Sunday, September 18, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI, APOKEA MSAADA WA DOLA 200,000 KUTOKA KWA RAIS WA UGANDA KUSAIDIA WAHNGA WAHANGA WA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA.

bub1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea msaada wa fedha kiasi cha  dola laki mbili (USD 200,000) kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Doroth Samali Hyuha wapili kutoka (kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda Elibariki Maleko. Msaada huo umetolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa Tetemeko la ardhi mkoani Kagera.bub5

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  mchango wa fedha kiasi cha dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) uliotolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni Ikulu jijini Dar es Salaam.bub7

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Uganda hapa nchini Doroth Samali Hyuha mara baada ya kuwasilisha mchango wa kiasi cha fedha Dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni.bub8

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Naibu Balozi wa Kenya hapa nchini Boniface Muhia mara baada ya kupokea salamu za pole kutoka kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kwa misaada mbalimbali ambayo inatarajiwa kuwasili mkoani Kagera kutoka Kenya muda wowote. PICHA NA IKULU

Saturday, September 17, 2016

RAIS DK. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA TETEMEKO LA ARDHI BUKOBA

bub3msi1msi02

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU YATOA TAHADHARI KUHUSU KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA MKUTANO DODOMA

images
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais  Ikulu Bw. Gerson Msigwa. 
 msi2

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI HAMAD MASAUNI AKAGUA MPAKA WA TANZANIA NA KENYA-NAMANGA

1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe, Hamad Masauni akisalimiana na Askari wa Uhamiaji katika kituo cha Uhamiaji cha Namanga, Mkoani Arusha wakati alipokwenda kukagua usalama wa mpaka huo ambapo aliwataka Askari hao kuendelea kufanya Oparesheni za mara kwa mara ili kuhakikisha hakuna wahamiaji haramu ambao watapita katika mpaka huo.
 2

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe, Hamad Masauni akitoka kukagua mojawapo ya ofisi ya Uhamiaji katika mpaka wa Namanga, Mkoani Arusha wakati alipokwenda kukagua usalama wa mpaka huo ambapo aliwataka Askari wa Uhamiaji katika kituo cha Namanga kuendelea kufanya Oparesheni za mara kwa mara ili kuhakikisha hakuna wahamiaji haramu ambao watapita katika mpaka huo.
 3

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe, Hamad Masauni akikagua mpaka wa Tanzania na Kenya (Namanga), Mkoani Arusha wakati alipokwenda kukagua usalama wa mpaka huo ambapo aliwataka Askari wa Uhamiaji katika kituo cha Namanga kuendelea kufanya Oparesheni za mara kwa mara ili kuhakikisha hakuna wahamiaji haramu ambao watapita katika mpaka huo.Katikati ni Mkuu wa kituo cha uhamiaji Namanga, Abdalah Katimba na Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Arusha, Bw. Mwakipesile.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani).