Monday, September 30, 2019

MGALU ASEMA, WANAWAKE NI JESHI KUBWA.

 
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu, (kulia) wakijadili jambo wakati wa maadhimisho ya Umoja wa Wanawake yaliyofanyika kiwilaya katika Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo.
 
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu, akizungumza katika maadhimisho hayo.
................................ 

Na Shushu Joel, Chalinze.

NAIBU Waziri wa Nishati Subra Mgalu ambaye pia ni mbunge wa viti maalum (UWT) kupitia mkoa wa Pwani, amewataka wanawake kujiamini zaidi kwa kuwa wao ni jeshi kubwa na lenye uwezo wa hali ya juu.

Akizungumza katika maadhimisho ya Umoja wa Wanawake kiwilaya yalivyofanyika katika Jimbo la Chalinze, wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, alisema kuwa wanawake wamekuwa ni tegemeo kwenye ufanikishaji wa mambo mbalimbali ya kijamii .

"Wanawake ni jeshi kubwa na lenye kutegemewa kwenye chama na serikali hivyo kinamama tuongeze uaminifu kwenye jamii zetu ili tuzidi kuendelea kuwa nguzo zaidi" Alisema Mgalu.

Aidha amewapongeza kinana wote waliojitokeza katika sherehe hizo na kuwataka kutembea kifua mbele kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za vijiji na mitaa kwani umoja wao ndio ushindi wao.

Mgalu amewataka kinamama kukumbuka wajibu wao wa kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika kuwachagua viongozi wa CCM ili kukIfanya chama hicho kuendelea kushika dola.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja huo wilaya ya Bagamoyo Rukia Masenga, amempongeza Naibu Waziri huyo kwa jinsi anavyofanya kazi za umoja wa Wanawake na hasa kuwaweka kitu kimoja wanawake wa mkoa wa Pwani.

Aidha aliongeza kuwa kinamama ni jeshi linalojitambua na hivyo amemuhakikishia naibu Waziri huyo kuwa ushindi ni lazima upatikane.

KIKWETE NI JEMBE LINALOLIMA KIANGAZI NA MASIKA: UWT.


Na Shushu Joel, chalinze.

Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, wamempongeza mbunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete kwa Utendaji wake wa kazi katika jimbo hilo.

Kwa kawaida wakulima walio wengi hapa nchini hutumia muda mwingi katika shughuli ya kilimo kwenye kipindi cha masika lakini Mbunge wa Chalinze amekuwa akilima masika na kiangazi.

Maneno hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Bagamoyo, Bi. Rukia Masenga, alipokuwa akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya Umoja huo ambayo kiwilaya yalifanyika katika Kijiji Cha Msoga, halmashauri ya chalinze.

"Mbunge wa Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete amekuwa ni kiongozi wa kuigwa katika taifa hili kutokanana na jinsi alivyosimamia maendeleo makubwa katika jimbo lake na sisi Umuiya ya Wanawake ndani ya wilaya hii tumeridhishwa na utekelezaji wa ilani katika Jimbo lake "Alisema Bi Rkia.

Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete amewashukuru kina mama hao kwa kuona kile kilichokuwa kinahitajika kwa wananchi kinatekelezeka kwa kiwango kikubwa.

Aliongeza kuwa chalinze imetekeleza ilani ya CCM kwa vitendo kutokana na kupunguza na kumaliza yale yaliyokuwa ni changamoto kubwa kwa Wananchi wa Halmashauri hiyo ikiwemo shida kubwa ya Maji na Afya ya kina Mama na Watoto.

Akizungumzia ujenzi wa Vituo cha afya katika Halmashauri ya Chalinze, Mh. MBunge alisema kazi kubwa imefanyika kujenga Zahanati kila kijiji na leo ni vijiji Vichache ambavyo Zahanati zao hazijakamilika.

Kwa Upande wa Vituo vya Afya hali ni nzuri sana kila Kata ispokuwa kata 3 tu, ambazo nazo ziko mbioni kwenye Ujenzi.

Kwa Upande wa Elimu wamejenga Vyumba zaidi ya madarasa 48, Umeme umesambazaa katika jimbo zima la Chalinze na Miundombinu ya Barabara inakwenda vizuri na Serikali imepanga kutumia Milioni 158.5 kwa ajili ya Barabara za Mji wa Chalinze ambazo zitajengwa kwa kiwango cha lami na madaraja madogo.

Wakati huo huo, Mh. Mbunge Kikwete ameipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kuipatia Chalinze Shilingi Bilioni 16 kwa ajili ya kutatua changamoto ya Maji iliyokuwa kero kubwa sana miaka ya nyuma.


Fedha ambazo amezieleza kuwa zinakwenda kumaliza shida ya maji sio tu kwa wana Chalinze lakini pia kwa Maeneo ya miji ya Jirani hasa Ngerengere, na Magindu kwa upande wa Kibaha Vijijini.

Mh. Mbunge pia amewapongeza wanawake kwa jinsi wananvyokuwa mstari wa mbele katika ufanisi wao wa kuchangamkia fursa ndogo ndogo za halmashauri.

Hadi sasa vikundi zaidi ya 80 vya wanawake vimeweza kufikiwa katima kata mbalimbali lakini kubwa pia ni jinsi wanavyorudisha mikopo hivyo.

Kwa hakika nyie ni wa kipekee, mh. Mbunge alimaliza.

OMARI MGUMBA AKEMEA KILIMO KUFANYWA ADHABU SHULENI.

NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba akizungumza na watumishi wa Halamashauri ya wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji na Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani, Zainabu Abdallah
.....................................



NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba amewataka walimu wa shule za Msingi na Sekondari waache kutumia kilimo kama adhabu ya kuwapa wanafunzi wakati wanapokosea kwani inawajengea tafsiri mbaya kwa jamii na baadae wanapokuwa, wanachukia kilimo.

Mgumba alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa ziara yake wilayani Pangani ambapo alisema kwamba kuna tabia ambayo imejengeka kwa walimu hao kwamba mtoto anapokosea anaambiwa leo utakwenda kulima siku nzima, utakwenda kumwagilia hali ambayo inapelekea baadae wakikua wanakuwa hawahitaji kilimo kwa sababu awali waliona kama adhabu.


Alisema hapana, suala hilo sio jema na ndio maana wao wanasema kilimo ni uti wa mgongo lakini watafungamanisha kilimo na elimu ili watoto tokea anakuwa ajue kwamba nchi hii uchumi wake unategemea kilimo.


“Hivyo ninapoambiwa niwe na tuta la mchicha sio adhabu bali ni sehemu ya kuniandaa kielimu nije kujitegemea au nije kuajiri wengine kwenye mashamba yao kwani bila kufanya hivyo tutakuwa tunaimba kitu kingine wakati uchumi wetu unategemea kilimo”Alisema Naibu Waziri huyo.


Naibu Waziri huyo alisema kwamba mkakati wa serikali ni kuimarisha kilimo hivyo wataendelea kufungamanisha elimu na kilimo chao.


Akizungumzia Kilimo cha Minazi wilayani humo Naibu Waziri huyo alisema kwamba kilimo cha minazi ni kweli hawajapata ufumbuzi wa magonjwa yake kwa miaka zaidi ya 30 sasa, ambayo yanasababsihwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.


Alisema pia hilo linatokana na kukubali kuletewe mbegu ya kisasa ambayo haiendani na mazingira ya nchi hivyo kama Taifa  wameendelea kuimarisha vituo vyao vya utafiti hasa cha utafiti wa minazi mikocheni lengo ni kuanza kurudi kwenye kuzalisha miche kutumia minazi ya asili inayokabiliana na hali ya hewa na ikolojia ya ya nchi yetu .


“Na sasa tumeanza kuzalisha kitalu cha miche asili Bagamoyo na itasambazwa nchi nzima kwa lengo la kupanda na hatimaye kuweza kurejesha minazi hiyo ”Alisema.



Akizungumzia udogo wa bei ya nazi nchini Naibu Waziri huyo alisema kwamba nazi zinauzwa bei ndogo na imeendelea kuwa ndogo ni kutokana na ushindani uliopo kwenye soko la ndani, kanda na kimataifa kwa sababu ya bidhaa mbadala.


“Hivyo kila nazi ikipanda bei, watu wanakwenda kutumia mafuta lakini kila tunapoacha kutumia nazi na kutumia mafuta na kwenda kwenye chukuchuku wanapunguza mahitaji ya nazi ”Alisema.


Hata hivyo alisema kwamba wanakuja na mkakati wa kuanzisha viwanda ambavyo vitaongeza thamani bidhaa hiyo ili kupanua soko la nazi hapa nchini na mbegu za nazi ambazo zinaweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi huku akieleza kwamba wakienda kuongeza thamai tatizo hilo litakwisha.


Katika hatua nyengine Naibu Waziri huyo aliwataka watanzania kuendelea kutumia nazi kwani wanapoendelea kuitumia zaidi wanaongeza mahitaji na soko la nazi litakuwa kubwa huku akisistiza kwamba watakaendelea kutumia mafuta bei ya nazi itashuka.


Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso alisema kwamba zao la nazi limeathiriwa na maradhi kwa muda mrefu na bado tiba yake haijapatikana miaka 30 sasa.

Alimwambia Naibu Waziri Mgumba kwamba ugonjwa huo umekuwa haupati ufumbuzi kama lilivyokuwa gonjwa la ukimwi hivyo walimuomba watafiti na watalamu wafanye utafiti ambao utafika mwisho na wenye manufaa na kuweza kurudisha uchumi wake.

Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji kulia akimueleza jambo Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumba wakati wa ziara yake wialayani humo.

MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani, Mwalimu Hassani Nyange.