Wednesday, March 21, 2018

MPINZANI WA YANGA CAF KUJULIKANA SAA 8:30 MCHANA LEO.


Yanga SC imeangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako watamenyana na moja ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo.

Hiyo ni baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Township Rollers Jumamosi jioni Uwanja wa Taifa mjini Gaborone nchini Botswana.

Timu ambazo zimefuzua hatua ya mtoani ambazo Yanga anaweza kukutana nazo ni Fosa Juniors kutoka Madagascar,CARA Brazzaville (Con),Costa do Sol ya Msumbiji,Akwa United na Enyimba za Nigeria,Deportivo Niefanga ya Equatorial Guinea,Welayta Dicha ya Ethiopia,,El Masry ya Misri,Hilal El  Obied ya Sudan,Raja Casablanca na Berkane za Morocco,Djoliba ya Mali,CR Belouizdad ,USM Alger za Algeria,La Mancha ya Congo Brazaville na Supersport United ya Afrika Kusini.

Timu ambazo zimetolewa Ligi ya Mabingwa na kuangukia Shirikisho ni Yanga ya Tanzania,Aduana Stars ya Ghana,Al-Hilal Omdurman  ya Sudan,Rayon Sport ya Rwanda,ASEC Mimosas na WAC  za Ivory Coast,Gor Maria ya Kenya,As Vita Club ya DRC,Plateau  United na MFM FC za Nigeria,Generation Foot ya Senegal,Bidvest Wits ya Afrika Kusini,CF Mounana ya Gabon,St,George ya Ethiopia ,Zanaco United ya Zambia na US Songo ya Msumbiji.

Droo ya ratiba ya mechi za mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho inatarajiwa kupangwa Leo majira ya saa 8:30 Mchana kwenye makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Mjini Cairo huku inatarajiwa kuwa Live kupitia ZBC2 kwa mjibu wa taarifa ya Shirikisho hilo

AJALI YA GARI YA MKURUGENZI WA TBC, WAWILI WAFARIKI.


Watu wawili wamekufa wilayani Kasulu mkoani Kigoma katika ajali ya gari la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Dkt. Ayub Rioba lililokuwa likitokea wilayani Kibondo kwenda Kigoma Mjini.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliosababisha gari kuacha njia na kuwagonga waenda kwa miguu watatu.

Gari la Mkurugenzi Mkuu wa TBC lililopata ajali lenye namba za usajili  STK 8769 lilikuwa na abiria wawili akiwemo mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu wa kanda ya magharibi TBC Mhandisi Zebron Mafuru ambao  wote wametoka salama na hali zao ni nzuri.

Dkt. Rioba yuko katika ziara ya kukagua vituo vipya vya matangazo vilivyojengwa katika maeneo ya mipakani.

RAIS DKT. MAGUFULI AIVUNJA BODI YA NHC.


SERIKALI YATENGA BILIONI TANO KUNUNUA MASHINE YA KUPIMA VIPIMO VYA TB.


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya wadau wa Sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019.
...................................

NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kununua mashine za kupima vipimo vya ugonjwa wa kifua kikuu katika zahanati na vituo vya afya nchini. 

Hayo yamezungumzwa jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa dawa za kutibu ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa watoto kuanzia umri wa miaka 14 kushuka chini.

“Serikali imadhamiria kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu hivyo tumetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kuongeza mashine nyingine za kufanya uchunguzi kwa haraka ugonjwa wa Kifua Kikuu zinazoitwa Genexpert ” alisema Waziri Ummy. 

Aidha Waziri Ummy alisema kuwa marufuku kwa watoa huduma kutoa matibabu ya Kifua Kikuu kwa gharama yoyote kwani huduma hiyo ni bure. 

Kwa mujibu wa Waziri Ummy alisema kuwa marufuku kwa waganga wa kienyeji kuwashikilia wagonjwa wa Kifua kikuu na badala yake wawaruhusu waende hospitali kwa ajili ya msaada wa haraka. 

Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa takribani  watu laki moja na 60 wana maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa makadirio ya mwaka 2016. 
Sambamba na uzinduzi wa dawa hizo Waziri Ummy amegawa mashine nyingne za Genexpert kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa makohozi ili kugundua kuna maambukizi au hapana kwa hospitali za  ,Kairuki, Agakhan,  Regency , TMJ na Indumandal ambazo kila mashine moja inagharimu shilingi milioni 34 .

Aidha Waziri Ummy ametoa rai kwa wazazi na walezi wa watoto kwenda hospitali mara wanapoona dalili moja wapo ya TB ikiwemo kuumwa mara kwa mara kwa muda wa wiki mbili, kukosa furaha, mtoto kulia mara kwa mara, kupungua uzito , kuchelewa kukua na kikohozi cha mara kwa mara. 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimuangalia mtoto Salome katikati akinywa dawa ya Kifua Kikuu wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua Kikuu kwa watoto wadogo leo jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni Mratibu wa Kupambana na Magonjwa ya Kifua Kikuu na Ukoma Dkt. Beatrice  Mutayoba, anayefuata aliyevaa kitenge ni mzazi wa Salome Bi. Upendo Jeremiah.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akionyesha dawa kutibu Kifua Kikuu kwa watoto wadogo wakati wa uzinduzi wa dawa hiyo leo jijini Dar es salaam kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2018.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi baadhi ya wadau wa Sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2018.
Baadhi ya wadau wa Sekta ya afya wakifuatilia kwa makini Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2018.

MAGAZETI YA LEO TAREHE 21 MACHI 2018.

Tuesday, March 20, 2018

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA HOSPITALI YA ABDALLA MZEE PEMBA.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Rayna Abdala mwenye umri wa mwaka mmoja aliyelazwa kutokana na kuungua moto katika hospitali ya Abdala Mzee, mkoa wa Kusini Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Hafidh Jabir Ali mwenye umri wa miaka 3 aliyelazwa kutokana na kuungua na chai katika hospitali ya Abdala Mzee, mkoa wa Kusini Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Dkt. Wuxiao Shu juu ya matibabu ya mguu wa mtoto AzarAli mwenye umri wa miaka aliyelazwa  katika hospitali ya Abdala Mzee, mkoa wa Kusini Pemba.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi nje ya majengo ya hospitali ya Abdala Mzee, mkoa wa Kusini Pemba mara baada ya kukagua maendeleo ya hospitali hiyo. 

Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

MSITU WA ZIGUA SASA UMEREJEA KATIKA HALI YAKE YA KAWAIDA.


Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Alhaj, Majid Hemedi Mwanga akionyesha sehemu ya makazi ya watu waliokuwa wamevamia msitu wa Zigua hivi karibuni katika Doria maalu ya kukagua msitu huo iliyowashirikisha watendaji kutoka TFS wilaya ya Bagamoyo na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ambapo kwa pamoja wamejiridhisha kwamba hakuna mvamizi aliykuwemo ndani ya msitu huo kwa sasa.
........................................

Hifadhi ya msitu wa zigua imerejea katika hali yake ya kawaida baada ya kuwaondoa wavamizi ndani ya msitu huo.

Akizungumza na bagamoyokwanza blog amara bada ya kufanya doria maalum katika msitu huo, Kaimu Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) Halmashauri ya Chalinze David George Ntemi, alisema hali ya msitu huo kwa sasa inaridhisha kutokana na miti kushamiri na baadhi ya wanyama kuonekana kurejea ndani ya msitu huo ambao awali walianza kutoweka.

Alisema  hifadhi hiyo ya msitu wa Zigua, ulikuwa umeharibiwa na wananchi ambao walivamia kwa kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kulima, kukata miti na kuchungia mifugo hali iliyopelekea msitu kuharibika asili yake na wanyama kukimbia.

Aliongeza kwa kusema kuwa, mara baada ya kuwatoa wavamizi katika zoezi lililoshirikisha wilaya tatu za Bagamoyo, Handeni na Kilindi kwa sasa Hifadhi ya msitu wa Zigua kwa upande wa Bagamoyo uko vizuri baada ya kujihakikishia kuwa hakuna mtu hata mmoja ndani ya msitu huo kwa sasa.

Alisema Doria hiyo maalum imefanywa katika kipindi hiki ambacho tayari wakulima huandaa mashamba kwaajili kilimo cha mwaka hivyo lengo lilikuwa ni kujiridhisha endapo wakulima hao wamerudi au wameondoka moja kwa moja.

Aidha, alisema baada ya kuzunguuka eneo lote wapo watu wawili ambao waliozidisha mipaka yao na kuingilia sehemu ya msitu na kwamba tayari wameshapewa taarifa ya kuacha kupanda sehemu ya msitu ili kuepuka kuharibiwa mazao yao.

Akizungumzia umuhimu wa msitu huo Ntemi alisema msitu huo ni mapitio ya wanyama kutoka hifadhi ya taifa ya Saadani na kuelekea Mikumi.

Ntemi aliongeza kuwa, msitu huo pia ni chanzo cha maji cha mito ya saja na kigulu inayopeleka maji katika mto wami ambao unahudumia miji ya Chalinze na Bgamoyo.

Alisema msitu huo pia ni sehemu ya kuzalia wanyama ambapo kuharibika kwa msitu huo kutapelekea wanya hao kutoweka na hivyo kupoteza rasilimali za taifa.

Ntemi alisema kutunzwa kwa msitu huo kunapelekea kupatikana kwa mvua kwa wakati ambapo ukiharibiwa ni sababbu ya kutoweka kwa mvua hali itakayosababisha ukame katika ukanda huo.

Nae aliyekuwa akiongoza vikosi katika kuwatoa wavamizi Mkuu wa polisi wilaya ya Kipolisi Chalinze Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Janeth Magomi aliwataka wananchi wanaozunguuka msitu huo kutii sheria bila ya shuruti ili kuepuka usumbufu ambao wanaweza kuupata pindi wanapokaidi sheria.

Alisema viongozi wa Mkoa na wilaya kupitia mikutano mbalimbali na wananchi walishatoa maelekezo namna ya kuulinda msitu huo hivyo kila mwananchi akazingatia maelekezo ya viongozi na kuacha kuvunja sheria kwa makusudi.

Alisema kwa sasa hali ya msitu huo tulivu kwakuwa tayari wananchi wanaonekana kutii sheria bila ya shuruti.

Wananchi wa kata ya Kibindu waliozungumza na bagamoyokwanza blog walisema faida walizopata katika kuhamishwa kutoka kwenye msitu ni pamoa na kupata huduma za Afya, Barabara na Elimu.

Walisema katika maeneo ya msitu ilikuwa vigumu watoto kwenda shule na matibabu pale mtu anapoumwa lakini kwa sasa wanapata huduma zote kwa urahisi kwakuwa wapo katika makazi ya watu.
 Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Alhaj, Majid Hemedi Mwanga akiwa na watendaji kutoka TFS wilaya ya Bagamoyo wakitabasamu baada ya kuona hali ya msitu wa mzigua imeanza kuridhisha.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Bagamoyo, ambae ni Mkuu wa Wilaya ya hiyo Mh. Alhaj, Majid Hemedi Mwanga (aliyeshika fimbo) akiongoza Doria maalum ya kukagua msitu wa Zigua.

 Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Alhaj, Majid Hemedi Mwanga (kushoto) akifurahia jambo na wanakijiji waliotolewa ndani ya msitu wa Zigua kata ya Kibindu hivi karibuni wakati wa Doria maalum ya kukagua Msitu huo.