Tuesday, February 22, 2022

VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI MILIONI 1.6 VIMETOLEWA NCHINI.

 No description available.

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula,akizungumza wakati akifungua  kikao na  viongozi wa  Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini na viongozi wa Wamachinga  kutoka Mikoa 26 nchini kilichofanyika leo Februari 22,2022 jijini Dodoma.

....................................

Na.Alex Sonna, DODOMA

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Zainabu Chaula amesema mpaka sasa vitambulisho vya wajasiriamali milioni  1.6 vimetolewa nchini  kati ya vitambulisho  milioni 3.7.

Pia amesema mikakati iliyopo kwa sasa ni jinsi ya kuwapatia vitambulisho vyao  wajasiriamali milioni  2.1 waliobaki.

Hayo ameyasema leo Februari 22,2022 Jijini Dodoma wakati akifungua  kikao na  viongozi wa  Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini na viongozi wa Wamachinga  kutoka Mikoa 26 nchini, Dk. Chaula amesema kuwa Januari 25 mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan alikutana na viongozi wa  Wamachinga Mkoa wa Dar es salaam ambapo alipokea changamoto na mafanikio wanayokutana nayo.

Amesema kupitia kikao hicho Rais Samia  aliagiza kwamba wamachinga   ni kundi maalum na sasa liwe chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.

Amesema  taarifa aliyonayo ni kuwa  mpaka sasa vimetolewa vitambulisho milioni  1.6 vya wajasiriamali  kati ya vitambulisho  milioni 3.7 huku  mikakati iliyopo kwa sasa ni jinsi ya kuwapatia vitambulisho vyao  wajasiriamali milioni  2.1 waliobaki.

“Lakini taarifa niliyonayo  tunawamachinga milioni  3.7 sasa tunataka hawa waliobaki  milioni 2.1 tunawapaje vitambulisho sasa ndio maana tunatembea na wenzetu wa TAMISEMI watuambie mchakato unaendaje.Kitambulisho ni jambo jema hata sisi ofisini tuna vitambulisho kwahiyo kitambulisho kinakutambua wewe ni nani na upo wapi lile tutaliboresha,”amesema.

Kuhusiana na kuwatambua wamachinga amesema : “Uzuri mifumo  ya Serikali ni endelevu kwahiyo  suala la kutambuliwa sio kwamba walikuwa hawatambuliwi,walitambuliwa na walipata usaidizi wote unaostahili isipokuwa kwa sababu imeanzishwa Wizara mpya yenye mambo mahsusi”

Amesema mgawanyo wa shilingi bilioni 5 zilizotolewa na Rais Samia suala hilo Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) linaendelea kulishughulikia

“Ule mgawanyo uliishatolewa kwa ajili ya kuonesha miundombinu na mchakato unaendelea nina imani tukimaliza haya tutajua tunatokaje Tamisemi wataendelea na uratibu,”amesema.

Kwa upande wake,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Amon Mpanju amesema lengo la kikao hicho cha siku mbili  ni kulipokea hilo kundi kutoka Tamisemi walikokuwa wakiwahudumiwa mara baada ya Rais kuagiza liwe chini ya Wizara hiyo.

Amesema ndani ya siku mbili watapitishwa katika masuala ya uongozi,taratibu za kiuongozi na namna wanavyoweza kujiongoza kuanzia katika masoko mpaka Taifa,mifumo na mbinu mbalimbali za mawasiliano,pamoja na sheria,taratibu na kanuni za kuongoza umoja wao.

Naye,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Machinga nchini Ernest Matondo, amesema kuwa  wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu katika masoko kutokuwa rafiki ambapo ameomba fedha walizopewa zaidi ya shilingi bilioni 5 ziende kukarabati miundombinu hiyo ili waweze kufanya biashara katika mazingira mazuri.

“Nimpongeze Mheshimniwa Rais kwa kulitambua kundi hili maalum na kutupatia Wizara hili ni jambo la kumshukuru sana Mheshimiwa Rais,”amesema.

No description available.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju, akitoa salamu wakati wa kikao na  viongozi wa  Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini na viongozi wa Wamachinga  kutoka Mikoa 26 nchini kilichofanyika leo Februari 22,2022 jijini Dodoma.

No description available.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Onesmo Lyanga,akizungumza wakati wa kikao na  viongozi wa  Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini na viongozi wa Wamachinga  kutoka Mikoa 26 nchini pamoja na Wizara  ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum kilichofanyika leo Februari 22,2022 jijini Dodoma.

No description available.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Patrick Golwike,akizungumza wakati wa kikao na  viongozi wa  Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini na viongozi wa Wamachinga  kutoka Mikoa 26 nchini kilichofanyika leo Februari 22,2022 jijini Dodoma.

No description available.No description available.

Washiriki wa kikao wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula (hayupo pichani) wakati wa kikao na  viongozi wa  Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini na viongozi wa Wamachinga  kutoka Mikoa 26 nchini kilichofanyika leo Februari 22,2022 jijini Dodoma.

No description available.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Machinga nchini Ernest Matondo,akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula (hayupo pichani) mara baada ya kufungua  kikao na  viongozi wa  Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini na viongozi wa Wamachinga  kutoka Mikoa 26 nchini kilichofanyika leo Februari 22,2022 jijini Dodoma.

No description available.

No description available.

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao na  viongozi wa  Shirikisho la Umoja wa Wamachinga nchini na viongozi wa Wamachinga  kutoka Mikoa 26 nchini kilichofanyika leo Februari 22,2022 jijini Dodoma.

 

Wednesday, February 16, 2022

RC KUNENGE AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA BIASHARA PWANI.

 No description available.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa baraza la biashara la Mkoa huo.

.......................................

Na Victor Masangu, Pwani.

 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge l amefungua  mkutano wa baraza la biashara la Mkoa kwa ajili ya kujadili kero na changamoto zinazowakabili wawekezaji pamoja na wafanyabiashara lengo likiwa ni kuzitafutia ufumbuzi na kuweka mikakati ambayo itasaidia kuongeza kasi katika kukuza uchumi.

 

Katika mkutano huo ambao umehudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wawekezaji pamoja na wafanyabiashara umelenga kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kupitia sekta ya biashara.

 

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa kwa sasa lengo kubwa la Mkoa wa Pwani ni kuendelea kushirikiana bega kwa bega na wawekezaji wote pamoja na wafanyabiashara kwa kuwawekea mazingira wezeshi ambayo yatawasaidia katika kutimiza malengo yao.

 

 Aidha aliongeza kuwa katika kufikia malengo ambayo wamejiwekea watahakikisha wanaboresha zaidi huduma ya nishati ya umeme pamoja na miundombinu ya barabara ili kuwapa fursa wawekezaji hao kupata huduma stahiki.

 

 “Katika kikao hiki kitu kikubwa ninachowaomba tujadili mambo ya msingi ambayo yataweza kuleta athari ambazo ni chanya katika suala zima la kufanya biashara zetu ambazo zitakuwa na tija zaidi katika kukuza pato la Taifa,”alisema Kunenge.

 

 Pia alifafanua kwamba ana Imani kubwa kutokana na Mkoa wa Pwani unaongoza kwa viwanda nchi nzima wawekezaji na wafanyabiashara wakiwekewa mifumo mizuri ya kuwasaidia kwa kushirikiana na taasisi wezeshi kutaweza kuleta sura mpya na mabadiliko ya kimaendeleo kwa Mkoa wa Pwani.

 

  “Ukiangalia kwa sasa tuna jumla ya idadi ya viwanda vipatavyo 1,453 ambavyo kati ya hivyo kuna vya kati, vidogo pamoja na vikubwa na uzuri vyote hivi tumeshavifanyia uhakiki kwa hiyo tunazidi kupiga hatua,”alisisitiza Kunenge.

 

 Pia alimpongeza Rais wa awamu ya sita Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza Ilani kwa vitendo katika sekta mbali mbali ikiwemo kutaja vipaumbele vyake nane ambavyo viongozi na watendaji wanapaswa kuvitekeleza katika maeneo yao.

 

Kunenge pia aliongeza kuwa vipaumbele vyote nane ambavyo vimetajwa na Rais Mama Samia Suluhu vyote vipo katika maeneo ya Mkoa wa Pwani ikiwemo suala la kuwa na uchumi wa bluu, ufugaji, kilimo, uvuvi wa baharini pamoja na kutunza mazingira.

 

 Kwa Upande wake Katibu  Tawala wa Mkoa wa Pwani Mwanasha Tumbo alisema kwamba mkutano huo wa baraza la biashara utaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa upande wa wawekezaji pamoja na wafanyabiashara wadogo pamoja na wakubwa.

 

Nao baadhi ya washiriki wa mkutano huo wamempongeza Rais wa awamu ya sita kwa juhudi zake za kuhakikisha anaweka mipango mizuri ya kuwasaidia wawekezaji ili waweze kuwekeza katika Mkoa wa Pwani na kwamba anatekeleza ilani ya chama kwa vitendo.

No description available.