Mbunge wa jimbo
la Bagamoyo, Dkt. Shukuru
Jumanne Kawambwa, kulia akishiriki na watumishi wa Halmashauri pamoja na
wananchi wengine katika usafi
wa mazingira mapemahii leo.
..............................
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa ameshiriki mazoezi ya viungo mapema hii
leo pamoja usafi wa mazingira katika mji wa bagamoyo.
Akizungumza
mara baada ya kumaliza
mazoezi ya viungo na usafi, Dkt. Shukuru
alisema ni vyema kila mwananchim akjiwekea utaratibu
wa kufanya mazoezi ili kuweka mwaili
katika nzuri ki afya.
Alisema sio tu
mazoezi ya pamoja
yanayowakusanya watumishi wa serikali na watu binafsi lakini
pia kila mtu
ajiwekee utaratibu wa kufanya
mazoezi mwen yewe kablaya kukutana kwa
pamoja.
Aliongeza kuwa kitendo cha kukutana
pamoja kinaleta umoja na mshikamano
mion goni mwa jamii kwakuwa
watu wa aina mbalimbali wanakutana na
kushirikiana katikamazoezi bila
ya kujali mtu cheo
chake na uwezo
wake wa kifedha.
Akizungumzia swala usafi alisema kuwa, kufanya usafi wa mazingira
kutasaidia kuondoa mazalia ya
mbu na na uchafu ambao
unaweza kuwa chanzo cha magonjwa mbalimbali katika mitaaa.
Aliongeza kuwa swala usafi ni
jukumu la kila mtu
katika sehemu yake ya kazi, biashara au nyumbani kwake ambapo kila mmoja akidumisha usafi mji
wote utakuwa safi.
Mazoezi ya
viungo na usafi katika mji
wa Bagamoyo yametekelezwa
kwakushirikiana wananchi na wakuu wa
idara mbalimbali katika Halmashauri ya Bagamoyo wakiongozwa
na Katibu tawala wilaya ya
Bagamoyo, Arica Yegela.
Mshauri wa Mgambo
wilaya ya Bagamoyo, Meja
Iddi Musira, akishiriki usafi
wa mazingira mapema hii leo.
Watumishi
wa Halmashauri ya Bagamoyo, na
wananchi mbalimbali wakishiriki usafi
wa mazingira mapema hii leo mjini
Bagamoyo.
Mbunge wa jimbo
la Bagamoyo, Dkt. Shukuru
Jumanne Kawambwa, kulia akizungumza na baadhi ya watumishi walioshiriki mazoezi ya viungo na usafi wa mazingira mapema hii leo.
Watumishi
wa Halmashauri ya Bagamoyo, na
wananchi mbalimbali wakishiriki usafi
wa mazingira mapema hii leo mjini
Bagamoyo.
Mazoezi
yalifanyika katika uwanja wa
Mwanamakuka
Afisa utamaduni
Wilaya ya Bagamoyo, Hamisi Kimenya, akitoa maelekezo ya nini cha kufanya baada ya kumalizika kwa
mazoezi ya viungo katika uwanja wa
Mwanamakuka mapema hii
leo.
Diwani wakataya Kiromo, Hassan R. Usinga, (Wembe) akiwa ndani ya mtaro
wa maji taka mapema hii leo
katika usagi wa mazingira.
Diwani wakataya Kiromo, Hassan R. Usinga, (Wembe) akiwa ndani ya mtaro
wa maji taka mapema hii leo
katika usagi wa mazingira.
No comments:
Post a Comment