TPDC YAWALIPA FIDIA WANANCHI LINDI.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la maendeleo ya petrol Tanzania (TPDC) Dr. James Matarangio katikati akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Bilioni 2.036 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kulia kwake kwa ajili ya ulipaji wa fidia kwa wananchi wa Mto mkavu ili kupisha ujenzi wa Mradi wa Gesi asilia (LNG) na kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na uhusiano TPDC, Marie Msellemu ............................................... Na HADIJA HASSAN, LINDI. SHIRIKA la Maendeleo ya Petrol Tanzania TPDC limekamilisha zoezi la ulipaji wa fidia kwa wananchi 693 wa Mtaa wa Likong’o, Masasi ya leo na Mto mkavu ili kupisha Mradi wa kiwanda cha uchakataji wa Gesi asilia (LNG) katika kata ya Mbanja Manspaa ya Lindi Mkoani humo kwa kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi bilioni 5.2. Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania TPDC , Dr.James Mataragio kwa Mkuu wa Mkoa wa Li...