Monday, October 31, 2016

DC. BAGAMOYO AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA ZAHANATI ZA KEREGE NA MAPINGA PAMOJA NA SHULE YA MSNGI MTAMBANI, WALIMU WATORO, MANESI WATORO KUSHUGHULIKIWA.



Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh.  Majidi Mwanga, akiwa na mtoto aliyefika  Kliniki katika Zahanati ya  Mapin ga mapema hii leo, ambapo  mtoto huyo alizawadiwa shilingi elfu  kumi na mkuu wa wilaya.



Kulia ni Daktari wa Zahanati ya  Mapinga, Shabani akielezea baadhi ya changamoto  zilizopo katika zahanati hiyo mapema hii leo mara mkuu  wa wilaya alipotembelea ghaflaili kubaini watumishi  watoro na kuangalia utoaji wa huduma kwa ujumla.





Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Majidi Mwanga akipata  maelezo kutoka kwa Nesi wa zahanati ya Mapinga mapema hii  leo alipotembelea ghafla.




Daktari Shabani wa Zahanati ya Mapinga akimuonyesha  mipaka ya zahanati hiyo mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Majidi Mwanga mara  alipotembelea ghafla katika zahanati hiyo mapema hii  leo


Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo akiwa katika Zahanati ya  Kerege mapema hii leo mara  alipofanya  ziara  ya kushtukiza illi kuona utendaji  kazi  katika zahanati hiyo, kulia ni Daktari Asha wa zahanati hiyo



Daktari Asha wa zahanati ya  kerege akimuonyesha  mkuu wa wilaya  kitu  katika zahanati hiyo maraalipotembelea ghafla mapema hii leo





BONDIA THOMAS MASHALE ADAIWA KUUWAWA DAR ES SALAAM.

thomas-mashali
Bondia mtanzania Thomas Mashali maarufu kama (Simba Asiyefugika), amekutwa amekufa huku akiwa na majeraha  usiku wa kuamkia leo huko maeneo ya Kimara jijini Dar es salaam kutokana na sababu ambazo hazijajulikana mpaka sasa.

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa Oganization ya ngumi za kulipwa nchini PST Antony  Lutta, amesema kuwa taarifa walizozipata ingawa bado  hazijathibitishwa inaonyesha Thomas Mashali ameuwawa.

Lutta ameongeza kwamba marehemu enzi za uhai wake amekuwa na tabia ya kufanya vurugu akiwa amelewa sasa hatujui nini kimempata ambapo  mwili wake umekutwa maeneo ya Kimara jijini Dare s salaam ukiwa na majeraha baada ya hapo  ulichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa katika  hospitali ya taifa muhimbili.

Marehemu Mashali kabla ya kifo chake alikuwa  acheze na bondia Chimwemwe kutoka nchini Malawi ,pigano ambalo lilipangwa kufanyika mkoani  morogoro siku ambayo bondia mwenzake Dullah Mbabe alipangwa kucheza pigano la utangulizi.

Mashali ambaye  jina lake la  kuzaliwa ni Christopher Fabian Mashali,aliyezaliwa Septemba 09 mwaka 1989,ameacha rekodi ya kushinda mapambano 19 kati ya hayo 9 akishinda kwa KO,amepoteza mapambano 5 kati ya hayo amepigwa kwa KO mapambano 4 huku akitoka sare pigano moja tu.

Marehemu ameacha mke na watoto.
CHANZO FULL SAHNGWE BLOG.

Sunday, October 30, 2016

DC. KONGWA AZINDUA KAMPENI YA ONDOA NJAA KONGWA (ONJAKO).


Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO)
 

Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO)
 ...........................................


Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deo Ndejembi ameanzisha kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO) yenye dhamira ya kuwasaidia wananchi kuondokana na hali yanjaa ambayo ni kadhia kubwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo sambamba na Taifa kwa ujumla.

Kuanzishwa kwa Kampeni ya Okoa njaa Wilaya ya Kongwa imejili wakati Mkuu huyo wa Wilaya ya Kongwa Akizungumza na Wakuuwa Idara na vitengo, Madiwani wa Kata zote zilizopo Wilayani humo, Watendaji wa Kata, Maafisa Tarafa, Waratibu Elimu Kata, Wenyeviti wa Vijiji vyote 87 vya Wilaya ya Kongwa na watendaji wao, pamoja na wadau waalikwa na Kilimo.

Akizindua kampeni hiyo Dc Ndejembi alisema kuwa Kampeni hiyo imezinduliwa Mwezi Octoba kwa ajili ya msimu wa mwaka 2016/2017 na inatarajiwa kuwa kampeni Endelevu katika kipindi cha Miaka mitano.
 
Ameeleza kuwa huu ni mkakati maalumu katika Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma ili kukabiliana na hali ya Ukame ambayo ni tatizo sugu katika maeneo mengi nchini.

Kutokana na hayo DC Ndejembi ameagiza kuwa na kilimo cha Mtama zaidi kuliko Mahindi. Kwani Wilaya ya Kongwa ina Kaya 59141, na kila kaya kama ikilima Heka mbili (2) za Mtama, Mavuno itakuwa Tani 71000, za Mtama sawa na 83% ya hitaji la chakula Wilayani Kongwa.

Katika kukabiliana na njaa mahitaji mengine mahususi yametajwa ikiwa ni pamoja na Kuongeza uzalishaji wa mtama toka tani 1/ Hekta mwaka 2016 hadi tani3/hekta ifikapo mwezi June 2021, Kuongeza Uzalishaji wa Muhogo mbichi toka tani 6/hekta Mwaka 2016 hadi tani 10 hekta mwaka 2029, Kuongeza uzalishaji wa zao la Alizeti toka tani 1.2/ hekta mwaka 2016 hadi tani 1.8/hekta mwaka 2021.

Pia Mhe Ndejembi alisema kuwa mahitaji mengine ni pamoja na Kuongeza uzalishaji wa ufuta toka tani 0.5/hekta mwaka 2016 hadi tani 1.2/hekta ifikapo june 2021, pamoja na Kuongeza pato la Mtu/watu toka Tsh 500,000/= Mwaka 2016 hadi Tsh 800,000/= June 2021.

DC Ndejembi ameagiza kufanyika utaratibu wa kuhakikisha kila kaya inalima Heka zisizopungua mbili (2) za Mtama, Mbili za Mahindi, kulingana na eneo husika wakishauriwa na maafisa ugani lakini mtama ni lazima kwa kila kaya hata kama analima mahindi.

Pia amewaagiza vijana wote wasio na kazi Wilayani Kongwa wapewe Hekari mbili kila mmoja ili waache kucheza pool table na kujihusisha na vikundi Ovu vya wizi na matumizi ya Dawa za kulevya.

Saambamba na hayo Mhe Ndejembi aamepiga marufuku kuchezwa mchezo wa Pool Table mpaka ifikapo majira ya saa 10 jioni, hivyo kwa yeyote atakaye kiuka utaratibu huo atakuwa amekiuka amri halali ya serikali.