Rais Magufuli ateua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa TMA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 Baruapepe: press@ikulu.go.tz Tovuti : www. ikulu.go.tz Nukushi: 255-22-2113425 OFISI YA RAIS, IKULU, 1 BARABARA YA BARACK OBAMA , 11400 DAR ES SALAAM . Tanzania. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Ikulu, Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Buruhani Salum Nyenzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa ( TMA ). Dkt. Nyenzi ( Tanzania Bara ) anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili. Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Makame Omar Makame kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TMA. Dkt. Makame ( Zanzibar ) ni Mhadhiri Mwandamizi wa Jiografia katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar ( SUZA ). Taa...