Friday, September 23, 2016

WASTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA WAAGWA DAR

maz7
Maofisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakipunga mikono ikiwa ni ishara ya kuwaaga Wastaafu hao wakati wakipita katika magari Maalum (hawapo pichani).
 maz1

Wastaafu wa Jeshi la Magereza wakiwasili katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga, Dar es Salaam wakiwa wameongozwa na Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile wakielekea Jukwaa Kuu kupokea Salaam ya Heshima. Hafla ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi la Magereza imefanyika leo Septemba 23, 2016.
 maz2

Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile akiwa katika Jukwaa Kuu akipokea Salaam ya Heshima kutoka kwenye Gwaride Maalum la kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza.
 maz3

Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile akikagua Gwaride Maalum la kuwaaga Wastafu wa Jeshi la Magereza lililoandaliwa na Maofisa wa Jeshi la Magereza.
 maz4

Gwaride Maalum likipita mbele ya Jukwaa kwa Heshima.
 maz5

Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakipiga Saluti wakati Gwaride Maalum likipita mbele ya Jukwaa kwa heshima. Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
 maz6

Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile akiwa pamoja na Wastaafu wengine wa Jeshi la Magereza wakitoa Salaam za mwisho wakiwa kwenye magari wakati Gwaride Maalum likiwa limeunda Umbo la OMEGA.
 maz9

Kamishna Mstaafu  wa Magereza Deonice Chamulesile(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wastaafu wa Jeshi la Magereza pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

SHEIKH ALHADI ASEMA RAIS MAGUFULI HAJAKATAA KUONANA NA VIONGOZI WA DINI

dsm
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum akionyesha gazeti la Tanzania Daima kwa waandishi wa habari.
....................................


Viongozi wa Dini nchini, wamesema Rais JOHN MAGUFULI Hajakataa kuzungumza wala kuwapuuza viongozi hao ambao wamemuomba kukutana naye, kama inavyoenezwa na baadhi ya
vyombo vya habari.

Akizungumza leo jijini, Dar es Salaam na waandishi wa habari Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum, amesema taarifa zilizochapishwa na gazeti la Tanzania Daima la Septemba 21 ISSN 0856 9762 toleo na.4310 sio za kweli.

“taarifa hizo sio za kweli, taarifa hizo zimelenga kumgombanisha Rais na Viongozi wa Dini na watanzania kwa ujumla na hilo halitafanikiwa,” alisema Sheikh Alhad.

Aidha Viongozi hao wamesema uamuzi wao wa kumuomba Rais kuonana naye, haujatokana na kuagizwa na UKAWA, bali umetokana na maono waliyopewa na Mwenyezi Mungu.

Amefafanua kuwa Rais MAGUFULI anawaheshimu Viongozi wa dini na mara zote amekua akiwaomba wamuombee na kusema leo ni siku ya tano tangu wamuandikie barua ya kumuomba kukutana naye na wanaimani Rais atakutana na Viongozi hao.

Ameeleza kuwa Barua hiyo imeandikwa Septemba 19 na kupelekwa siku hiyo hiyo Ikulu, ikiwa imesainiwa na Katibu Mkuu wa Bakwata, Katibu Mkuu wa CCT na Katibu Mkuu wa TEC.

“Naomba watanzania wasisikilize maneno hayo kwasababu hayana nia njema kwa Taifa letu, naamini Mh Rais tutaonana nae na tutaongelea mustakbali wa nchi katika mambo mbalimbali,” alisistisa Sheikh Alhad 
Akizungumzia utendaji wa Serikali ya Rais MAGUFULI, Sheikh ALHAD amesema Rais amerejesha nidhamu Serikalini, ukusanyaji mapato umeimarika na pia pengo kati ya wasionacho na walionacho linaanza kupungua.