Thursday, April 13, 2017

HABARI PICHA BUNGENI LEO 13 APRILI 2017.

S 1A
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
AA
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango akiwasilisha Ripoti ya mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa za Fedha za Serikali kuu , Fedha za Miradi ya  Maendeleo, Fedha za Mashirika ya Umma na majibu ya hoja na mpango wa  kutekeleza mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma kwa mwaka wa Fedha 2015/2016.
 A 1
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleimani Jafo akiwasilisha Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais (TAMISEMI,UTUMISHI NA UTAWALA BORA) kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
A 2
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
A 3
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwasilisha Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Usimamizi wa Mikataba iliyoingiwa kati ya Serikali na Hospitali za Binafsi Nchini katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
A 4
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Isack Kamwelwe akiwasilisha Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi katika Usimamizi wa uchukuaji wa Maji kutoka Vyanzo vya Maji katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
 A 5
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Ufundi Mhe. Stella Manyanya akiwasilisha Ripoti  ya Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Uzalishaji wa Wahitimu katika Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
 A 6
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
 A 7
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
 A 8
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt Medrid Kalemani  akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
A 9
Mbunge wa Bunda Mjini (CHADEMA) Ester Bulaya akiuliza swali  katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
Z
 Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo  akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
 Z 1
 Mbunge wa Mafia (CCM) Mhe. Mbaraka Kitwana Dau akiuliza swali  katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
 Z 2
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angelah Kairuki  katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
 Z 3
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhe. Isack Kamwelwe akijadiliana jambo na Mbunge wa Mtama Mhe. Nape Moses Nnauye katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
 Z 4
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
Z 5
Ujumbe kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wakiongozwa na Mkaguzi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof Mussa Assad wakifuatilia kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
 S
Wabunge wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017. 

CAG ATOA RIPOTI YAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2015/2016.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Prof. Musa Assad akizungumza na waandishi wa Habari(hawapo Pichani) kuhusu Ripoti ya Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha unaoisha 2015/2016 Leo Aprili 13,2017 Mjini Dodoma.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Prof. Musa Assad akizungumza na waandishi wa Habari(hawapo Pichani) kuhusu Ripoti ya Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha unaoisha 2015/2016 Leo Aprili 13,2017 Mjini Dodoma.
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Prof. Musa Assad na Mwenyeketi Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe.Naghenjwa Kaboyoka  wakiangalia moja ya kitabu cha Ripoti kutoka Ofisi yake wakati alipokutana na  na waandishi wa Habari(hawapo Pichani) kuhusu Ripoti ya Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha unaoisha 2015/2016 Leo Aprili 13,2017 Mjini Dodoma.

MKAZI WA BAGAMOYO MBARONI KWA KUSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU.

unnamed
Kamanda wa polisi mkoani Pwani, kamishna msaidizi mwandamizi, (SACP) Onesmo Lyanga, akizungumza na waandishi wa habari, ofisini kwake.

JESHI la polisi mkoani Pwani, linamshikilia Amiri Alalae (26)mkazi wa Toptop, wilaya ya Bagamoyo kwa kosa la kusafirisha wahamiaji haramu 30 raia wa nchini Ethiopia. 

Kamanda wa polisi mkoani humo, Onesmo Lyanga, alisema tukio hilo limetokea april 13 majira ya saa kumi usiku huko maeneo ya Kilomo kata ya Kilomo tarafa ya Yombo. 

Alieleza kuwa askari wa jeshi la polisi waliokuwa kwenye doria maeneo mbalimbali ya wilaya ya Bagamoyo walifanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu hao wakiwa wameingia nchini bila kibali. 

“Wakiwa wamepakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T. 824 DFG  aina ya Town hiace pickup lililokuwa likiendeshwa na Amiri Alalae “alisema kamanda Lyanga. 

Kamanda Lyanga alisema, wahamiaji waliingia nchini kwa njia ya majini wakitumia majahazi na kushukia maeneo ya bandari bubu ya Jitu Kuu kutoka nchi jirani ya Kenya. 

Alisema watawakabidhi kwa idara ya uhamiaji ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria. 
Kamanda huyo alitoa rai kwa wananchi hasa madereva kuacha tabia ya kusafirisha wahamiaji haramu kwa lengo la kujiongezea kipato. 

Alisema kwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kamwe hawatakuwa na muhali na wale wote wanaofanya biashara hiyo ndani ya mkoa wa Pwani.