Tuesday, October 26, 2021

BAGAMOYO YAPOKEA BILIONI 1.4 ZA IMF.

 No description available.

 

Halmashauri ya Bagamoyo wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, imepokea Bilioni 1.4 kwaajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ndani ya Halmashauri hiyo.

 

Fedha hizo ni sehemu ya fedha zilizotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF kwa Tanzania, ambazo ni shilingi Trilioni 1.3 kwaajili ya Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19.

 

Wakati huohuo Halmashauri ya Chalinze imepokea jumla ya shilingi milioni 250 ikiwa ni mgao wa tozo za serikali zinazotokana na miamala ya simu ambazo zitatumika kujenga kituo cha Afya Fukayosi.

May be an image of road, tree and sky 

Eneo ambalo litajengwa kituo cha Afya Fukayosi.

May be an image of one or more people, people standing, tree and sky

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo Ndg.Shauri Selenda akikagua eneo ambalo litajengwa kituo cha Afya Fukayosi.

May be an image of standing and outdoors 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo Ndg.Shauri Selenda akikagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Udindivu kata ya Mapinga.

CHALINZE YAPOKEA BILIONI 1.6 ZA IMF

 No description available.

Top of Form

Bottom of Form

Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, imepokea Bilioni 1.6 ambazo zimepelekwa kwenye sekta ya Elimu na X-ray kwaajili ya huduma za Afya.

 

Fedha hizo ni sehemu ya fedha zilizotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF kwa Tanzania, ambazo ni shilingi Trilioni 1.3 kwaajili ya Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19.

 

Katika mgawanyo wa fedha hizo ndani ya Halmashauri, Halmashauri ya Chalinze imepanga kujenga vyumba 66 vya Madarasa katika shule za sekondari 19, ambapo jumla ya kata 15 za Halmashauri hiyo zitafaidika na mpango huo.

 

Wakati huohuo Halmashauri ya Chalinze imepokea jumla ya shilingi milioni 280 ikiwa ni mgao wa tozo za serikali ambazo zitatumika kujenga kituo cha Afya Msata na Bweni la watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya Msingi Chalinze

 

MAGAZETI YA LEO TAREHE 26 OKTOBA 2021.


No description available.

No description available.

No description available.

No description available. 

 

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

WAZIRI GWAJIMA KUZINDUA KITUO CHA ELIMU YA MASAFA MOROGORO LEO.

 No description available.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Doroth Gwajima, Jumanne ya leo tarehe 26 Oktoba 2021, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kituo kipya cha Elimu ya Masafa (CDE), kilichojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani kupitia kituo cha Kuzuia na kudhibiti maradhi (CDC).

 

Sherehe za Uzinduzi huo zitafanyika katika kituo hicho kilichopo mkoani Morogoro, Wilaya ya Morogoro karibu na Mizani ya Zamani, na zitahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Mashiriki ya kimataifa, uongozi wa Mkoa wa Morogoro, Chuo Kikuu Mzumbe na  Mwakilishi Mkazi wa Kituo cha Kuzuia na  Kudhibiti Maradhi cha Marekani CDC, Dr. Mahesh Swaminathan.

 

Ujenzi wa Kituo cha Elimu ya Masafa (CDE) Morogoro, ulianza Januari 2016, kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto na Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Maradhi (CDC). Lengo la Kituo hicho ni kuendelea kutoa mafunzo yenye ubora kwa wafanyakazi wa Afya waliopo kazini, kwa njia ya masafa kupitia mtandao na  Mafunzo ya ana kwa ana.

  

Kituo hicho kitapanua wigo, uratibu, maendeleo na kutekeleza mpango wa Serikali kupitia Wizara ya Afya wa kutoa mafunzo ya masafa na kutekeleza mipango ya elimu kwa walengwa kufikia Viwango vya Kitaifa.

 

Kupitia msaada uliotolewa na Kituo cha Kimataifa cha CDC, Kituo hicho kimefungwa vifaa vya kisasa vitakavyowezesha mafunzo kwa njia ya mtandao kuendeshwa nchi nzima, kutumia teknolojia kuendesha mikutano kwa njia ya video, pamoja na kujenga mfumo wa utunzaji kumbukumbu kwa kozi za masomo ya kielektroniki zitakazokuwa zinatolewa.

 

Wadau wengine walioshiriki kwa karibu kufanikisha kukamilika kwa utendaji wa kituo hicho ni Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na Shirika la Sayansi ya Usimamizi wa Afya (MSH) ambao kwa kiasi kikubwa wameshiriki katika kuandaa mitaala ambayo itasadia kufikiwa malengo ya Kituo ya utoaji huduma za Afya zenye ubora kwa watoa huduma na wadau wa afya nchini kote.

 

Hadi sasa Kituo cha Elimu Masafa kimenufaisha wataalamu wa Afya takribani 34,357, hivyo kukamilika kwa jengo la Kituo hicho kutaongeza idadi ya wanufaika.

 

Mashirika mengine yanayotazamiwa kushiriki sherehe hizo ni pamoja Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), Shirika la Idadi ya Watu Ulimwenguni (UNFPA), Shirika la Menejimenti na Maendeleo ya Afya (MDH), Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na  Utamaduni (UNESCO), Benjamin Mkapa Foundation,  I-Tech Tanzania, Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto (UNICEF), JHPIEGO, Mfuko wa Kimataifa (Global Fund), Amref, CRS, CSSC, PATH, Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania na wadau wengine mbalimbali wanaotoa huduma za Afya nchini.