Tuesday, April 4, 2017

SERNGRTI BOYS KWENDA MOROCO KESHO.

SERENGETI-BOYS-SA
Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys, inatarajiwa kusafiri kesho saa 10.45 jioni kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Emirates kwenda Morocco kupitia Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).

Timu hiyo yenye wachezaji 23 na viongozi wanane watakuwa Uwanja Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere kuanzia saa 7.00 mchana kwani wanatakiwa kuanza kuingia uwanjani saa 7.45 kwani saa tatu baadaye ndipo ndege itakapopaa.

Wanahabari wanaweza kupata mahojiano ya mwisho kadhalika kupata picha za habari wakati huo wa mchana kabla hawajaingia ndani kwenye ukaguzi wa taratibu za (check in logistics).

Kabla ya kusafiri, timu hiyo ilikuwa kambini hapa nyumbani tangu Januari 29, mwaka huu na baada ya kambi ya mwezi mmoja na nusu, ilicheza mechi tatu za kirafiki za kimataifa.

Machi 30, 2017 ilicheza Burundi ‘Intamba Murugamba’ na kushinda mabao 3-0 kabla ya kurudiana tena Aprili 1, mwaka huu na kushinda mabao 2-0. Mechi zote mbili zilifanyika Uwanja wa Kaitaba, ulioko Bukoba mkoani Kagera.

Mechi ya mwisho hapa nyumbani ilifanyika Aprili 3, mwaka huu dhidi Ghana ‘Black Starlets’ na kutoka sare ya 2-2 katika mchezo ulifanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Serengeti Boys ilitumia mchezo kama ishara ya kuwaaga mamilioni ya Watanzania kabla ya kusafiri kwenda kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14, mwaka huu.

Serengeti Boys itakuwa Rabat, Morocco kufanya kambi ya takribani mwezi mmoja kuanzia Aprili 5, mwaka huu. Ikiwa huko angalau itacheza mechi za kirafiki zisizopungua mbili dhidi ya wenyeji morocco na timu nyingine ya jirani ama Tunisia au Misri.

Kambi hiyo ya Morocco itamalizika Mei mosi, mwaka hu ambako timu itasafiri hadi Cameroon. Ikiwa Cameroon, timu itacheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya wenyeji yaani Mei 3 na 6, mwaka huu kabla ya kusafiri Mei 7, mwaka huu kwenda Gabon ambako Serengeti Boys imepangwa kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola.

Vipimo vya mechi dhidi ya Ghana kadhalika hapo baadaye Cameroon, vitakuwa mwafaka kwenye kufanya tathmini ya uwezo wa Serengeti Boys kwani wapinzani hao wamekuwa na rekodi nzuri kwenye soka la vijana na kwa kipindi hiki zimepangwa kundi A pamoja na wenyeweji Gabon na Guinea.

Kila la kheri Serengeti Boys katika mapambano ya kuwania ubingwa wa Afrika kadhalika kucheza fainali za Kombe la Dunia hapo Novemba, mwaka huu zitakazofanyika India. Serengeti Boys inaweza na Mtanzania tunakuomba kuichangia timu hii kwa namna ya 223344 kupitia mitandao yote ya simu.

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA WAZIRI WA MICHEZO WA ZANZIBAR

Z 2
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembeakifurahia jambo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Rashid Ali Juma wkati walipokutana Jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo mafupi juu ya hali ya Michezo nchini.
 Z 1
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua mbalimbali SErikali  inazofanya  katika kuimarisha Michezo nchini.Kulia kwake ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Rashid Ali Juma na Kushoto kwake ni Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dkt.Hassan Abbas.
Z
Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Rashid Ali Juma akizungumza na waandishi  juu ya Maendeleo ya Michezo ya Zanzibar  kwa ujumla leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe.

MAPOKEZI YA JK BUNGENI YAVUNJA REKODI.

S
Rais Mstaafu wa awamu ya  nne, Jakakaya Mrisho Kikwete akishiriki kuimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa kikao cha bunge mjini Dodoma Aprili 4, 2017. Mheshimiwa Kikwete alikwenda bungeni kushuhudia kuapishwa  kwa mkewe mama Salma.
.......................
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamelipuka kwa shangwe kufuatia Spika wa Bunge hilo kumtambulisha Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara alipowasili Bungeni hapo kwaajiliya kushuhudia kuapishwa kwa mkewemama Salma Kikwete.

Baadhi ya wabunge wamesikika wakisema kuwa wamemmisi Rais Mstaafu huku wengine wakisema rudi baba na wengine wakitaka aruhusiwe kuingia eneo la wabunge iliawsalimie kwa kuhutubia.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jobu Ndugai alisema katika kipindi chote alichokaa Bungenihaijawahi kutokea mgenikupokelewa kwashangwe kama JK. 

Picha ya video iliyokuwa ikionyesha namna wabunge wakimshangilia Rais huyo Mstaafu wa awamuya nne  ilionekana wabunge wote kuwa na furaha na mapenzi makubwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete hata wale wa upinzani.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alitawala vipindi viwili kwa muda miaka10 na kumaliza utawala wake  kwa mujibu washeria mwaka 2015.