Tuesday, August 30, 2016

WAISLAMU WA BOKO BEACH WAOMBA MSAADA WA KUJENGEWA MSIKITI


Picha ya Msikiti unaotarajiwa kujengwa Boko Beach, kama inavyoonekana kwenye mchoro.
Katibu wa Swaffatul Mukarama,Abdul Saidi Shomari, akielezea kuhusu nama walivyopata wazo la kujenga msikiti katika eneo hilo  la Boko Beach Manispaa ya  Kinondoni jijini Dar  es Salaam. 
Katibu wa Swaffatul Mukarama,Abdul Saidi Shomari, akiwaomba waislamu popote walipo kuchangia ujenzi wa msikiti katika eneo hilo  la Boko Beach Manispaa ya  Kinondoni jijini Dar  es Salaam. 
Mwenyekiti wa Swaffatul Makarama, Yusufu Mjugu akifafanua jambo mbele ya waislamu waliohudhuria kikao hicho
Mwenyekiti wa Swaffatul Makarama, Yusufu Mjugu akitoa mchanganuo  wa  fedha hizo zitakavytu mika kwenye ujenzi wa  msikiti mbele ya waislamu waliohudhuria kikao hicho
Jengo la Msikiti unaotarajiwa kujengwa  kama  linavyoonekana kwenye mchoro
Jengo la Msikiti unaotarajiwa kujengwa  kama  linavyoonekana kwenye mchoro
......................................................................................................................

Waislamu wa maeneo mbalimbali wameombwa  kuchangia ujenzi wa Msikiti  katika mtaa wa Boko beach jijini Dar  es Salaam kutoka  na eneo hilo  kukosekana msikiti kwaajili ya ibada ya swala.

Katika kikao kilichoitishwa na waislamu wa mtaa huo wa Boko Beach   ili kujadili namna ya kujenga  Msikiti, Katibu madrasa ya Swaffatul Mukarama, ambao ndio wasimamizi wa juenzi  huo, Abdul Saidi  alisema wamefikia uamuzi wa kuanzisha wazo  la kujenga msikiti  kwakuwa eneo hilo halina msikiti na kwamba amewaomba waislamu kutoa ushirikiano ili kufanikisha  ujenzi huo.

Alisema eneo hilo halina Msikiti licha ya kuwepo kwa waislamu wengi hali inayopelekea kukosekana swala  ya jamaa, na kuongeza kuwa ili upate swala ya jamaa unalazimika kutembea umbali mrefu mpaka Boko basihaya mahalipo ulipo msikiti.

"Eneo hili lote la Boko Beach halina Msikiti waislamu wa hapa tunaikosa swala ya jamaa na pia watoto wetu wanakosa kujua umuhimu wa swala licha ya kuwa tunawasomesha Madrasa" Alisema katibu Ust. Abdul. 
 
Aliongeza kuwa awali walikuwa hawana hata madrasa ya kusomesha watoto, lakini mama mmoja Bi Zuena Salum alitoa sehemu ya kiwanja chake na kwaajili ya ujenzi wamadrasa ambayo inaendelea mpaka sasa.

Kufuatia uhitaji wa msikiti, waislamu wa eneo hilo pamoja na mama aliyetoa eneo la madrasa kuwa uandaliwe mchoro na lijengwe jengo litakalojumuisha Msikiti  pamoja na Mdrasa ya vijana.

Alisema kufuatia hali wamelazimika kusajili bodi ya wadhamini ili  kusimamia mambo kwa ufanisi bila ya kukiuka sheria za nchi na kwamba usajili upokatika hatua za mwisho  kukamilika.

Akielezea mchakato wa ujenzi huo wa msikiti, Katibu wa bodi ya wadhamini Wanura Maranda, alisema hatua za awali zimeshakamilika ikiwa ni pamoja na kupata michoro ya jengo na makadirio ya gharama ya ujenzi kutoka kwa wakadiriaji majengo.

Aliongeza kuwa, kutokana na  ufinyu wa Kiwanja jengo hilo  litakuwa na ghorofa mbili ili  kupata sehemu ya kuswalia na madrasa ya watoto, aliongeza kwa kusema kuwa walitamani kujenga zaidi ya ghorofa mbili  lakini  hali kifedha wamehofia gharama itakuwa kubwa hali ya  kuwa hawana hata pesa ya kuanzia ujenzi  huo.

 Ust. Maranda alizitaja gharama za ujenzi wa msikiti huo kuwa ni  shilingi milioni mia tano na arubaini na saba, laki moja themanini na nne, mia sita  kumi  na tano tu, 547,184,615/= ili  kukamilisha ujenzi  huo.

Aidha, alisema kuwa wao wameanzisha wazo hilo lakini hawana fedha, hivyo aliwaomba waislamu  popote walipo kutoa ushirikiano na kufanya biashara na MwenyeziMungu kwa kuchangia ujenzi  huo wa msikiti.

Alibainisha kuwa waislamu wanaweza kuchangia kwa njia tofauti, kuchangia kwa kila muislamu alichojaaliwa, mtu mmoja peke yake ikiwa ataweza kujitolea kujenga jengo lote, kwakutoa vifaa au kwa kuingiza fehda katika akaunti iliyofunguliwa Benki ya Amana kwa jina la ya Swaffatul Mukarama, namba ya Akaunti ni 003140405030001 piya una kuwasiliana moja kwa moja na katibu wa Bodi  kwa namba 0713422774 Mwenyekiti namba 0713326287.

Madrasa ya Swaffatul Mukarama imeanzishwa mwaka 2011 ikiwa na wanafunzi 3. kutokana na wazo la Bi Zuena kutoa sehemu ya kiwanj chake ambapo mpaka mpaka sasa ina wanafunzi 70.

Monday, August 29, 2016

UVCCM YAAHIRISHA MAANDAMANO YAKE.

index 

Umoja wa Vijana wa CCM tuliutangazia umma na  dunia kwamba ifikapo Agosti 31 mwaka huu tutaitisha maandamano ya amani nchi nzima yenye lengo la kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk John Pombe Magufuli kwa utendaji wenye tija, ufanisi na uliorudisha imani na matumaini kwa wananchi.

Msimamo na dhamira ya kufanya maandamano hayo ya amani yenye maudhui na kusudio hilo, bado uko pale pale ingawaje si kwa tarehe tuliopanga na kutangaza awali yaani Agosti 31 mwaka huu.

Jumuiya yetu kama mjuavyo ni ya Vijana wa CCM, (UVCCM) inapata malezi kwa karibu mno na Jumuiya ya Wazazi ya CCM. Wiki ya jana Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Nd. Abdallah Bulembo alikutana na waandishi wa habari akitutaka UVCCM  tuahirishe maandamano ya Agosti 31 mwaka huu hadi wakati mwingine.

Kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, Jumuiya ya Wazazi ndiyo Msimamizi wa Malezi, Maadili na Adabu kwa Vijana wote nchini, sisi UVCCM tunaamini kuwa sikio halishindani na kichwa, mtoto ni mtoto kwa Wazazi wake hakui, hana jeuri wala ubishi.

Mtoto au watoto wanaokaidi amri, ushauri au maelekezo ya Wazazi wao huitwa watukutu, wenye viburi, manunda na wasioambilika. UVCCM  si watukutu, hatukufunzwa tuwe wabishi, wakaidi na wenye viburi.

Tumezingatia kutii  maelekezo, makatazo na maonyo , tumeambiwa tuahirishe maandamano yetu nasi tumekubali na kuheshimu mambo tuliyoaswa.

Sambamba na hilo tumepata majibu ya barua yetu tuliyomwandikia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP Ernes Mangu) inayotutaka tuache kufanya maandamano yetu kwa sababu Polisi wamezuia mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa na  maandamano nchi nzima.

Jambo jingine ambalo limetufanya pia tuahirishe maandamano yetu ya Amani ni taarifa ya kintelejinsia  iliowasilishwa na Kamati yetu ya Usalama na Maadili ya UVCCM mbele ya kikao cha Sekreteriet yetu, nayo ilipendekeza  suala hilo liahirishwe kwa wakati huu hadi muda mwingine.

Pia jambo jingine ambalo limefanya maandamano hayo tuyabatilishe ni kulipisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) ambalo litakuwa katika shughuli za maadhimisho miaka 52 tokea kuanzishwa kwake.
   
Wanajeshi wetu watakuwa katika kazi mbalimbali za kijeshi kwenye kambi zao na mitaani kufanya usafi wa mazingira, hivyo isingependeza na wala si heshima wakati sisi tukiandamana, wao wakifanya kazi muhimu kila mmoja wetu zinazomgusa badala yake ni vyema kuwaunga mkono jambo wanalolifanya la usafi wa mazingira.
  
UVCCM tumekubali, hatutaki kuingia katika uvunjaji wa sheria hasa baaada ya kutakiwa kuahirisha na mamlaka za Kisheria hadi wakati mwingine muafaka na si wakati huu.

Tunaelewa kwamba uamuzi wetu wa awali wa kutaka kuandamana kwa amani hata kama tungenyimwa kibali ungetugharimu, ungetusababishia madhara na pengine hasara, kwa wakati huu na kuona jambo lenyewe ni la kuipa Ari serikali katika kuhimiza Uwajibikaji, Utendaji na Usimamizi bora wa Uendeshaji wa masuala ya kiutawala.

Tulishusha maagizo kwa Makatibu wetu wote wa Mikoa yote 32 na Wilaya 171 ya Kichama tukiwataka waandike barua katika Ofisi za Ma RPC na OCD, washirikiane ili kuratibu maandamano na kuyafanikisha kama tulivyokusudia.

Watendaji wetu wa ngazi husika wamefuata maelekezo, wametii taratibu zetu za kiutendaji na leo tumewajulisha tena wasitishe maandamano hadi tutakapowapa tena maelekezo mengine. Tunawahimiza na kuwataka ni vyema kutii mamlaka za Kikanuni na Kisheria.

UVCCM kwa wakati huu tumeamua kuachana na maandamano badala yake tunajikita katika matayarisho ya kuwapeleka Vijana wetu wakashiriki katika Mafunzo ya Siasa, Utawala, Uongozi, Ufundi na Ujasiriamali yatakayoanza kufanyika katika Chuo chetu kilichopo huko Ihemi Mkoani Iringa ambapo kitakuwa kielelezo na alama nzuri ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa vitendo.

Tumewataka Makatibu wetu wa Mikoa na Wilaya kuendelea na zoezi la Uratibu na Uhakiki kwa Vijana ambao watateuliwa kushiriki Mafunzo hayo  huko Ihemi.

UVCCM tunarejea kusema tena kwamba dhamira ya maandamano yetu ya kusifu Utendaji wa Serikali ya awamu ya tano iko pale pale ila tutapanga tarehe nyingine katika wakati ujao badala ya  kufanyika Agosti 31 mwaka huu kama tulivyotangaza hapo awali.

UVCCM tunawataka Vijana wote kuendelea kuheshimu Tunu ya Amani Umoja na Mshikamo wetu kwa Taifa.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
KAIMU KATIBU MKUU