TAKUKURU BAGAMOYO YATOA SOMO SHULE ZA SEKONDARI.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani, Suzana Raimond kulia akizungumza katika Tamasha la klabu za wapinga rushwa shuleni, kushoto ni Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Bagamoyo, Raimond Katima. Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga akifungua Tamasha la klabu za wapinga rushwa shuleni. ................................. Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Bagamoyo imeandaa Tamasha la klabu za kupinga rushwa katika shule za sekondari. Katika Tamasha hilo lililofanyika Shule ya Sekondari ya Baobab iliyopo Mapinga wilayani Bagamoyo, Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga ambapo aliwataka wanafunzi kujifunza kuchukia rushwa ili kuwa raia wenye uzalendo na nchi yao. Alisema vijana ni kundi muhimu linalopaswa kutambua ubaya wa rushwa kwakuwa hao ndio wanaondaliwa kuwa viongozi wa baadae hivyo kutambua ubaya wa rushwa kwao kutapelekea nchi kupata viongozi wenye uzalendo watakaoiletea nchi yao maendeleo. Aidha...