WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA, CRDB BAGAMOYO WAKATA KEKI PAMOJA NA WATEJA WAO.
WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA, CRDB BAGAMOYO WAKATA KEKI PAMOJA NA WATEJA WAO. Benki ya CRDB tawi la Bagamoyo imesherehekea wiki ya huduma kwa pamoja na wateja wake waliofika kupata huduma siku ya leo jumatano tarehe 07 Oktoba 2026. Akizungumza wakati wa kuwakaribisha wateja katika hafla hiyo fupi Kiongozi wa timu ya mauzo na huduma, Sigsbert Mapunda, amesema CRDB inaungana na watoa huduma kote nchini kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja. Amesema wanayo furaha kushiriki sherehe hiyo pamoja wateja wao waliowahi kufika asubui na mapema huku wateja wote wataoendelea kuja watapata keki na vinywaji ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha sherehe hiyo. Akizungumza kwa niaba ya wateja walioshuhudia hafla hiyo, mfanyabiashara maarufu mjini Bagamoyo Mama Diha amesema wao kama wateja wa CRDB wamefurahi kwa kuthaminiwa na kupewa nafasi ya kushiriki pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB Bagamoyo. Mama Diha amesema wamekuwa wakifika katika Benki hiyo kupata huduma za kutoa na kuweka lakini tofauti leo ...