NA HADIJA OMARY, LINDI.
Sharifa Mkwango ameshinda kuwa Mwenyekiti mpya wa chama cha mpira wa miguu Wanawake (TWFA) Mkoa wa Lindi atakaehudumu nafasi hiyo kwa muda wa miaka mitano baada ya kushinda kwa Kura za ndio
Uchaguzi huo umefanyika Jana huko Manispaaa ya Lindi ambao ulihusisha pia nafasi za wajumbe wawili wa kamati tendaji ambao ni Bi. Subira Mwangata na Beatrice Victor pamoja na nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa (TWFA) Bi.Sifa Mwaya
Akifungua mkutano huo Afisa Michezo wa Manispaa ya Lindi Jamal Lisuma kwa niaba ya Katibu tawala wa Wilaya ya Lindi hudhaifa Rashid aliwataka viongozi watakaochaguliwa kutatua changamoto zilizopo Katika Mkoa wa Lindi upande wa soka la Wanawake ikiwemo kuongeza vilabu vya timu za Wanawake na kuanzisha ligi ya Wanawake Ngazi za Wilaya na Mkoa
Amesema lengo la hayo yote ni kutafuta vipaji vya wachezaji hao wanawake wanaoweza kuunda timu ya Mkoa inavyoweza kushiriki ligi kuu ya Wanawake Tanzania Bara.
Kwa upande wake Bi Sharifa Mkwango Mwenyekiti mpya wa (TWFA) ameahidi kufanya uhamasishaji kwa Jamii kuona Umuhimu wa kuwekeza Katika Michezo kwa watoto wa Kike.
Katibu wa kamati ya Uchaguzi Fidea Mnunduma amewapongeza wajumbe kwa kutimiza wajibu wao na kutenda haki kwenye uchaguzi huo na kwamba Kura zimepigwa vizuri hakuna zilizoharibika kila Mmoja ametumia haki yake kwa kutimiza wajibu wake
"Kamati ya uchaguzi inawashukuru wajumbe wote kwa ushirikiano uliouonysha lakini Leo mmeweza kupata viongozi wapya wa TWFA kamati ipo itadumu kwa miaka minne kama mutakuwa na tatizo lolote kamati imefungua milango njooni mtuone"
No comments:
Post a Comment