Tuesday, September 19, 2023
Monday, September 18, 2023
Sunday, September 17, 2023
RC MAKALLA AZINDUA MAJARIBIO YA CHANZO KIPYA CHA MAJI BUTIMBA, KUTATUA UHABA WA MAJI NYAMAGANA NA WILAYA TATU ZA MWANZA, 69BIL ZATUMIKA.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla Septemba 15, 2023 amezindua Majaribio ya Chanzo Kipya cha Tiba ya Maji Butimba kituo ambacho kitazalisha Lita milioni 48 kwa Siku kilichojengwa na Kampuni ya Sogea Satom chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA).
Akizungumza na wananchi baada ya kubonyeza kitufe na kuwasha mitambo ya Maji na hivyo kuanzisha rasmi majaribio Mhe. Makalla amesema katika muda mfupi ujao wananchi wanaoishi Nyamagana Katika maeneo ya Sahwa, Igoma, Kishiri, Wilaya ya Ilemela Nyamhongolo na Kisesa Katika Wilaya ya Magu na Usagara Katika Wilaya ya Misungwi wataanza kupata Maji kutoka katika chanzo hicho kilichogharimu zaidi ya bilioni 69.
Mhe. Mkuu wa Mkoa ametumia hafla hiyo kumshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha ili kutekeleza mradi huo unaotarajia kuongeza uzalishaji hadi lita milioni 138 kwa siku kutokana na chanzo cha sasa kuzalisha lita milioni 90 na miradi mingine inayolenga kuondoa kero ya Maji kwa wananchi Mkoani humo na wataalamu wote waliofanikisha ujenzi wa mradi huo.
Vilevile, Mhe. Makalla amebainisha kwamba kupitia mradi wa LVWATSAN kwa suluhisho la muda wa Kati tayari zabuni kwa ajili ya ujenzi wa mtandao wa mabomba na Matenki makubwa Sita yenye uwezo wa kuhifadhi maji jumla ya Lita milioni 31 imetangazwa na kwamba mkandarasi anatarajiwa kupatikana siku za usoni.
"Ndugu wananchi, napenda kuchukua fursa hii kuwaomba mnapoona maji yakivuja mtaani mtoe taarifa MWAUWASA nanyi mzishughulikie taarifa hizo kwa haraka na kwa umakini ili kuokoa maji, kuwatia moyo wananchi na kuzuia matatizo kama hayo yasijitokeze tena sehemu ileile." Mkuu wa Mkoa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa, Mhe. Sixbert Jichabu amesema chama tawala kina matarajio makubwa kwa serikali yao na Mhe. Rais Samia ameamua kuwaletea huduma bora wananchi na ametoa pongezi kwa
Akiongea kwa niaba ya Wana Nyamagana Mhe Stanslaus MABULA Mbunge Jimbo la Nyamagana amemshukuru Rais wa awamu ya Sita Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Kutoa zaidi ya Bilioni 69 za Mradi huo ambapo toka ameingia madarakani amekuta Mradi huo upo hatua ya awali Ya manununuzi Lakini kwa dhamira ya kumtua ndoo MWANAMKE kichwani ametoa fedha hizo. Mhe Mabula amesema, amehemewa na furaha nyingi kwa maji kuanza kuwafikia wanachi wa pembezoni mwa Nyamagana punde uzinduzi huo unapoanza.
Hafla Hiyo ya uzinduzi imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya NYamagana Mhe Amina Makilagi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe Hassan, Mbunge Jimbo la Ilemela Mhe Angelina Mabula, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi MWAUWASA Mhe Christopher Gachuma pamoja na Wajumbe wake, Kamati ya siasa Nyamagana ikiongozwa na Peter BEGA, Mwenyekiti wa CCM Imelema Yusuph Bujiku pamoja na Kamati za ulinzi na usalama Wilaya ya Ilemela, Nyamagana na Mkoa.
Saturday, September 16, 2023
YANGA SC YACHUNGULIA HATUA YA MAKUNDI CAFC, SIMBA SC YATOKA KIBABE ZAMBIA
NA EMMANUEL MBATILO
Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara wanaendelea kufanya ziara Kimataifa ambapo leo imefanikiwa kuinyuka Al-Merrikh 2-0 mchezo ambao umepigwa kwenye dimba la Pele Kigali nchini Rwanda
Katika mchezo huo Yanga Sc imeweza kupata mabao kupitia kwa washambuliaji wao Kenned Musonda pamoja na Clement Mzize ambapo mabao yote yamefungwa kipindi cha pili.
Kwa upande wa majirani zao Simba Sc ambao walikuwa wanakipiga kule Ndola nchini Zambia wamelazimisha sare ya mabao 2-2, mabao ya Simba Sc yamefungwa na Mzambia Claotos Chama.
WAZAZI BUKOBA WAASWA KUWALINDA WATOTO DHIDI YA UBAKAJI NA ULAWITI.
Na Alodia Babara, Bukoba
Serikali pamoja na Viongozi wa madhehebu ya dini katika Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera wamekemea vitendo vya ubakaji na ulawiti na kuwaasa wazazi kuchukua tahadhari dhidi ya watoto wao ili kuwaepusha na vitendo hivyo ambavyo vinaharibu ndoto za baadae kwa watoto hao.
Viongozi hao wameyasema Septemba 15,2023 kwenye kongamano la watoto, vijana na makundi maalumu lililoandaliwa na shirika lisilo la serikali la Tanzania Youth Development Organization (TYDO) lililopo Manispaa ya Bukoba linalojihusisha na kuibua vipaji vya watoto na vijana kimichezo lengo la kongamano lilikuwa ni kutoa Elimu kuhusu unyanyasaji wa kijinsia.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima akifungua kongamano hilo amesema wazazi wanapaswa kutimiza wajibu wao kwa kuwalea watoto wao katika maadili mema ili badae nao waweze kuwasaidia.
"Kuna wazazi wanakumbatia tabia ovu za watu wanaowanyanyasa watoto wao mfano unakuta mtoto anabakwa au analawitiwa lakini familia mbili zinashirikiana na kumaliza tatizo hilo bila kuhusisha vyombo vya sheria na badae mtoto atakapokua akajua kuwa alifanyiwa kitendo kibaya wazazi wakala fedha bila kuchukua hatua mtoto atachukia sana wazazi, tuache tabia hiyo" amesema Sima
Amesema wazazi wawatunze watoto wao kwa kuwapeleka shule na kuhakikisha wanafuatilia tabia na mienendo ya masomo yao kwani watakaposomesha watoto nao watawatunza badae.
Dc Sima amemtia moyo Mkurugenzi wa Taasisi ya TYDO Shadrack Bernadi kwa kuanzisha Taasisi hiyo ambayo inasaidia kuwaweka pamoja watoto, vijana na makundi maalumu na kutoa elimu kwao jinsi ya kuchukua tahadhari dhini ya watu wanaotaka kuharibu maisha yao.
Kwa upande wa Shehe wa wilaya ya Bukoba Yusuph Kakwekwe amesema kuwa, wazazi wametupilia mbali malezi ya watoto wao, wazazi hawapeleki watoto wao madrasa au shule za jumapili kwa wakristo huko ndiko wangejifunza maadili na kuwa na hofu ya Mungu.
Amesema kuwa, kuna wazazi wanawatuma watoto,vijana wao waende kuhemea bila kuwapa fedha na kuwa wanakuwa wana maana kwamba mtoto aende akatende mambo maovu ili apewe chochote.
"Wewe mzazi unapomtuma mtoto/ kijana aende kuhemea mahitaji ya familia bila kumpa fedha unakuwa unahitaji atoke katika malezi, wazazi mmesababisha talaka ambazo zimekuwa kiini cha watoto kupoteza maadili, mzazi unapata fedheha ukiwa duniani na ahera utaulizwa" amesema Shehe Kakwekwe
Amesema vijana wanaosaka vipaji mbalimbali wanapaswa kuwa na elimu kwani wenye vipaji bila elimu hawana uwezo wa kutunga nyimbo na wanaporomoka haraka.
Akitoa mada ya unyanyasaji wa kijinsia sagent Dorothea Samwel kutoka dawati la polisi Bukoba, ametoa somo kwa watoto na vijana kuacha kupokea vizawadi mbalimbali zikiwemo pipi, chipsi kutoka kwa watu wasio wa karibu nao na kuwa watu hao wanakuwa wanaandaa mazingira ya kuwabaka na kuwarawiti.
Sajant Samwel amewataka wazazi kuacha migogoro kwenye familia zao kwani wanatoa mwanya mkubwa wa waharifu wa watoto na vijana wao na kuwa migogoro hiyo inarudisha nyuma maendeleo ya familia.
Mkurugenzi wa Taasisi ya TYDO Shadrack Bernadi amesema kuwa, kampein ya kupinga unyanyasaji ni endelevu na wamesajiri watoto na vijana 100 ambao wamekuwa wakiwaweka pamoja kwa ajili ya michezo na kuibua vipaji vyao pamoja na kutoa elimu ya kuepukana na unyanyasaji wa kijinsia ambao unahatarisha maisha yao.



















.jpeg)
















.jpeg)

.jpeg)

























.jpeg.jpg)
