Wednesday, September 13, 2023

MATUMIZI YA MAJOKOFU, VIYOYOZI VYA MITUMBA YANACHANGIA KUHARIBU TABAKA LA OZONI-DKT JAFO

 

Serikali imewataka wananchi kuepuka kuingiza nchini na kutumia majokofu au viyoyozi vilivyokiwshatumika (mtumba) ambavyo vinatumia gesi haribifu kwa tabaka la ozoni na badala yake watumie bidhaa zenye uwezo mdogo wa kuchangia ongezeko la joto duniani.


Waziri wa Nchi Ofisi Ya Makamu Wa Rais (Muungano Na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema hayo wakati akitoa Tamko kuhusu Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni jijini Dodoma leo Septemba 13, 2023.


Amesema hayo wakati Tanzania ikitarajia kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni Septemba 16, 2023 kama kumbukumbu ya tarehe ya kutiwa saini Itifaki ya Montreal ya mwaka 1987 kuhusu kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni ambalo kazi yake kubwa ni kuchuja sehemu kubwa ya mionzi ya jua isifike kwenye uso wa dunia. 


Akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa katika utekelezaji wa Mkataba wa Montreal Serikali ilitoa mafunzo kwa maafisa wa mipakani kuwa kutambua vifaa vinavyotumia kemikali haribifu kwa tabaka la ozoni ambalo linapoharibiwa huruhusu mionzi ya jua kufika kwenye uso wa dunia na hivyo kusababisha madhara.


Dkt. Jafo alisema tabaka la ozoni linapoharibiwa husababisha saratani ya ngozi, mtoto wa jicho, upungufu wa kinga dhidi ya maradhi, kujikunja kwa ngozi, kuathirika kwa ukuaji wa mimea pamoja na kuongezeka kwa joto duniani na hivyo kuchangia katika mabadiliko ya tabianchi.


Hivyo, alitoa wito kwa wananchi kununua bidhaa zilizowekwa nembo rasmi isemayo “Ozone friendly” au “low global warming potential” au yaani “sahibu wa Ozoni” au “uwezo mdogo wa kuchangia ongezeko la joto duniani”. 


Madhara mengine aliyataja kuwa ni kuathirika kwa ukuaji wa mimea vile vile, baadhi ya kemikali hizi husababisha kuongezeka kwa joto duniani na hivyo kuchangia katika mabadiliko ya tabianchi.

 

“Ukiangalia mwaka juzi (2021) kuna kazi mbalimbali zilikuwa zikifanyika kwa mafundi wa majokofu pamoja na kutembelea maduka ili kuhamasisha na kutoa mafunzo kwa mafundi ili waweze kutambua madhara yake na kuchukua hatua,” alisema Jafo.

 

Mafunzo hayo yalilenga namna ya kudhibiti uingizaji wa kemikali nchini kwa Maafisa wa Idara za Serikali zilizopo katika Mpaka wa Namanga. 

WATOTO ZAIDI 85,000, BUKOBA KUPATIWA CHANJO YA POLIO.

 

Na Alodia Babara- Bukoba.


Watoto zaidi ya 85,000 wenye umri chini ya miaka nane wanatarajia kuchanjwa chanjo ya polio Halmashuri ya Wilaya ya Bukoba, kuanzia Septemba 21 hadi Septemba 24, Mwaka huu 2023


Mratibu wa chanjo halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Yohana Baruba amesema hayo hivi karibuni, wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema wanalenga kuchanja watoto wenye umri chini ya miaka minane wapatao 85,795 kuanzia Septemba 21 hadi Septemba 24.


Yohana amesema, chanjo hiyo itatolewa nyumba kwa nyumba, mashuleni, makanisani, msikitini, vituo vya kutolea huduma za afya na katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi.


Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Siima 

amesema zoezi hilo ni la kitaifa na si dogo ndio maana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi ili kuwezesha upatikanaji wa huduma hiyo inayotarajiwa kutolewa katika mikoa sita ya Tanzania ikiwemo Kagera.



"Tunapaswa kushirikiana wote kwa hili kuhakikisha tunafanikisha zoezi hilo ikitokea mtendaji yoyote akagoma kwenda kuhamasisha na kueleza umuhimu wa kupata chanjo hii kwa wananchi au kupotosha zoezi,tupate taarifa zake tutamchukulia hatua kwa muijbu wa sheria maana tukiendelea kuwalea na kuwafumbia macho watu wa aina hiyo ni kuliangamiza Taifa" amesema Siima.


Siima amesema baada ya zoezi hilo kumalizika watafanya tathimini kuona mafanikio na changamoto zilizojitokeza ikiwemo kuwabaini watakao kwamisha zoezi hilo.


amesema ni vyema matangazo yanayohusu umuhimu wa chanjo yaendelee kutolewa, ikiwemo kubandika mabango yanayozungumzia tukio hilo, kuwashirikisha viongozi wa dini waweze kutoa matangazo hayo kwenye nyumba za ibada maana hili ni zoezi muhimu kwa ajili ya kunusuru watoto wetu na janga hilo.


"Tumelenga kufikia asilimia 100 tunapaswa kuzidi asilimia hiyo hivyo tunapaswa kukemea upotoshaji wa aina yoyote mfano kuna watu wamekuwa wakitishia kuwa chanjo zina madhara tujipange wote kwa pamoja kukemea hayo.

MAGAZETI YA LEO TAREHE 13 SEPTEMBA 2023.