Saturday, October 28, 2017

MAGAZET YA LEO TAREHE 28 OKTOBA 2017.

TANESCO YATOA TAHADHARI.

WAWILI WAFARIKI KWA MAJI PWANI.

IMG-20171027-WA0061
Hali ya maeneo yakiwa yamejaa maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Mkoani Pwani na kuleta madhara makubwa ya vifo viwili na magari na wananchi kushindwa kupita katika baadhi ya barabara ,mito na madaraja.(picha na Mwamvua Mwinyi)
…………………………………………………………………..
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Miili ya watu wawili imeopolewa baada ya kuzama maji katika mvua kubwa iliyonyesha Oct 26/27 mwaka huu, Mkoani Pwani .

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Pwani ,Blasilus Chatanda ,akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matukio hayo alisema ,Oct 27majira ya saa 2.30 asubuhi huko Mheza kata ya Pangani wilayani Kibaha, Saimon Ramadhani umri kati ya miaka 25-30 alifariki dunia baada ya kusombwa na maji.

Alisema Saimon alikuwa akijaribu kuvuka kwenye mto Mpiji uliokuwa umejaa maji kufuatia mvua hiyo .

Katika tukio jingine ,Chatanda alielezea ,majira ya saa 5 asubuhi ,mwili wa mtu aliyetambulika kwa majina ya Issa Ally (mgambo),umeokotwa huko mto Kiluvya .

Marehemu anadaiwa kuzama maji wakati akijaribu kumuokoa mtoto aliyetaka kusombwa na maji na hakuweza kuonekana hadi maji yalipopungua na kukutwa amekufa umbali wa km nne toka eneo alilozama maji .

Chatanda alisema,miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Tumbi na itakabidhiwa kwa ndugu baada ya kufanyiwa uchunguzi wa daktari .

“Watu tuwe na tahadhari katika wakati huu wa mvua ,tusiamini maeneo yenye maji mengi ” alisema Chatanda .

Jeshi la Polisi Mkoani Pwani ,limetoa rai kwa wananchi kuchukua tahadhari wakati wa kuvuka mito na maeneo yenye maji mengi ,katika kipindi hiki cha mvua ili kuepusha madhara yasiyo ya lazima .

Monday, October 23, 2017

DC BAGAMOYO AMUAGIZA MKURUGENZI WA CHALINZE KUFUATILIA KESI ZA WATU WALIOWAPA MIMBA WANAFUNZI.



Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze kufuatilia wanafunzi wote waliopata mimba na kushindwa kuendelea na masomo ili kuwachukulia hatua za kisheria wazazi, pamoja na wanaume ambao wamewatia mimba.

Akizungumza katika mahafali ya 10 ya wanafunzi waislamu wanaosoma katika katika shule ya Sekondari Chalinze, Mkuu huyo wa wilaya alisema zipo badhi ya kesi zinaendelea mahakamani na kwamba lengo ni kuhakikisha kila aliyehusika kwa namna moja au nyingine kukatisha masomo ya mwanafunzi anachukuliwa hatua stahiki za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.

Aidha, alisema katika wilaya ya Bagamoyo Tarafa ya Chalinze ndio inayoongoza kwa kwanafunzi kukatisha masomo kwasababu ya kupata mimba hivyo amemuagiza Afisa Tarafa wa Tarafa ya Chalinze kupata takwimu ya wanafunzi waliokatisha masomo yao katika Tarafa hiyo.

Akizungumzia maadili katika jamii mkuu huyo wa wilaya ya bagamoyo aliwataka mabinti wa kiislamu kuvaa mavazi ya stara katika maisha yao ya kila siku ili kuepuka vishawishi kwa wanaume hali itakayopelekea kukatisha masomo yao na kupata magonjwa ya zinaa ikiwemo UKIMWI.

Alisema jamii inapaswa kutambua kuwa UKIMWI bado upo na kwamba njia kubwa inayopelekea kupata maambukizi ya VVU ni kufanya zinaa hivyo aliwataka vijana kuepuka starehe ambazo zitakatisha ndoto zao na ndoto za wazazi wao.

Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza la ulamaa BAKWATA wilaya ya Bagamoyo, sheikh Simba Aboubakari aliwataka vijana wanaomaliza elimu ya sekondari waonyeshe tofauti kati yao na wale ambao hawakufika ngazi hiyo ya elimu.

Alisema Elimu bora ni ile inayompelekea mtu kuwa na tabia njema, madili mema yanayotafsiriwa kwa vitendo katika jamii inayomzunguuka.