Posts

MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCM (NEC)

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) alipokuwa akizungumza na kumpongeza Dk.Bashiru Ali (kulia) mara baada ya kuteuliwa na kupata ridhaa ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC)kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa  ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(katikati), Katibu Mpya wa CCM Taifa Dk.Bashiru Ali (kulia) mara baada ya kuteuliwa na kupata ridhaa ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa  ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(hayupo pichani),   Katibu Mpya wa CCM Taifa Dk.Bashiru Ali (kulia) alipokuwa akiw...

RAIS DKT. MAGUFULI AANDAA FUTARI IKULU.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijiunga na wageni mbalimbali kuchukua futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018.   Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally akiswalisha viongozi na waalikwa mbalimbali swala ya Magharibi kabla ya futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha kufuturu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheik Aboubakary Zubeiry Ally  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018 Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek akipakua futari akiwa ameongozana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Balozi wa Saudi Arabia nchini Mhe. Mohamed bin Mansour al Malik Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa ...

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC)

Image

NAIBU WAZIRI SUBIRA MGALU AFAFANUA MIRADI YA UMEMEVIJIJINI INAYOENDELEA KUTEKELEZWA.

Image
Serikali imesema itaendelea na usambazaji wa umeme vijijini kupitia miradi inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kasi zaidi ili vijiji vyote vilivyoingizwa kwenye Mradi vifikiwe na umeme. Kauli hiyo imetolewa Bungeni na Naibu Waziri wa Nishati Subira Hamisi Mgalu wakati wa kuchangia Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/19 ambapo amewahakikishia wabunge kuwa Serikali kupitia wizara ya Nishati imejipanga kwa kasi mpya ya utekelezaji wa Miradi hiyo. Naibu waziri huyo wa Nishati alisema wizara imepokea changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa kusambaza umeme vijijini kwenye Miradi inayotekelezwa   kupitia Wakala wa Nishati Vijiini (REA) na kwamba tayari wizara imejipanga kuhakikisha changamoto hizo zinapatiwa ufumbuzi ili kazi isipate vikwazo. Katika kuchangia Bajeti ya wizara ya Nishati wabunge walitaka kujua vijiji ambavyo havijafikiwa na umeme ni mkakati upi wa wizara kuhakikisha vijiji hivyo vinapata umeme kupitia Wakala wa Nishati...

KAIMU DC KIBAHA, MAJID MWANGA, ATAKA VIJANA JKT KULINDA AFYA ZAO.

Image
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kibaha Alhaj Majid Mwanga, ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo akikagua gwaride la vijana wa kujitolea Operesheni Merelani waliopata mafunzo ya awali ya kijeshi sherehe hizo zilifanyika uwanja wa mabatini huko Mlandizi wilayani Kibaha katika Kikosi cha Jeshi 832 KJ-RUVU JKT.   Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kibaha Alhaj Majid Mwanga, ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni Merelani uwanja wa mabatini huko Mlandizi wilayani Kibaha katika Kikosi cha Jeshi 832 KJ-RUVU JKT. ............................................. Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kibaha Alhaj Majid Mwanga amewataka vijana wanaomaliza mafunzo ya JKT kutunza afya zao ili waweze kushiriki katika shughuli za kujenga Taifa kikamilifu. Majidi aliyasema hayo wakati wa kufunga   mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa kujitolea operesheni Mererani yaliyofanyika katika kikosi cha jeshi 832 KJ-RU...

RC NDIKILO ATAKA WANANCHI WALINDE MISITU.

Image
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewataka wananchi mkoani humo kuacha kuvamia maeneo hifadhi za misitu ili kuruhusu uoto wa asili kwa manufaa ya taifa. Mhandisi Ndikilo ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kukagua Hifadhi ya Msitu wa Zigua ambayo kwa muda mrefu ilikuwa imevamiwa. Akizungumza mara baada ya kujionea hali ilivyo kwa sasa katika msitu huo Mkuu huyo wa Mkoa alisema baada ya kuwaondoa wavamizi katika hifadhi za misitu za mkoa wa Pwani hali za misitu hiyo imerejea kama kawaida na kwamba sasa misitu hiyo imeanza kupendeza. Alisema kufautia kurudi kwa hali ya kawaida katika Misitu hiyo Mkuu huyo wa Mkoa alisema wananchi mkoani humo wanapaswa kuwa walinzi wa misitu hiyo na kwamba waache kuvamia na kufanya shughuli za kibanadamu. Aliitaja misitu hiyo iliyopo Mkoa wa Pwani kuwa ni Msitu wa Zigua, Msitu wa kazi mzumbwi, na Msitu wa Ruvu kusini Akizungumzia umuhimu wa Msitu wa Zigua alisema msitu huo ni mapitio ya wanyama kutoka mbuga ya...

WANAWAKE BAGAMOYO WAPEWA ELIMU YA UJASILIAMALI.

Image
Wanawake wa Bagamoyo wamepewa elimu ya ujasiliamali ili waweze kujikwamua kiuchumi. Semina hiyo ambayo imeandaliwa na ... ililenga kuwajengea uwezo katika shughuli zao katika uzalishaji wa bidha mbalimbali. Aidha, kinamama hao wametakiwa kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kukabiliana na ushindani wa soko. Muwezeshai wa semina hiyo alisema ni lazima kina mama waiamini kile wanachofanya kwani kuiamini ni njia moja wapo ya kufikia malengo. Kwa upande wao wanawake hao wajasiliamali wilayani Bagamoyo wamesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kuzalisha bidhaa zao na kudhindwa kufikia malengo wanayojiwekea. Walisema miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na kukosa elimu ya ujasiliamali hali inayopelekea kinamama wengi kufanya kazi zao chini ya kiwango. Waliongeza kwa kusema kuwa upatikanaji wa malighafi ni tatizo linalowakwamisha wengi kwakuwa malighafi zimekuwa zikiuzwa kwa bei ya juu au kukosekana kabisa na hatimae mjasiliamali anakata tamaa ya kuende...