Monday, March 23, 2026
MAKAMU WA RAIS AONGOZA MAADHIMISHO YA KILELE CHA WIKI YA MAJI 2026
Friday, March 20, 2026
MFALME WA SWEDEN AMUAGA BALOZI MATINYI
Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Mobhare
Matinyi, akiwa katika picha ya pamoja na Mfalme wa Sweden, Carl XVI Gustaf,
wakati alipokwenda kumuaga katika Jumba la Kifalme jijini Stockholm, tarehe 19
Machi, 2026 (Picha kwa hisani ya Jumba la Kifalme).
.......................................................
Mfalme Carl XVI Gustaf wa Sweden, amemuaga aliyekuwa Balozi
wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Mobhare Matinyi, katika hafla fupi iliyofanyika
kwenye Jumba la Kifalme jijini Stockholm, jana tarehe 19 Machi, 2026.
Katika mazungumzo yao mafupi, viongozi hao walijadiliana
namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili katika sekta
za nishati, mazingira, kilimo, utalii, miundombinu, madini na teknolojia.
Mfalme Gustaf aliipongeza Tanzania kwa kuweka utulivu nchini
na kubuni mipango thabiti ya kutafuta maendeleo na kukuza uchumi wake licha ya
changamoto nyingi zinazoikabili dunia nzima hivi sasa.
Balozi Matinyi alimshukuru Mfalme Gustaf kwa ushirikiano
mzuri alioupata katika kipindi alichohudumu nchini Sweden ambapo Tanzania
imefaidika katika sekta za nishati, kilimo, miundombinu, teknolojia na elimu ya
juu.
Hii ilikuwa mara ya tatu kwa Balozi Matinyi kukutana na
Mfalme Gustaf tangu awasili nchini Sweden mwezi Mei 2025. Mara ya kwanza
ilikuwa wakati wa kukabidhi hati zake za utambulisho tarehe 12 Juni, 2025, na
tarehe 9 Desemba, 2025, kwenye mazungumzo ya kibalozi ya mwisho wa mwaka.
Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania, Stockholm, Sweden,
19 Machi, 2026.
Sunday, March 8, 2026
JET YAPONGEZA JUHUDI ZA WANAWAKE KATIKA KUTUNZA MAZINGIRA.
Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kinawatakia heri wanawake wote nchini na duniani katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 8,2026.
JET inatambua mchango mkubwa wa mwanamke katika kulinda na kuhifadhi mazingira.
Kwa muda mrefu wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika matumizi ya rasilimali asilia ndani ya familia na jamii, hivyo kuwa na nafasi muhimu katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Mwanamke ndiye mlezi wa familia na mara nyingi ndiye anayehusika moja kwa moja na matumizi ya nishati ya kupikia, maji, na rasilimali nyingine muhimu za mazingira.
Kupitia nafasi hiyo, wanawake wameendelea kuwa kichocheo muhimu cha utunzaji wa mazingira, kwa kuhamasisha matumizi bora ya rasilimali, kupunguza uharibifu wa misitu, na kuhimiza mbinu rafiki kwa mazingira katika shughuli za kila siku za kijamii na kiuchumi.
Katika maadhimisho haya, JET pia inatoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake thabiti katika kulinda mazingira, hususan kupitia ajenda ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.
Hatua hii ni muhimu katika kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa, kuboresha afya za wananchi, na kuchangia juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
JET inaamini kuwa juhudi hizi zina mchango mkubwa katika kuimarisha maendeleo endelevu na kulinda mifumo ya ikolojia ambayo ndiyo msingi wa ustawi wa jamii na uchumi wa Taifa.
Aidha, JET inatoa wito kwa wadau wote—serikali, sekta binafsi, asasi za kiraia na jamii kwa ujumla—kuendelea kuwawezesha wanawake kwa elimu, teknolojia na rasilimali zitakazowawezesha kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira.
Uwezeshaji wa wanawake katika masuala ya mazingira ni uwekezaji wa moja kwa moja katika mustakabali wa Taifa na dunia kwa ujumla.
Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania kitaendelea kutumia taaluma ya uandishi wa habari kuelimisha umma, kuhamasisha uwajibikaji, na kukuza uelewa kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira kwa maendeleo endelevu.
Imetolewa na:
John Chikomo
Kwa niaba ya
Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET)
Friday, February 20, 2026
Thursday, February 12, 2026
SERIKALI YASHUSHA ADA KWA WANABLOGU.
SERIKALI YASHUSHA ADA KWA WANABLOGU.
TCRA Yazindua Redio ya Kisasa 'DSB'
SERIKALI imetangaza neema ya kihistoria kwa wanablogu, vijana wabunifu, na watoa maudhui mtandaoni nchini kwa kupunguza ada za leseni kwa kiwango kikubwa, hatua inayolenga kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali na kurasimisha shughuli za wahabarishaji wa mitandao.
Hatua hiyo imekuja kufuatia utafiti wa kina na mikutano ya kimkakati ya takribani mwaka mzima kati ya mtandao wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ikielezea vikwazo vya gharama vilivyokuwa vikikwaza uandishi wa habari za kidijitali nchini.
Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Watoa Huduma za Utangazaji (ABC 2026) jijini Dodoma leo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamisi Mwinjuma, amesema ada ya leseni kwa watoa maudhui mtandaoni imeshushwa kutoka Sh500,000 hadi Sh50,000 tu, huku ada ya maombi ikiwa ni Sh10,000 pekee.
Mageuzi hayo pia yamegusa kundi la wakusanyaji wa maudhui (Online Content Aggregators), ambao ada yao imeshushwa kutoka Sh1,000,000 hadi Sh100,000 pekee. Aidha, kundi la "Amateteur" limeanzishwa kwa ajili ya vijana wanaochipukia ili waweze kujitambulisha rasmi na kukuza vipaji vyao bila vikwazo vya kifedha.
Mapinduzi ya Teknolojia ya DSB
Wakati neema hiyo ikitangazwa, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri Bakari, ametangaza kuanza kwa teknolojia mpya ya utangazaji wa redio ya kidijitali nchini inayojulikana kama Digital Sound Broadcasting (DSB).
Teknolojia hiyo itaanza kufanya kazi katika mikoa mitano ya majaribio ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, na Mbeya, lengo likiwa ni kuongeza ubora wa sauti na huduma za utangazaji nchini.
"Tumekamilisha maandalizi yote ya kiudhibiti na watoa huduma wa miundombinu wameshapatikana. Hii ni hatua kubwa ya kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani na kuimarisha utangazaji, hususan maeneo ya vijijini," alisema Dkt. Bakari.
Utafiti: Redio Bado ni Kinara
Katika mkutano huo, Injinia Andrew Kisaka wa TCRA amewasilisha matokeo ya utafiti wa hali ya utangazaji kwa mwaka 2025/2026, ukionyesha kuwa redio inaendelea kuwa chanzo kikuu cha habari kwa asilimia 85 ya Watanzania. Hata hivyo, utafiti huo umebaini ukuaji mkubwa wa matumizi ya intaneti miongoni mwa vijana, ambapo asilimia 45 hupata habari kupitia mitandao ya kijamii kabla ya kusikiliza redio au kutazama televisheni.
Upande wa televisheni, utafiti unaonyesha asilimia 65 ya watazamaji wanatumia ving'amuzi, huku maudhui ya ndani yakipendwa zaidi kwa asilimia 70. Serikali imewahimiza watoa huduma za kienyeji kuwekeza zaidi kwenye majukwaa ya kidijitali (OTT) ili kukidhi mahitaji ya soko la sasa.
Ulinzi wa Hakimiliki na Mikopo
Ili kuhakikisha wanahabari wa kidijitali wanufaika na kazi zao, Serikali imezielekeza taasisi za COSOTA na TCRA kuandaa mpango wa kulinda hakimiliki na kudhibiti uharamia mtandaoni. Aidha, Serikali imeanza kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa watengeneza maudhui kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi.
Hadi kufikia Desemba 2025, TCRA imetoa jumla ya leseni 707 za utangazaji, zikiwemo 318 za maudhui mtandaoni, jambo linaloashiria kukua kwa uhuru wa habari na demokrasia nchini chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Friday, December 19, 2025
ITHIBATI YA WAANDISHI WA HABARI NI NGAO YA TAIFA KATIKA VITA.
SERIKALI YAAHIDI ULINZI NA USHIRIKIANO KWA WAANDISHI WA MTANDAONI.






















































