati ni Diwani wa viti Maalum Shumina Rashidi na wa kwanza Kushoto ni Diwani wa viti maalum Tarafa ya Yombo, Togo Malihega, wakishuhudia uzinduzi wa kisima cha maji shule ya msingi Kerege.
Kaimu Afisa Elimu Msingi, Alex Mwakawago akizungumza wakati wa uzinduzi wa kisima shule ya msingi Kerege.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Juliasi Mwang'anda akimkaribisha mgeni rasmi.

BAKHRESA AANZA KUPANDA MIWA BAGAMOYO KWAAJILI YA KIWANDA CHA SUKARI.


Baadhi ya miche ya miwa ikiwa katika kitalu tayari kwa kupandwa katika shamba la Bagamoyo Sugar mwishoni mwa wiki.
Mtaalam mzawa wa kufunga mabomba ya maji ya umwagiliaji miwa katika shamba la Bagamoyo Sugar Bi. Gloria Mmasi akiendelea na shughuli za ufungaji wa mabomba katika shamba hilo tayari kwa kuanza kuotesha miwa.
..............................................

Agizo la Rais John Pombe Magufuli la kuipatia Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) Group LTD ardhi yenye ukubwa wa ekari 10,000 kwa ajili ya kuwekeza katika kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari katika Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani limetekelezwa.

Msemaji wa Makampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) Group LTD, Bw Hussein Sufian ameiambia Idara ya Habari (MAELEZO) leo katika mahojiano maalumu ilipokuwa ikifuatilia utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli alilolitoa tarehe 6 Oktoba, 2017 baada ya kufungua kiwanda cha vinywaji baridi cha  Kampuni hiyo kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani.

Bw. Sufian amesema, tayari Kampuni yake imetenga takriban Shilingi Milioni 75/- kwa ajili ya kuanza uwekezaji katika shamba hilo kwa shughuli za kilimo cha miwa na kufafanua kuwa, hatua ya awali ya upandaji wa miwa kwenye vitalu imeanza.

 Amesema, maandalizi ya upandaji wa miwa katika Kitalu A chenye ekari 48 umekamilika. Aidha, upandaji wa miwa katika eneo la jumla ya ekari 8 kati ya hizo utaanza tarehe 3 Februali na ekari nyingine 40 utafanyika mwezi Juni na Julai, 2018.

“Baada ya kukamilika kwa upandaji katika Kitalu “A” mwaka huu (2018), tunatarajia ifikapo Januari na Juni 2019 tutaendelea kupanda miwa kwenye kitalu “B” chenye ukubwa wa ekari 300. Mzunguko huo utaendelea hivyo hivyo mpaka kufikia hekari 2030 ambazo tumekusudia kuanza ujenzi wa kiwanda mapema 2019 na uzalishaji wa sukari kiwandani ifikapo Septemba 2020, “alisema Bw. Sufian.

Akielelezea zaidi juu ya mradi huo, Bw. Sufian amesema kwamba tayari watu 50 wameajiriwa, kati ya hao 20 ni wa kudumu na 30 vibarua. Watu 5 wanafanya kazi za kiufundi na 45 nguvu kazi. 

Aidha, Kampuni hiyo imeajiri Wataalamu 2 kutoka nje ambao ni Bw. Abraham Star Mtaalamu wa Umwagiliaji kutoka Israel na Mtaalamu wa Kilimo cha miwa kutoka India, Bw Narayan Krishna, kiwanda kinakusudia kuajiri watu 1000 ifikapo mwaka 2020.

Ili kilimo hicho cha miwa kiwe endelevu,  pamoja na mambo mengine uchimabji wa visima na utengeneaji wa mabwawa matatu umefanyika ambapo maji yanavutwa kutoka mto Wami kilometa 5 mpaka katika bwawa lililotengenezwa la Tambezi 1.

Maji yanapojaa yanavutwa kupelekwa bwawa dogo katika Kitalu A na sehemu ya mitambo ya  kuchuja maji, ambapo kila Kitalu kitakuwa na kituo cha kusukuma maji na kupeleka kwenye mabomba makubwa kisha madogo yanayopita katikati ya mimea iliyopandwa na kufanya umwagiliaji wa matone.

Agizo la Rais Magufuli lilikusudia kuondoa pengo la uzalishaji wa sukari kwa matumizi ya kawaida nchini ambapo katika kipindi cha mwaka 2016/ 2017 mahitaji yalikawa ni tani 590,000 kati ya hizo tani 135,000 ni mahitaji ya kiwandani na 455,000 ni mahitaji ya kawaida ya binadamu.

Uzalishaji wa sukari nchini ulikuwa tani 350,846 na kufanya kuwa na upungufu wa tani 259,156.  Hivyo uzalishaji wa tani elfu 30 mpaka 70 utaondoa pengo la uhaba wa sukari nchini Tanzania.
Eneo la shamba la Bagamoyo Sugar litakalo oteshwa miwa likiwa katika hatua za awali tayari kwa kuoteshwa miwa mwishoni mwa wiki.
Mtaalam mzawa wa upandaji miwa katika shamba la Bagamoyo Sugar akionesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ya kuapanda miwa.
Baadhi ya wafanyakazi wa shamba la Bagamoyo Sugar wakiendelea na maandalizi ya shamba tayari kwa kuotesha miwa.
Mmoja wa wafanyakazi wa shamba la miwa akimwagilizia baadhi ya miche ya miwa tayari kwa kuoteshwa katika shamba la Bagamoyo sugar.

Thursday, February 1, 2018

UWT KEREGE WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA UJENZI WA KITUO CHA AFYA .

Diwani wa viti Maalum Tarafa ya Yombo, Togo Malihega (kulia) akiongoza kina mama wa UWT kata ya Kerege walipotembelea ujenzi wa kituo cha Afya Kerege, leo Tarehe 01 February 2018.
...........................................................

Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) kata ya Kerege Wilayani Bagamoyo wametembelea kituo cha Afya Kerege kujionea ujenzi wa kituo hicho.

Umoja huo wa Wanawake wa Tanzania katika kutembelea kituo hicho wamepata nafasi ya kufanya usafi katika kituo hicho ambacho kinaendelea na ujenzi kwa sasa.

Aidha, walisema wanamipongeza Serikali chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kutenga fedha kwaajili ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya mbacho awali ilikuwa ni Zahanati.

Walisema ujenzi wa kituo hicho cha Afya utasaidia kinamama wa kata ya Kerege na maeneo ya jirani kupata huduma ya uzazi karibu ukilinganisha na sasa ambapo hulazimika kufika Hospitali ya wilaya kwaajili ya huduma hiyo.

Walisema kwa muda mrefu wananchi wa Kerege na maeneo ya jirani wamekuwa wakipata tabu kujifungua huku wengine wakipoteza maisha kutokana na umbali wa kufuata huduma ya uzazi.

Waliongeza kwa kusema kuwa ujenzi wa kituo hicho cha Afya kata ya Kerege ni kielelezo tosha cha kuona Serikali ya chama cha Mapinduzi inasimamia ilani yake hali inayopelekea kuweza  kutekeleza miradi mbali.

Walisema kufuatia Ujenzi huo ni wazi kuwa wananchi wataendelea kujenga imani na Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake kutokana na utekelezaji wa ahadi zake kwao.

Mtaalamu wa Ujenzi kutoka Ofisi ya Mhandisi wa wilaya, Sikutegemea Daudi alisema majengo hayo yapo katika hatua za mwisho kukamilika na kwamba hivi karibuni majengo hayo yatakabidhiwa ili yaanze kazi.

Ujenzi wa kituo cha Afya Kerege ni mpango wa serikali katika kuhakikisha inaongeza vituo vya Afya nchini ambapo kata hiyo ni miongoni mwa kata zilizopata fedha za ujenzi huo.

Majengo yaliyojengwa mpaka sasa ni jengo la wodi ya wazazi, jengo la upasuaji, Maabara na jengo watumishi.

Kufuatia kugawanywa kwa Halmashauri ya Bagamoyo na kupatikana Halmashauri ya Chalinze, Halmashauri ya Bagamoyo imebaki bila ya kituo cha Afya.

Kukamilika kwa kituo cha Afya Kerege kutaifanya Halmashauri ya Bagamoyo kuwa na Kituo kimoja cha Afya kati ya kata 11.
 Kina mama wa UWT kata ya Kerege wakiingia ndani ya jengo la upasuaji walipotembelea ujenzi wa kituo cha Afya Kerege leo Tarehe 01 February 2018.
 Kina mama wa UWT kata ya Kerege wakishangilia mara baada ya kuingia ndani ya jengo la upasuaji walipotembelea ujenzi wa kituo cha Afya Kerege leo Tarehe 01 February 2018.
Muonekano wa majengo ya kituo cha Afya Kerege wilayani Bagamoyo.

RAIS DKT MAGUFULI MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa  Ibrahim Hamisi Juma baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim  Juma na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Omar Makungu, , Naibu spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora –  Mhe George Mkuchika katika picha ya pamoja na viongozi wa dini na Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuhutubia wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) Mhe. Godwin Ngwilimi  baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya mwaka mpya wa mahakama ama Siku uya Sheria kwenye uwanja wa Mahakama kuu Ocean Road jijini Dar es salaam leo.

Picha na IKULU