Friday, December 2, 2016

WANANCHI WAZUIA MSAFARA WA MBUNGE WA JIMBO. LA MKURANGA ABDALLAH ULEGA

ule2
Mbunge wa  Jimbo la Mkuranga Mkoani Pwani, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibuyuni  Kata Panzuo baada kufunga barabara kwa lengo la kufikisha malalamiko yao.
 ule3
Mkazi wa kijiji cha Kibuyuni  Kata Panzuo,Juma Mwengele akizungumza kwaniaba ya wananchi wezake  wa Kata ya Panzuo juu ya Ng’ombe ambao wanapita kuharibu vyanzo vya Maji na hata mazao.
 ule4
Mbunge wa  Jimbo la Mkuranga ,Abdallah Ulega akikagua timu kabla ya mchezo wa Kombe la Ulega Cup.
...........................
 
WANANCHI wa Kata ya Panzuo wamelazimika kufunga barabara kwa lengo la kufikisha malalamiko yao Kwa  Mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega ambaye Alikuwa anatoka kijiji cha mkuruwili, kusikiliza kero yao hususani Ng’ombe ambao wamekuwa tatizo kubwa katika Wilaya ya Mkuranga.

Wananchi hao ambao walilazimika kukaa katikati ya barabara walimweleza Mbunge Ulega kwamba wanataka kusikia kauli yake juu ya uharibufu unaofanywa na Ng’ombe hao.
 
Akizungumza kwaniaba ya wananchi wezake  Mkazi wa kijiji hicho Juma Mwengele alisema kuwa wamelazimika kufunga barabara ili kuonesha hisia zao kwamba wanakerwa na uharibufu unaofanywa na Ng’ombe ambao wanapita kuharibu vyanzo vya Maji na hata mazao.
 
“Ndugu mbunge kwaza tunaomba samahani sana Kwa kuharibu utaratibu wako lakini tumeladhimika kufanya hivyo kutokana na wanyama wanaitwa ng’ombe,kwakweli wanatuasili mno na tuseme tu hatuwataki sisi.”alisema Mwengele.
 
Aliongeza kuwa ng’ombe wamekuwa tatizo kubwa na kadri siku zinavyokwenda hali inazidi kuwa mbaya mno kwani wanyama hao kila siku wanaingia Kwenye maeneo muhimu hususani kwenye vyanzo vya Maji pamoja na mashambani.

DC BAGAMOYO AMPA SIKU MOJA OCD CHALINZE KUMUHAMISHA MKUU WAKITUO CHA WAMI KWA KUTOSHUGHULIKIA MATATIZO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA.

Mkuu  wa wilaya ya Bagamoyo, Majid  Mwanga  amempa siku moja kamanda wa polisi wilaya ya  Kipolisi Chalinze SSP Janeth Magomi, kumuondoa mkuu wa kituo cha  polisi cha Wami kufuatia tuhuma za  kuwapendelea wafugaji na kuwanyanyasa  wakulima na  kupelekea  kushindwa kuwachukulia hatua wafugaji wanaoingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima.

Agiza hilo  amelitoa kwenye  Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha  Mandela kata ya Mandela ambapo awali wananchi  walipata nafasi ya kutoa  malalamiko yao  mbele ya mkuu wa wilaya na kufanya kero  kubwa iliyotawala katika mkutano huo ni kuhusu wafugaji  kuingiza mifugo  kwenye  mazao ya  wakulima na kwamba polisi waliopo kituo cha  polisi Wami wameshindwa kuwasimamia ili kudhibiti hali hiyo.
Akizungumza mbele ya  mkuu  wa wilaya mzee mmoja  alisema aliwahi kufika kituo cha    PolisiWami kutoa Taarifa ya kuliwa mazao yake,  lakini hatua  waliyochukua  Polisi ni  kumwambia huyo mzee akatafute mgambo ili  amkamate mfugaji aliyeingiza mifugo kwenye shamba  lake jambo  limemsikitisha mzee huyo.

Aidha, wananchi mbalimbali walizungumza  katika mkutano huo, wamelalamikia kitendo cha wafugajikuwa na uwezo wa kuharibu mazao ya wakulima bila ya kuchukuliwahatua yoyote.

Kero hizo za wafugaji kwa wakulima ni pamoja na mifugo kula mazao  ya wakulima na hata wanapotakiwa kutoa fidia ya mazao hayo  wamekuwa hawatimizi  kwa kile kinachodaiwa kulindwa na  Polisi, mkuu wa wilaya   anachukua jukumu  la kuomba namba za simu za wafugaji wanaodaiwa na wakulima na kuwapigia simu ili walipe fidia za wakulima.
Mkuu wa Polisi wilaya ya Kipolisi Chalinze. Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP Janeth Magomi akimsikiliza  mkuu  wa wilaya wakati wa mkutano  uliofanyika  kijiji cha Mandela  kata ya Mandela Halmashauri ya Chalinze,  kulia ni mkuu  wa kituo cha Polisi  Wami ambae mkuu  wa wilaya ameagiza ahamishwe.
Wazee wa Kijiji cha  Mandela  wakipiga makofi mara baada ya  mkuu  wa wilaya kutoamaamuzi ya kuhamishwa kwa mkuu wa kituo cha  polisi Wami.
Wananchi wa kijiji cha Mandela wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga alipofanya mkutano wa hadhara na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi  wa  kata ya Mandela, Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo.