Thursday, March 16, 2017

MAKAMO WA RAIS WA TZ AWASILI MBABANE SWAZLAND KUHUDHURIAMKUTANO SADC.

koromije
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikagua gwaride la Heshima lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
..............................


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan  amewasili mjini Mbabane – Swaziland leo 16-Mar-2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
  
Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Mfalme Mswati III mjini Mbabane – Swaziland, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Viongozi mbalimbali ambao wameongozwa na Waziri wa Utumishi wa Umma wa Serikali ya Swaziland Owen Nxumalo.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan baada ya kuwasili uwanjani hapo amekagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake na kushuhudia vikundi mbalimbali vya burudani uwanjani hapo.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dakta JOHN POMBE MAGUFULI ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama inayojulikana kama SADC DOUBLE TROIKA kwenye mkutano huo.

Hapo kesho tarehe 17-Marchi-2017, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan atahudhuria mkutano wa Wakuu na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama unaojulikana kama SADC Double Troika  ambao utajadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)na Falme ya Lesotho.

Mkutano huo wa SADC Double Troika utafanyika kwa kuzingatia mapendekezo ya mkutano wa Mawaziri wa Kamati Ndogo ya Siasa na Diplomasia uliofanyika Dar es Salaam tarehe 24 februari 2017 ambapo mawaziri hao walionyesha ipo haja ya kuitisha mkutano huo ili kujadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama kwenye hizo.

Mkutano wa SADC Double Troika utahusisha nchi Sita wanachama wa asasi hiyo ambazo ni Tanzania,Swaziland, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika msafara wake amefuatana na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Dakta Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Amina Salum Ali.

                   Imetolewa na                       
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbabane – SWAZILAND.

 BANE 3
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia vikundi vya Burudani  mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane  Swaziland leo  march,16, 2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
BANE 2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili  Heshima  kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
BANE
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Swaziland alipowasili  kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

ZANZIBAR YAPATA UANACHAMA WA CAF NA FIFA.

CVVVVVVVVVVVVV
mkutano mkuu wa 39 wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) unaoendelea mjini Addis-Ababa, Ethiopia, umepitisha ombi la chama cha soka Zanzibar (ZFA) kuwa mwanachama rasmi wa CAF.
 
Ni jambo la kihistoria kwa Zanzibar kwani safari hii ombi lao limepitishwa bila kupingwa na inakuwa nchi ya 55 mwanachama wa kujitegemea wa CAF.

Awali Zanzibar ilikuwa inaunganishwa na Tanzania bara chini ya TFF na kupelekea kukosa haki za kushiriki kama nchi kwenye mashindano yanayoandaliwa na CAF pamoja na yale ya FIFA.

Pendekezo hilo lilipelekwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ndugu, Jamal Malinzi na lilipokelewa na wajumbe 54 wengine waliokuwepo.

Hii maana yake ni kuwa kwa sasa CAF ndio shirikisho mwanachama wa FIFA kwa upande wa mabara lenye wanachama wengi zaidi kuliko wote.

Vilabu vya Zanzibar vimekuwa vikishiriki mashindano mbalimbali ya CAF lakini kwa ngazi ya kitaifa hawakuwa na ruhusa na walicheza kwa kuungana na Tanzania bara na kushiriki kama Tanzania.

Kwa maana hiyo basi, chama cha soka cha Zanzibar kitapata uwezeshaji wa kifedha moja kwa moja kutoka CAF na FIFA kwa ajili ya timu ya taifa.

AHMED AHMED ASHINDA URAIS WA CAF.

Rais wa chama cha soka cha Madagascar Ahmad Ahmad ameshinda kiti cha Urais wa Shirikisho la Soka Afrika  katika uchaguzi uliofanyika  leo March 16, 2017.

Uchaguzi uliomalizika Addis Ababa umempa ushindi Ahmad Ahmad baada ya kupata kura 30 dhidi ya 20 za Issa Hayatou.

Matokeo hayo yanahitimisha miaka 29 ya utawala wa Hayatou kama kiongozi wa juu wa soka la Afrika.

Mipango na mbinu kabla ya uchaguzi zimepelea kuwashangaza wengi baada ya kushuhudia kambi ya Hayatou ikidondoshwa.

Hayatou mwenye miaka 70 sasa, alikuwa rais wa CAF tangu mwaka 1988 wakati huo Lionel Messi akiwa na miezi tisa tu tangu azaliwe wakati mtawala huyo mzaliwa wa Cameroon alipotangazwa kusimamia soka la bara la Afrika.

Alianza kutawala tangu March 10, 1988 alikuwa anaifukuzia rekodi ya kuendelea kusalia madarakani kwa awamu ya nane mfululizo.

Uchaguzi ulifanyika leo baada ya mkutano mkuu wa 39 huko mjini Addis Ababa.

Ahmad, who appeared very emotional, becomes only the seventh Caf president in the body’s 60-year history.

Ahmad anakuwa rais wa saba wa CAF kwenye historia ya shirikisho hilo lenye miaka 60 hadi sasa tangu kuanzishwa kwakwe.
 ISSA-hayatou_caf
Rais wa zamani wa Shirikisho  la Soka Afrika Issa Hayatou.