Saturday, October 21, 2017

JANETH MASABURI ATEULIWA KUWA MBUNGE.


BAGAMOYO YATUMIKA KUSAFIRISHIA WAHAMIAJI HARAMU.



Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani (ACP)Jonathan Shanna akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa watanzania wawili waliokuwa wakisafirisha wahamiaji haramu 21 .(picha na Mwamvua Mwinyi)
............................................


Na Mwamvua Mwinyi-Bagamoyo

JESHI la polisi mkoani Pwani ,linawashikilia wahamiaji haramu 21 ,raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali ikiwa ni kinyume na sheria .

Aidha limewakamata watanzania wawili waliokuwa wakiwasaidia kuingia nchini wahamiaji hao ambapo pia inausaka mtandao unaojihusisha na biashara hiyo.

Akielezea kuhusiana tukio hilo ,kamanda wa polisi Mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shanna alisema ,octoba 20 usiku  , eneo la Ruvu darajani wilaya ya kipolisi Mlandizi askari wakiwa doria waliwakamata Yabata Shaban (30) mkazi wa Bagamoyo na Mohammed Ayub (20) mkazi wa Bunju wakiwasafirisha wahamiaji hao.

Alisema watuhumiwa walikuwa wakiwasafirisha raia hao kwa kutumia usafiri wa gari aina ya Noah yenye namba za usajili T.209 DEW .
“Walikuwa wakitokea Ethiopia kwenda Afrika ya Kusini ,” Waliingia nchini kwa usafiri wa majahazi wilayani Bagamoyo .

Kamanda Shanna alielezea ,Bagamoyo ndio lango kuu lina bandari bubu kama 17 ,ambazo baadhi ya watanzania wanazitumia vibaya kupitisha magendo na kufanya biashara ya kusafirisha wahamiaji haramu .

Alibainisha kwamba ,watataifisha mali zote za watu wanaojihusisha na biashara ya usafirishaji wa wahamiaji haramu.

Kamanda Shanna aliwatahadhalisha ,wale wanaotoa vyombo vyao vya majini na nchi kavu kusafirisha wahamiaji wanaoingia nchini pasipo kufuata  sheria za nchi kwani navyo vitataifishwa .

Alisema Jeshi la polisi mkoani humo, linaendelea na mahojiano na watuhumiwa wote ili kubaini mtandao wao na wale wanaowasaidia kuingia nchini .

Kamanda huyo ,alisema kuwa wahamiaji hao watafikishwa idara ya uhamiaji kwa hatua nyingine za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani .

Ni siku chache zimepita waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba alipotembelea magereza ya Kigongoni -Bagamoyo,mkoani hapo na kukutana na wimbi la wahamiaji haramu gerezani ambao wengi wao wanasubiria kumaliza kifungo chao na kupelekwa makwao kwa gharama za serikali .

Kutokana na hilo alisema hakuna sababu ya serikali kuendelea kutumia mamilioni ya fedha za walipa kodi kuwahudumia wahamiaji haramu wanaoingia kiholela bila kufuata taratibu .

Nchemba alieleza, badala yake wajihudumie ama wahudumiwe na nchi zao ili kuliondolea mzigo Taifa.


Friday, October 20, 2017

HAYA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2017.

Kiwango cha ufaulu wa Darasa la saba 2017 kimeongezeka kwa asilimia 2.40 ukilinganisha na mwaka 2016.
 
Akitangaza matokeo ya darasa la saba Katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Tanzania (NECTA) Dkt. Charles Msonde alisema jumla ya watahiniwa 662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata alama 100 au zaidi kati ya alama 250 wanazopaswa kupata.

Dk Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 341,020 ambao ni sawa na asilimia 70.93 na wavulana ni 321,015 sawa na asilimia 74.80 .
Amesema idadi ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76.
Dk Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia 70.36, hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.40.

Katibu Mtendaji huyo alisema ufaulu katika masomo ya Kiswahili, Kiingereza na Hisabati umepanda kwa asilimia kati ya 4.25 na asilimia 10.05 kulinganishwa na mwaka 2016.

"Kwa masomo ya Sayansi na maarifa ya jamii ufaulu umeshuka kwa asilimia kati ya 3.56 na asilimia 13.97 kulinganisha na mwaka 2016.

"Watahiniwa wamefaulu zaidi katika somo la Kiswahili ambalo ufaulu ni asilimia 86.86 na somo walilofaulu kwa kiwango cha chini zaidi ni Kiingereza, lenye ufaulu wa asilimia 40.30," amesema Dk Msonde.

Katibu Mtendaji, Dk Msonde amezitaja shule 10 bora kitaifa kuwa ni St Peter iliyopo Kagera, St Severine  (Kagera), Alliance (Mwanza), Sir John (Tanga), Palikas  (Shinyanga), Mwanga (Kagera), Hazina (Dar es Salaam), St Anne Marie (Dar es Salaam), Rweikiza (Kagera) na Martin Luther (Dodoma).
Amezitaja shule 10 ambazo hazikufanya vizuri kuwa ni Nyahaa ya Singida, Bosha (Tanga), Ntalasha (Tabora), Kishangazi (Tanga), Mntamba (Singida), Ikolo (Singida), Kamwala (Songwe), Kibutuka (Lindi), Mkulumuzi (Tanga) na Kitwai A (Manyara).

Aliitaja mikoa iliyoongoza kitaifa kuwa ni Dar es Salaam, Geita, Kagera, Iringa, Kilimanjaro, Njombe, Arusha, Mwanza, Katavi na Tabora.
Dk Msonde amesema mikoa iliyofanya vibaya ni Singida, Tanga, Tabora, Songwe, Lindi na Manyara.

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

PSLE-2017 EXAMINATION RESULTS





























NAIBU WAZIRI WA NISHATI, SUBIRA MGALU ATEMBELEA MRADI WA UMEME MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM.



Naibu wizara ya Nishati Subira Mgalu (wa pili kushoto) akiwa katika Ziara ya kukagua Mradi wa Umeme Mbagala jijini Dar es Salaam, unaotarajiwa kuzalisha MW 50.

Aidha, aliongea  na Wananchi Wakazi wa Mbagala ,Kurasini na Kigamboni na kuzungumzia Shida ya kukatika kwa Umeme Inayotokana na kuongezeka kwa mahitaji ya Umeme kuliko uzalishaji.

Na kwamba kwa sasa shida hiyo inapatiwa  Tiba ya moja kwa Moja na itabaki kuwa historia.

Mradi huo unatarajiwa kukamilika mapema  Desemba 2017.
 Naibu wizara ya Nishati Subira Mgalu akikagua Mradi huo.

MAGAZETI YA LEO TAREHE 20 OKTOBA 2017.