Sunday, February 12, 2017

AMANA BANK, YAPIGA HODI BAGAMOYO.



Afisa mawasiliano, wa Amana Bank, Jamali  Issa Juma, kulia akizungumza katika mkutano huo, kati kati ni Meneja wa Tawi  la  Tandamti  Kariak oo ,  Juma Yamlinga, kutoka  kushoto ni Meneja wa shuleya  Sirajulmunir  Kiwangwa,  Mwinjuma  Nyawale na  wa pili  kushoto ni  Amiri wa Taasisi ya  Sirajulmunir  Islamic Center,  (SIMIC) Abdallaah  Kindamba.
.......................................
Benki  inayofuata sheria za  kiislamu hapa nchini, Amana Bank, imefanya  mkutano mjini  Bagamoyo wenye  len go  la kutam bulisha huduma  zake  kwa  wakazi  wa mji huo.

Katika mkutano huo watoa mada kutoka Amana Bank waliweza kufafanua  aina mbalimbali za Akauntizinazopatikana ndani ya Amana Bank huku wakielezea mfumo wa kiislamu katika kufanya miamala ya  kifedha  kwa mujibu  wa sheria za  kiislamu.

Awali akizungumza  wakati wa ufunguzi  wa mkutano huo, Amiri  wa Taasisi ya Sirajulmunir  Islamic Center (SIMIC) Sheikh Abdallaah  Kindamba, alisema  Mwenyezimungu  ndani ya   Qur ani  ameharamisha riba na amehalalisha biashara, hivyo ni  wajibu  wa kilamuislamu  kuhakikisha  anaepuka  miamala ya  kifedha  inayoambatana na riba.

Alisema  kutetereka  kwa  uchumi  duniani,  na mtu mmoja  mmoja ni  matokeo ya  watu  kuacha  amri  za mwenyezimungu  na kufanya  yale yaliyokatazwa  ikiwemo  kula riba.

Aliongeza kuwa njia pekee  ya kurekebisha  uchumi  ni  kuepuka kabisa miamala  ya  kifedha  yenye riba ikiwemo mikopo  yenye riba  inayotolewa na taasisi mbalimbali za  kifedha.

Alisema katika macho ya kawaida mtu ataona anafaidka lakini matokeo yake ni kudhalilika hapaduniani huku adhabu ya  mwenyezimungu  ikimsubiri  kwa  kufanya yale aliyokatwa.

Akizungu mza katika  mkutano huo, Meneja wa  Amana Bank tawi Tandamti  Kariakoo,  Juma Tamlinga,  alisema Benkihiyo inafuata misingi ya sheria  za kiislamu na  hivyo  kuondokana  kabisa na  maswala ya  riba hali  iliyopelekea waislamu wengi  kuitumia kwa  kuweka fedha  zao na kupata  mikopoya vitu mbalimbali.

Alisema Amana Bank  ina akaunti  za aina  mbalimbali ikiwemo, Akaunti za  kawaida,  Akaunti  za  wanawake,  Akaunti  za muda maalum, Akaunti za watoto  na  Akaunti  za hija, ambapo alisema  watu  mbalimbali wamefaidika na Akaunti hizo ikiwemo  kuweka fedha kidogokidogo  kwaajili ya kwenda  kutekeleza ibada ya Hijja.

Nae Afisa mawasiliano wa Amana Bank, Jamali Issa alisema  Amana Bank  ni  miongoni  mwa Benki za  Kiislamu  duniani  ambazo zinatoa huduma zakekwa kufuata  sheria  za  kiislamu na  kusema  kuwa Benki  zimekuwa na faida sio tu  kwa mtu  mmoja mmoja bali hata  kwataifa  kwa ujumla.

Aliongeza  kuwa Benki  za  kiislamu  zilianzishwa tokamiaka ya  sitini  amba mpaka sasa nchi  kadhaa duniani zinatu mia  mfumo  huo  wa  kutoa  huduma za    kib en ki  kwasheria  za  kiislamu.

Alisema  katika sheria  ya  kiislamu imeharamishwa riba na  kuhalalishwa biashara,  hivyo  Amana Banki inaendesha shughuli zake  kwa kuzingatia  hilo ambapo  inatoa mikopo  ya vitu  mbali mbali bila ya  riba.

Alisisitiza kuwa katika  sheria ya  kiislamu fedha sio  bidhaa  ispokuwa  fedha hubadilishwa kwa vitu ili  kuweza kupata  maana ya  biashara.

Mkutano huo  ambao  umelenga kutoa elimu  kwa  wakazi  wa Bagamoyo kuhusu huduma  zinazotolewa na  Amana  Bank  umehudhuriwa na watu  mia tano huku  zaidi ya watu  mia mbili  wakiwa wamefungua Akaunti papohapo.








No comments:

Post a Comment