Monday, May 15, 2017

STIKA ZA BIMA BANDIA ZABAINIKA.

unnamed
ASKARI wa usalama barabarani wilayani Kibaha mkoani Pwani wakisikiliza elimu juu ya matumizi ya mfumo wa kubaini stika bandia kwa magari mbalimbali,mfumo ulianzishwa na mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini TIRA
 A

kamishna wa mamlaka ya usimamizi wa bima nchini,dr.Baghayo Saqware ,wa kwanza kulia akieleza jambo kwa askari wa usalama barabarani eneo la Mailmoja Kibaha
A 2
Jopo la wajumbe kutoka mamlaka ya usimamizi wa bima nchini wakihakiki stika za bima katika moja ya lori eneo la mizani Mailmoja Kibaha.
............................



MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA),imeanza kampeni endelevu ya kuhakiki magari yenye stika za bima bandia ili kuondoa wimbi la stika hizo ambalo hulisababishia serikali kukosa mapato.

Aidha zoezi hilo litawezesha kubaini mtandao wa makampuni yanayotengeneza stika hizo .

Akizindua zoezi hilo mjini Kibaha,kamishna wa mamlaka ya usimamizi wa bima nchini,dr.Baghayo Saqware ,alisema kampeni hiyo itaendeshwa kwa kusimamiwa na jeshi la polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani kwa kushirikiana na TIRA.

Alieleza kwamba ,uhakiki huo utafanyika kwa kutumia mfumo wa teknolojia ya TEHAMA-unaoitwa TIRA –MIS .

Saqware alisema,askari wa usalama barabarani wanapaswa kutumia mtandao na ujumbe wa kawaida kwenda namba 15200 ambapo watapokea maelezo ya halisi ya stika anayoikagua.

Hata hivyo alibainisha kuwa,wameamua kubuni mfumo huo ili kukomesha wizi unaofanywa na baadhi ya makampuni yanayotengeneza stika na wamiliki wa magari.

Kamishna huyo alisema,tatizo hilo linaweza kukua zaidi endapo mamlaka hiyo itaendelea kukaa kimya ikiwa ni watengeneza wakuu wa stika hizo za bima.

“Tatizo ni kubwa hasa mikoa inayopitiwa na barabara kuu ya Dar es salaam ,Pwani na Arusha”
“Kutokana na hilo tumeona vyema tukaanza kujenga ufa kabla ya ukuta ,Hali isije kuwa mbaya zaidi’alisisitiza Saqware.

Saqware alielezea,wamezindua zoezi na kampeni hiyo rasmi kwa kuanzia wilaya ya Kibaha kwa kutoa elimu kwa askari wa usalama barabarani juu ya mfumo huo.

Alisema kila ofisi yao ya kanda itatekeleza zoezi hilo kwa kutoa elimu kwa wananchi,askari wa usalama barabarani na madereva.

Nae kamanda wa usalama barabarani mkoani Pwani,Abdi Issango ,alisema zoezi hilo limeanzishwa katika muda muafaka kwani utitiri wa stika feki ni kero kubwa.

Alisema wimbi la stika bandia linakwamisha mapato ya serikali na kuumiza wananchi wasio na hatia.

Kamanda Issango ,itasaidia kukamata magari yenye stika feki ili kubaini mtandao wa makampuni mbalimbali yanayotoa bima zisizo halali.

“Watu waliokuwa wakiuziwa bima bandia, kwa sasa watauziwa bima halali na watapata haki zao bila usumbufu “ “Kuna kesi nyingi za bima feki ama wamiliki wengine hutumia stika moja ya bima kwenye magari yake zaidi ya kumi,kinyume na taratibu za TIRA”alifafanua Issango.
 
Kamanda Issango ,alisema bima ni kinga ya ajali ,wahanga wanatakiwa kufidiwa hivyo kama gari limepata ajali halijakata bima  linamnyima mwananchi haki yake ya matibabu,majeruhi na kifo.

Alisema kwa mkoa wa Pwani hali hairidhishi ,kwani magari mengi yamekuwa yakifoji ,na kuwa na stika walizozipata kwa njia za mkato.

Kamanda Issango ,alitoa wito kwa wananchi hasa wamiliki wa mabasi,malori na magari binafsi kuacha kupitia njia zisizo halali kununua ama kutengeneza stika bandia .

MAGAZETI YA LEO TAREHE 15 MAY 2017.

AAFullSizeRender

Sunday, May 14, 2017

MAUAJI MENGINE KIBITI.

KATIB

Na Mwamvua Mwinyi, Kibiti 

WAKATI serikali ikijipanga kuanzisha Mkoa wa kipolisi katika wilaya ya Rufiji, Kibiti ,Mafia na Mkuranga ,katibu wa CCM kata ya Bungu ,wilaya ya Kibiti, Halife Mtulia amepigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kibiti, Zena Mgaya, alisema marehemu ameuawa majira ya saa 4 usiku may 13 .

Alisema alipata taarifa la tukio kutoka kwa viongozi wa CCM kata. 
Zena alieleza Mtulia ameuawa akiwa anatoka uwani mwa nyumba yake kwenda kuoga akiwa ameshika ndoo ya maji ndipo wauaji wawili walipojitokeza na kumuua kisha kutokomea kusikojulikana. 

“Wauaji hao walitumia usafiri wa pikipiki kwa kuiacha mbali na eneo la tukio na baada ya kutimiza adhma yao walitembea kuifuata walipoipaki kisha kuondoka “alielezea Zena.

Alisema Marehemu alikuwa Katibu wa CCM Kata ya Bungu, Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa kutoka wilaya ya Kibiti na mjumbe wa Serikali ya kijiji Nyambunda na ameacha mke na watoto. 

Zena alisema kufuatia matukio ya mauaji kijiji cha Nyambunda kata ya Bungu kimeshapoteza Mwenyekiti wa kiiji, Mtendaji wa Kijiji, na wenyeviti watatu wa vitongoji vilivyoko katika kijiji hicho .

Alipoulizwa kuhusiana na uchaguzi wa ndani ya chama unavyoendelea ngazi ya shina na matawi Zena alisema wanachama wanagomea kujitokeza.

“Uchaguzi wa safari hii ni mgumu hakuna anaejitokeza kugombea kabisa, watu wanahofu “alifafanua.

Nae Asha Hemed na Ramadhani Swedy walisema hali bado ni mbaya kiusalama katika wilaya hiyo na Rufiji.

Walisema jeshi la polisi lisambaze askari wake na maeneo ya vijijini ambako wahalifu hao ndio wamejikita huko.

Matukio hayo ni pamoja na Jan 19,ambapo mjumbe wa serikali ya kijiji cha Nyambunda ,Oswald Mrope, aliuawa kwa kupigwa risasi.

March 1,mwenyekiti wa kijiji cha Nyambunda Said Mbwana aliuawa.
Octoba 24,2016 afisa mtendaji wa kijiji cha Nyambunda Ally Milandu alipigwa risasi na kufa na novemba 6,2016 .

Tukio jingine ni lile la mwenyekiti wa kitongoji cha Nyang’unda kijiji cha Nyambunda Mohammed Thabiti alipigwa risasi akielekea kwake.

Jeshi la polisi Pwani limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai , linaendelea kupambana na kuwasaka wahalifu na kuimarisha ulinzi.