Posts

ASKARI WA USALAMA BARABARANI PWANI, WAPATA MAFUNZO KUTOKA ITDA.

Image
Askari wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani wamepata Mafunzo kutoka kwa wataalam wa Chama cha Madereva Wasafirishaji wa Nchi za nje (ITDA). Awali akifungua mafunzo hayo Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani, Mrakiibu wa Polisi (SP) Mosi B. Ndozero, alisema amefurahi kuona Mkoa wa Pwani umekuwa ni moja ya Mikoa ambayo imepatiwa Elimu hiyo ambayo itawasaidia Askari wa usalama Barabarani kuweza kumtambua Dereva anayeendesha gari husika na uelekeo wa gari hilo katika Nchi jirani. Kwa upande wake afisa kutoka Chama cha Madereva Wasafirishaji wa Nchi za nje (ITDA), Solomon Kassa alisema mfumo huo utaongeza ufanisi katika kazi na uhakika katika kazi kwa ujumla kwa askari wa usalama barabarani ikiwemo kupunguza ajali za Barabarani zianazosababishwa na madereva (IN-TRANSIT VEHICLES) wasio na sifa Barabarani kwani kwa kutumia mfumo huu madereva wenye sifa ndio watakaoruhusiwa kuendesha magari ya IT. Sambamba na hilo ameleeza kuwa Chama cha Madereva Wasafir...

MUWEKEZAJI MTURUKI AMPIGA MFANYAKAZI WAKE KIBAHA.

Image
Na Omary Mngindo, Kibaha. Mkazi wa Kijiji cha Soga Kata ya Soga wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani Kashinde Maonaje, amejeruhiwa eneo la shingo kufuatia kupigwa Kareti na muwekezaji Mturuki akiwa kazini kampuni ya yapiMarkezi.   Mkazi huyo amepigwa na Mturuki huyo ambaye ni bosi wame, akiwa kazini saa 4 usiku, baada ya kumkabili kiongozi huyo akimwelezea moja ya changamoto iliyopo, inayohusiana na utendaji wa kazi anayoifanya kitengo cha umeme. Alisema kuwa akiwa katika eneo lake la kazi, kulijitokeza tatizo la kiufundi kuhusu umeme, ambapo alimfuata bosi huyo akamwelezea hali hiyo, lakini cha kushangaza alijikuta anapigwa kareti eneo la shingo, hali iliyomsababishia madhara makubwa. "Ilikuwa usiku kulijitokeza tatizo linaohusiana na umeme kwenye kebo, nikamkabili bosi wangu, ghafla nikamuona amekunja uso, nikajikuta nimepigwa kareti shingoni, kama mnavyoniona hata kugeuka ni shida," alisema Maonaje. Baada ya kujionea tukio hilo baya na la ...

MGALU ATOA ONYO KWA MKANDARASI WA UMEME VIJIJINI KILIMANJARO

Image
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngarenairobi, Wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro alipokuwa katika ziara ya kazi, Agosti 25, 2019. ................................... Na Veronica Simba – Kilimanjaro. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametoa onyo kali kwa Mkandarasi Urban & Rural Engineering, ambaye anatekeleza mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu mkoani Kilimanjaro, kwa kumwambia asiijaribu serikali kwa kutikisa kibiriti kwani njiti zimejaa na kitawaka. Alitoa onyo hilo kwa nyakati tofauti Agosti 25, 2019 akiwa katika ziara ya kazi kwenye Wilaya za Hai na Siha, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na viongozi wao kuwa kasi ya mkandarasi huyo hairidhishi. Akizungumza katika mkutano na wananchi wa Hai, Naibu Waziri Mgalu alikiri mbele yao kuwa utendaji kazi wa mkandarasi husika unasuasua na zaidi ameonesha vitendo vya utovu wa nidhamu kwa serikali kwa kutoitikia wito alipoitwa kushiriki kwen...

AMUIBA MTOTO WA MIEZI 3 NA KUTOWEKA NAE.

Image
Mtu asiyejulikana amemuiba mtoto wa miezi mitatu aitwae Swaum Saidi na kutoweka nae kusikojulikana. Akitoa Taarifa kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Wankyo Nyigesa, alisema tukio hilo limetokea Tarehe 25 agosti 2019 majira ya saa saba mchana maeneo ya Msongola wilaya ya kipolisi Mlandizi. Alisema mama wa mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Mariam Shomari mwenye umri wa miaka 25 aligundua kuibiwa mtoto wake baada ya kurejea nyumbani kutoka kuomba kibiriti nyumba ya jirani. Kamanda Nyigesa aliendelea kusema kuwa, mama wa mtoto huyo alienda kuomba Kibiriti kwa jirani yake umbali wa mita mia mbili na kwamba baada ya kurejea nyumbani hakumkuta mtoto wake ambae alimuacha chumbaani. Alisema mwizi huyo wa mtoto alitumia mbinu ya kumdanganya mtoto mdogo wa miaka mitatu3, Fatma Saidi aliyebaki na mtoto huyo kwa kumwambia ametumwa kumchukua mtoto ili ampeleke kwa mama yake. Mwizi huyo wa mtoto alifanikiw...