Friday, May 19, 2017

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

SOUPO
  • MAJAMBAZI WATATU WAMEUAWA NA KUPATIKANA KWA SILAHA MBILI WILAYANI NYAMAGANA
KWAMBA TAREHE 19.05.2017 MAJIRA YA SAA 02:30HRS USIKU KATIKA VIWANJA VYA ST. MARY’S MTAA WA NDOFE WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU WATATU WANAOZANIWA KUWA NI MAJAMBAZI WANAOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 

1.BENEDICTO THOBIAS @ BENE MIAKA 31, MKAZI WA NYAMATARA BUHONGWA, 2.MABULA SEGEJA @ BULA, NA 3.CHARLES THOMASI GARULA WALIJERUHIWA KWA RISASI NA BAADAE KUFARIKI DUNIA WAKATI WAKIPELEKWA HOSPITALI BAADA YA WAKIRUSHIANA RISASI NA ASKARI POLISI, AMBAPO KATIKA TUKIO HILO ASKARI WALIFANIKIWA KUKAMATA SILAHA MBILI 1.BASTOLA AINA YA DUTY CZ 75P -07 YENYE NAMBA B.512637 IKIWA NA RISASI 15 NA MAGAZINI 2 NA 2.SHORT GUN ILIYOFUTIKA NAMBA IKIWA NA RISASI MBILI NA MAGANDA MAWILI YA RISASI.

AWALI ALIKAMATWA MGANGA WA KIENYEJI AITWAYE AYUBU NYAMWERU MIAKA 45 MKAZI WA KATORO MKOANI GEITA, AKIWA NA LAPTOP TATU MBILI AINA YA HP NA MOJA AINA YA ASUS NA SIMU MOJA AINA SUMSUNG AMBAYO ILIIBIWA KATIKA TUKIO LA KUVUNJA NYUMBA USIKU NA KUNYANG’ANYA MALI AMBAZO NI LAPTOP TATU, SIMU MBILI NA SILAHA AINA YA BASTOLA DUTY CZ 75P-07 NA FEDHA, TUKIO HILO LILILOTOKEA TAREHE 13.05.2017 KATIKA MAENEO YA NYAMONGOLO NA KUFUNGULIWA KESI YENYE KUMBU NAMBA NY/IR/3773/2017.

MTUHIMIWA HUYO AYUBU NYAMWERU ALIHOJIWA NA ASKARI NA KUTAJA WENZAKE ANAOSHIRIKIANA NAO KATIKA KUFANYA MATAKIO YA UVUNJAJI NA UNYANGA’ANYI HAPA MWANZA NA MAENEO MENGIINE LIKIWEPO TUKIO LA UJAMBAZI LILILOLIELEZA HAPO JUU NA MENGINE. 

ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA TAARIFA HIZO NA KUMKAMATA BENEDICTO THOBIAS @ BENE NA KUWEKA MTEGO SEHEMU TAJWA HAPO JUU AMBAPO WALIPANGA NA WENZAKE WAKUTANE ILI KWENDA KUTELEZA UHALIFU WALIOKUWA WAMEUPANGA.

AIDHA USIKU WA TAREHE 18.05.2017 MAJIRA YA SAA 2:30HRS WENZAKE WATANO WALIFIKA ENEO HILO NDIPO ASKARI WALIPOWAAMURU WAJISALIMISHE WALIKAIDI AMRI HIYO NA KUANZA KUFYATUA RISASI UWELEKEO WA ASKARI WALIPO NA ASKARI WAKAJIBU MAPIGO NA KUWEZA KUWAJERUHI MAJAMBAZI WAWILI TAJWA HAPO JUU NA ZILE RISASI WALIZOZIPIGA ZILIWEZA KUMJERUHI MWENZAO ALIYEKUWA AMEPELEKA ASKARI KWENYE ENEO LILE, WOTE WATATU WALIFARIKI DUNIA WAKATI WANAPELEKWA HOSPITALI KWA MATIBABU.

KATIKA ENEO LA TUKIO POLISI WALIFANIKIWA KUIPATA SILAHA BASTOLA HIYO DUTY CZ 75P-07 TAJWA HAPO JUU ILIYOKUWA IMEPORWA/KUNYANG’ANYWA KULE NYAMONGOLO MALI YA SULEIMANI WAZIRI ALIYEKUWA ANAMILIKI KIHALALI NA SHORT GUN ILIYOFUTIKA NAMBA. MIILI YA MAJAMBAZI HAO IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI, MSAKO WA KUWASAKA WENZAO AMBAO WAMETOROKA NA WENGINE WALIOKUWA WANASHIRIKIANA NAO BADO UNAENDELEA. KATIKA UPELELEZI WA AWALI MAJAMBAZI HAWA NA WENZAO WAMEKUWA WAKIFANYA MATUKIO YA UVUNJAJI WA NYUMBA USIKU NA KUFANYA UNYANG’ANYI NA KUBAKA PINDI WANAPOVUNJA NYUMBA ZA WATU USIKU.
  
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA, AKIWAOMBA KUENDELEA KUTOA TAARIFA SAHIHI NA MAPEMA ZA WAHALIFU/UHALIFU KWANI WANAWAFAHAMU NA PIA NI VIJANA WAO AMBAO WANAISHI NAO KATIKA MAKAZI YAO, ILI POLISI WAWEZE KUWAKAMATA KABLA HAWAJALETA MADHARA MAKUBWA KWA WANANCHI, PIA ANAWASHAURI VIJANA WAFANYE KAZI HALALI ZA KUJIPATIA KIPATO WAACHANE NA TABIA YA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA UJAMBAZI KWANI VITAGHARIMU MAISHA YAO.

IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

WATUHUMIWA 12 WA MAUAJI WABAINIKA PWANI.

unnamed
Kamanda wa polisi mkoani Pwani,kamishna msaidizi mwandamizi ,Onesmo Lyanga,wa kushoto,akizungumza jambo.
.................

JESHI la polisi mkoani Pwani ,limewabaini baadhi ya mtandao wa watuhumiwa wa mauaji yanayoendelea wilayani Mkuranga, Kibiti na Rufiji wapatao kumi na mbili akiwemo mwanzilishi wa mauaji Abdurshakur Ngande Makeo .

Aidha jeshi hilo linaendelea na msako kuwatafuta watu hao ambao wanne picha zao zimepatikana .

Akizungumzia hali ya kiusalama ya Mkoa kutokana na vitendo vya mauaji vinavyoendelea katika wilaya hizo ,Kamanda wa polisi mkoani hapo,Onesmo Lyanga ,alisema wanaendelea na mapambano na upelelezi kuwapata wahusika wote .

Alieleza ,jeshi la polisi limewabaini kwa majina na picha kwa baadhi yao .
Kamanda Lyanga ,aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Faraj Ismail Nangalava ,Anaf Rashid Kapera @Kapelo ,Said Ngunde na Omary Abdallah Matimbwa .

Wengine ni Shaban Kinyangulia ,Haji Ulatule ,Ally Ulatule ,Hassan Uponda ,Rashid Salim Mtulula ,Sheikh Hassan Nasri Mzuzuri  na Hassan Njame .
Kamanda Lyanga ,alieleza kwamba ,Saidi Ngunde inadaiwa anaishi Ikwiriri na Omar Abdallah Matimbwa anaishi Dar es salaam ambapo picha zao wanazo pamoja na ya Faraj na Anaf .

Alieleleza wengine nane bado picha zao hazijapatikana hadi sasa .
“Jeshi letu limebaini hayo kwa kushirikiana na wasiri wetu huku tukiendelea na uchunguzi zaidi ” alibainisha .

Kamanda Lyanga alisema ,watuhumiwa hao ,wamegundulika kuwa hupendelea kutembelea maeneo ya kisiwa cha Simbaulanga ,kisiwa cha Saninga kijiji cha Nchinga .

Kamanda huyo ,alifafanua kijiji kingine ni cha Mfesini kata ya Nyamisati na maeneo mbalimbali ya wilaya za Kibiti ,Rufiji na Mkuranga.

Jeshi hilo linatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa siri kufichua watuhumiwa kwani wanahatarisha hali ya usalama kimkoa .

Limetangaza bingo ya kumpatia sh. mil .tano yeyote atakaefanikisha zoezi hilo .

Hivi karibuni jeshi hilo lilitangaza kuwa kuna mtandao wa majina ya wauaji 102 ambao wanawasaka hadi sasa ili kudhibiti vitendo vya mauaji vinavyotia hofu wananchi .

Picha za wauaji wanaosakwa Pwani:
Aunnamed