Saturday, October 23, 2021

WAZIRI MAKAMBA AFANYA ZIARA YA KIKAZI NCHINI SAUDI ARABIA

 No description available.

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba (wa pili kulia) akiwa katika mazungumzo na Mhadisi Adil Saleh Alomair, Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati Jadidifu (wa kwanza kushoto) na Mhandisi Faisal Ali Al Swayed kutoka kampuni ya Advanced Electronics Company (wa pili kushoto) katika Makazi ya Balozi wa Tanzania nchini Saudia Arabia. Wa kwanza kulia ni  Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Ally J. Mwadini.

No description available.

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba akiwa katika mazungumzo na Mhandisi Faisal Ali Al Swayed kutoka kampuni ya Advanced Electronics Company (kushoto) huku Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio (wa kwanza kulia), Kamishna wa Petroli na Gesi,  Michael Mjinja (wa pili kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Saudia Arabia Balozi Ally J. Mwadini wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.

..........................................

Riyadh, Saudi Arabia,

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amewasili nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa mualiko wa Waziri wa Nishati wa Saudi Arabia, Mhe Abdulaziz bin Salman Al Saud.

Akiwa nchini humo Waziri Makamba anatarajiwa kushiriki hafla ya uzinduzi wa “Saudi Green Initiative” utakaofanyika Riyadh tarehe 23 Oktoba 2021 pamoja na kufanya mikutano ya kutangaza fursa za uwekezaji katika sekta ya Nishati nchini Tanzania. 

Mapema baada ya kuwasilia nchini humo, Waziri Makamba alikutana na kufanya mazungumzo na Mhandisi Faisal Ali Al Swayed kutoka kampuni ya Advanced Electronics Company na Mhandisi Adil Saleh Alomair, Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati Jadidifu (Renewable Energy).

Akizungumza na Mha. Faisal Ali Al Swayed, Waziri Makamba alisema “Tanzania imepiga hatua kubwa katika usambazaji wa nishati za gesi asilia na umeme lakini bado kuna uhitaji wa vifaa kama vile mita za kisasa za Gesi Asilia na Umeme kuendana na kasi ya usambazaji na teknolojia kwa ujumla”.

Aidha, Waziri Makamba alieleza nia ya Serikali kutumia zaidi teknolojia kukomesha tatizo la wizi na upotevu wa nishati jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali kuwapatia wananchi nishati ya uhakika.

“Moja ya kazi kubwa tuliyonayo sasa ni kuangalia namna tunaweza kutumia teknolojia kukomesha changamoto hii” alieleza Waziri Makamba na kuwakaribisha wataalamu hao kutembelea Tanzania kwa lengo la kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya Nishati.

Kwa upande wake Mha. Faisal alimhakikishia Waziri Makamba kuwa kampuni yake ina uwezo mkubwa wa kuzalisha mita kwa kuzingatia mahitaji ya mteja na kuahidi kuendelea kuwasiliana na Ubalozi kwa lengo la kuwekeza nchini Tanzania.

Katika ziara hiyo, Waziri wa Nishati, January Makamba ameambatana na Kamishna wa Petroli na Gesi, Michael Mjinja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio.

 

 

MAGAZETI YA LEO TAREHE 23 OKTOBA 2021.

 No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

No description available.

Friday, October 22, 2021

CHALINZE YATILIANA SAINI NA CHINA-TANZANIA FRIENDSHIP PROMOTION KWAAJILI YA UJENZI WA MAJUKWAA UWANJA WA MICHEZO MSOGA.

No description available.

Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze, Ramadhani Posi na Katibu Mkuu wa Tanzania- China Friendship Promotion Association (TCFPA) (kulia) Joseph Kahama, wakitiliana saini kwaajili ya ujenzi wa majukwaa ya kisasa katika uwanja wa michezo wa Msoga, wanne kutoka kulia waliosimama ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akishuhudia utiaji saini huo pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Ismail Msumi, Diwani wa kata ya Msoga Mh: Hassan Mwinyikondo.

.

May be an image of 9 people, people standing and indoor 

 Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze, Ramadhani Posi na Katibu Mkuu wa Tanzania- China Friendship Promotion Association (TCFPA) (kulia) Joseph Kahama, wakibadilishana mikataba ya ujenzi wa majukwaa ya kisasa katika uwanja wa michezo wa Msoga mara baada ya kutiliana saini, wanaoshuhudia ni baadhai ya viongozi wa kata ya Msoga wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete na baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania- China Friendship Promotion Association (TCFPA)

May be an image of 6 people, people standing and indoor 

 Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete, (katikati) akiangalia Mchoro unaoonyesha jinsi majukwaa hayo ya kisasa yatakavyokaa katika uwanja wa michezo wa Msoga.

May be an image of 7 people, people standing and outdoors 


Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete, (katikati) (katikati) akiongoza msafara huo wakiwa katika eneo la uwanja wa michezo wa msoga ambao unatarajiwa kujengwa majukwaa ya kisasa kupitia Tanzania- China Friendship Promotion Association (TCFPA) wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze, Ramadhani Posi na wa pili kushoto ni  Katibu Mkuu wa Tanzania- China Friendship Promotion Association (TCFPA).

May be an image of 3 people and indoor 

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete, akizungumza mara baada ya zoezi la kutiliana saini kukamilika.

 

 

Ujenzi huo unakadiliwa kutumi zaidi ya Tsh Milioni 240 na kwa awamu ya kwanza zitatolewa Tsh. Milioni 60.