Saturday, February 18, 2017

MBUNGE BAGAMOYO ASHIRIKI USAFI WA MAZINGIRA NA MAZOEZI YA VIUNGO.


Mbunge wa jimbo  la Bagamoyo,  Dkt.  Shukuru  Jumanne  Kawambwa, kulia  akishiriki na watumishi wa Halmashauri  pamoja na  wananchi  wengine katika  usafi  wa  mazingira mapemahii  leo.

Mbunge wa jimbo  la Bagamoyo,  Dkt.  Shukuru  Jumanne  Kawambwa.
..............................

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne  Kawambwa ameshiriki mazoezi ya viungo  mapema hii  leo  pamoja usafi  wa mazingira katika mji  wa bagamoyo.

Akizungumza  mara baada ya  kumaliza mazoezi  ya  viungo na usafi, Dkt.  Shukuru  alisema ni vyema  kila  mwananchim akjiwekea  utaratibu  wa  kufanya mazoezi ili  kuweka mwaili  katika  nzuri  ki afya.

Alisema sio tu  mazoezi ya  pamoja yanayowakusanya  watumishi wa  serikali na watu binafsi  lakini  pia  kila  mtu  ajiwekee  utaratibu  wa kufanya  mazoezi  mwen yewe kablaya  kukutana kwa  pamoja.

Aliongeza kuwa kitendo cha  kukutana  pamoja  kinaleta umoja na  mshikamano  mion goni mwa  jamii kwakuwa watu  wa aina  mbalimbali wanakutana  na  kushirikiana katikamazoezi  bila ya kujali  mtu  cheo  chake  na  uwezo  wake  wa kifedha.

Akizungumzia swala usafi  alisema kuwa, kufanya usafi  wa mazingira  kutasaidia  kuondoa  mazalia ya  mbu na  na uchafu  ambao  unaweza kuwa chanzo cha magonjwa mbalimbali katika mitaaa.

Aliongeza kuwa swala usafi  ni  jukumu  la kila  mtu  katika  sehemu yake ya  kazi, biashara au nyumbani kwake  ambapo kila mmoja akidumisha usafi  mji  wote utakuwa safi.

Mazoezi   ya  viungo na  usafi  katika mji  wa Bagamoyo  yametekelezwa kwakushirikiana  wananchi na wakuu  wa  idara  mbalimbali  katika Halmashauri ya Bagamoyo  wakiongozwa  na Katibu tawala  wilaya ya Bagamoyo, Arica Yegela.
Mshauri wa Mgambo  wilaya ya Bagamoyo, Meja  Iddi  Musira, akishiriki  usafi  wa mazingira mapema hii  leo.
Watumishi  wa  Halmashauri ya  Bagamoyo, na  wananchi mbalimbali wakishiriki usafi  wa mazingira mapema hii  leo  mjini  Bagamoyo.
 Mbunge wa jimbo  la Bagamoyo,  Dkt.  Shukuru  Jumanne  Kawambwa, kulia akizungumza na baadhi ya  watumishi  walioshiriki mazoezi ya  viungo na usafi  wa mazingira mapema hii  leo.
 Watumishi  wa  Halmashauri ya  Bagamoyo, na  wananchi mbalimbali wakishiriki usafi  wa mazingira mapema hii  leo  mjini  Bagamoyo.
Mazoezi  yalifanyika katika uwanja wa  Mwanamakuka
Afisa utamaduni  Wilaya ya Bagamoyo,  Hamisi  Kimenya, akitoa maelekezo  ya nini cha kufanya baada ya kumalizika kwa mazoezi ya viungo katika uwanja  wa Mwanamakuka  mapema  hii  leo.
Diwani wakataya Kiromo, Hassan R.  Usinga, (Wembe) akiwa ndani ya  mtaro  wa maji  taka mapema hii  leo  katika usagi wa mazingira.


Diwani wakataya Kiromo, Hassan R.  Usinga, (Wembe) akiwa ndani ya  mtaro  wa maji  taka mapema hii  leo  katika usagi wa mazingira.

Sunday, February 12, 2017

AMANA BANK, YAPIGA HODI BAGAMOYO.



Afisa mawasiliano, wa Amana Bank, Jamali  Issa Juma, kulia akizungumza katika mkutano huo, kati kati ni Meneja wa Tawi  la  Tandamti  Kariak oo ,  Juma Yamlinga, kutoka  kushoto ni Meneja wa shuleya  Sirajulmunir  Kiwangwa,  Mwinjuma  Nyawale na  wa pili  kushoto ni  Amiri wa Taasisi ya  Sirajulmunir  Islamic Center,  (SIMIC) Abdallaah  Kindamba.
.......................................
Benki  inayofuata sheria za  kiislamu hapa nchini, Amana Bank, imefanya  mkutano mjini  Bagamoyo wenye  len go  la kutam bulisha huduma  zake  kwa  wakazi  wa mji huo.

Katika mkutano huo watoa mada kutoka Amana Bank waliweza kufafanua  aina mbalimbali za Akauntizinazopatikana ndani ya Amana Bank huku wakielezea mfumo wa kiislamu katika kufanya miamala ya  kifedha  kwa mujibu  wa sheria za  kiislamu.

Awali akizungumza  wakati wa ufunguzi  wa mkutano huo, Amiri  wa Taasisi ya Sirajulmunir  Islamic Center (SIMIC) Sheikh Abdallaah  Kindamba, alisema  Mwenyezimungu  ndani ya   Qur ani  ameharamisha riba na amehalalisha biashara, hivyo ni  wajibu  wa kilamuislamu  kuhakikisha  anaepuka  miamala ya  kifedha  inayoambatana na riba.

Alisema  kutetereka  kwa  uchumi  duniani,  na mtu mmoja  mmoja ni  matokeo ya  watu  kuacha  amri  za mwenyezimungu  na kufanya  yale yaliyokatazwa  ikiwemo  kula riba.

Aliongeza kuwa njia pekee  ya kurekebisha  uchumi  ni  kuepuka kabisa miamala  ya  kifedha  yenye riba ikiwemo mikopo  yenye riba  inayotolewa na taasisi mbalimbali za  kifedha.

Alisema katika macho ya kawaida mtu ataona anafaidka lakini matokeo yake ni kudhalilika hapaduniani huku adhabu ya  mwenyezimungu  ikimsubiri  kwa  kufanya yale aliyokatwa.

Akizungu mza katika  mkutano huo, Meneja wa  Amana Bank tawi Tandamti  Kariakoo,  Juma Tamlinga,  alisema Benkihiyo inafuata misingi ya sheria  za kiislamu na  hivyo  kuondokana  kabisa na  maswala ya  riba hali  iliyopelekea waislamu wengi  kuitumia kwa  kuweka fedha  zao na kupata  mikopoya vitu mbalimbali.

Alisema Amana Bank  ina akaunti  za aina  mbalimbali ikiwemo, Akaunti za  kawaida,  Akaunti  za  wanawake,  Akaunti  za muda maalum, Akaunti za watoto  na  Akaunti  za hija, ambapo alisema  watu  mbalimbali wamefaidika na Akaunti hizo ikiwemo  kuweka fedha kidogokidogo  kwaajili ya kwenda  kutekeleza ibada ya Hijja.

Nae Afisa mawasiliano wa Amana Bank, Jamali Issa alisema  Amana Bank  ni  miongoni  mwa Benki za  Kiislamu  duniani  ambazo zinatoa huduma zakekwa kufuata  sheria  za  kiislamu na  kusema  kuwa Benki  zimekuwa na faida sio tu  kwa mtu  mmoja mmoja bali hata  kwataifa  kwa ujumla.

Aliongeza  kuwa Benki  za  kiislamu  zilianzishwa tokamiaka ya  sitini  amba mpaka sasa nchi  kadhaa duniani zinatu mia  mfumo  huo  wa  kutoa  huduma za    kib en ki  kwasheria  za  kiislamu.

Alisema  katika sheria  ya  kiislamu imeharamishwa riba na  kuhalalishwa biashara,  hivyo  Amana Banki inaendesha shughuli zake  kwa kuzingatia  hilo ambapo  inatoa mikopo  ya vitu  mbali mbali bila ya  riba.

Alisisitiza kuwa katika  sheria ya  kiislamu fedha sio  bidhaa  ispokuwa  fedha hubadilishwa kwa vitu ili  kuweza kupata  maana ya  biashara.

Mkutano huo  ambao  umelenga kutoa elimu  kwa  wakazi  wa Bagamoyo kuhusu huduma  zinazotolewa na  Amana  Bank  umehudhuriwa na watu  mia tano huku  zaidi ya watu  mia mbili  wakiwa wamefungua Akaunti papohapo.








WAZIRI MKUU AKABIDHIWA KAZI YA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA.

16

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri na Makatibu Wakuu baada ya kuwaapisha Mabalozi na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
.................................


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemkabidhi Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kazi ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya akiwa kama Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Dawa hizo nchini.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati akiwaapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji, Anna Peter Makakala, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers William Sianga pamoja na mabalozi watatu Mhe. Omary Yusuph Mzee, Mhe.Joseph Edward Sokoine pamoja na Mhe. Grace Aron Mgovano aliowateua hivi karibuni.

Dkt. Magufuli amesema kuwa Waziri Mkuu anatajwa kwenye Sheria Na.5 ya mwaka 2015 kuwa ni Mwenyekiti wa Tume hiyo ambapo Wajumbe wake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Elimu ana Mafunzo ya Ufundi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

“Nalipongeza sana Bunge la kipindi cha mwaka 2010 – 2015 chini ya Spika mstaafu, Mhe. Anne Makinda lililopitisha Sheria hii baada ya kuona sheria za mwanzo za kupambana na dawa za kulevya hazina nguvu hivyo Wabunge wa wakati ule walisimama kwa pamoja bila kujali itikadi za vyama vyao wakapitisha sheria hii,” alisema Dkt. Magufuli.

Aidha, Dkt. Magufuli amempongeza Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete kwa kusaini sheria hiyo haraka mara baada ya Bunge hilo kuipitisha kwa sababu alijua madhara ya dawa za kulevya katika nchi yetu.

Amefafanua kuwa sheria imeeleza wazi katika kifungu cha 10 cha Sheria Na.5 ya mwaka 2015 kuwa jukumu la kupambana na dawa za kulevya linasimamiwa na Serikali pekee yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Makamo wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya au mtu yoyote atakayekuwa amepewa mamlaka ya kusimamia Serikali.

Kwa upande wake Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa Taifa limeendelea kushuhudia kizazi chetu kikiendelea kudidimia kwa sababu ya matumizi ya dawa za kulevya na Serikali kwa mipango yake imeendelea kukemea, kudhibiti na kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya wazalishaji, wasambazaji, wauzaji na watumiaji wa dawa hizo.

“Jambo hili limeleta athari kubwa sana kwani vijana wetu wengi wamepoteza uwezo wa kujisimamia katika shughuli zao za maendeleo kwa sababu baada ya matumizi tumeona athari kadhaa zikiwezo za kudhoofishwa kwa mwili, uwezo wa kutafakari pamoja na kutoweka kwa uwezo wa kufanya kazi,”alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa ameongeza kuwa Taifa hili la Watanzania kwa kiasi kikubwa linawategemea vijana waweze kuleta msukumo wa maendeleo ndani ya nchi hivyo jambo hili likiachiwa linaweza kuleta athari kubwa katika ukuaji wa uchumi na maendeleo yetu kwa ujumla wake.

Alisisitiza kuwa vita hii ilianza, inaendelea na itaendelea kupiganwa hadi imalizike hivyo Watanzania hawana budi kuunga mkono jitihada zozote zinazofanywa na Serikali kuhakikisha wanatokomeza uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi yake kwa namna yoyote ile, kila mmoja anatakiwa kushiriki kikamilifu ili kubaini matumizi ya dawa za kulevya ndani ya nchi hii.