Thursday, March 2, 2017

SERIKALI YANUNUA MTAMBO MPYA WA KUTAMBUA KEMIKALI KWENYE MIGODI.

12
Mkemia Mkuu wa Serikali , Profesa Samwel Manyelle akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na ununuzi wa mtambo mpya wa kisasa  aina ya Energy Dispersive X Ray Fluorescence (EDXRF) kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara wa kutambua aina na kiasi cha madini (Metals)  kwenye migodi.
 3
Timu ya Waandishi wa habari wakifuatilia mazungumzo hayo.

MITAMBO YA KUTENGENEZA POMBE KALI (VIROBA) YAKAMATWA DAR.

mon4
Mashine zinazotumiwa na kiwanda cha Afro African Company kuzalisha pombe kali aina ya viroba pamoja na kutengenezea vifungashio vya plastiki vya kufungashia pombe hizo.
 mon3
Baadhi ya  maboksi yaliyokutwa kiwandani hapo ambapo ndani yake tayari kumejazwa pombe za aina mbalimbali aina ya viroba tayari kwa kuingizwa sokoni.
mon2
Mwanasheria wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira NEMC , Heche Suguti akiwaonyesha waandishi wa habari aina mojawapo ya pombe kali (kiroba) inayozalishwa na kampuni  hiyo pasipo kufuata kanuni za TFDA na  wala haikuwekwa stika kuweka stika za TRA.
 mon1
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi akimuhoji mmoja wa Wamiliki wa kiwanda cha Afro African Company kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam ambao ni wazalishaji na watengenezaji wa pombe mbalimbali aina ya viroba. Ofisi ya Makamu wa Raisi inaongoza uendeshaji wa ukaguzi wa viwanda vyote jijini Dar es Salaam vinavyozalisha na kutengeneza pombe kali(viroba)  na kufunga kwa vifungashio vya plastiki.