Monday, October 18, 2021

MHE. RAIS SAMIA AZINDUA MIRANDI YA MAENDELEO MKOANI ARUSHA

 No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Hospitali ya Jiji la Arusha katika Eneo la Njiro Arumeru Mkoani Arusha tarehe 17 Oktoba 2021. Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Arusha akiendelea na ziara yake ya kikazi kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi Mkoani Arusha.

No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimsalimia mtoto Nassir Mbarouk  aliyezaliwa usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Jiji la Arusha muda mfupi baada ya kuziindua rasmi Hospitali hiyo iliopo katika eneo la Chekereni Arumeru Mkoani Arusha tarehe 17 Oktoba 2021, aliye mshikilia mtoto huyo ni Mama Mzazi  Shadya Samson (32) mkazi wa Uswahilini Arusha. Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Arusha akiendelea na ziara yake ya kikazi kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.

No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimsalimia mtoto Samia Yona  aliyezaliwa usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Jiji la Arusha muda mfupi baada ya kuziindua rasmi Hospitali hiyo iliopo katika eneo la Chekereni Arumeru Mkoani Arusha tarehe 17 Oktoba 2021, aliye mshikilia mtoto huyo ni Mama Mzazi  Mary Joseph (34) mkazi wa Njiro Arusha. Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Arusha akiendelea na ziara yake ya kikazi kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.

No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Chekereni Arumeru Mkoani Arusha mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa Maji safi na Salama unaoendelea katika eneo hilo tarehe 17 Oktoba 2021. Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Arusha akiendelea na ziara yake ya kikazi kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi Mkoani Arusha.

No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Hundi ya shilingi milioni 387,380,675.00 kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Walemavu katika Tarafa ya Themi Mkoani Arusha tarehe 17 Oktoba 2021. Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Arusha akiendelea na ziara yake ya  kikazi kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi Mkoani Arusha.

SERIKALI YAIPA MWANZA BILIONI 344 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

No description available.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akizungumza na  Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Mwanza katika utaratibu wake wa kila wiki wa kutoa taarifa za utendaji kazi za Serikali.

...................................................

Na Ahmed Sagaff – MAELEZO

Mkoa wa Mwanza umepokea shilingi Bilioni 344 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya wananchi katika kipindi cha miezi sita ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Hayo yameelezwa leo jijini Mwanza na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alipokuwa akitoa taarifa ya kazi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita.

Amesema kiasi hicho cha fedha kimeelekezwa kwenye utekelezaji wa miradi ya ujenzi (bilioni 219.1), sekta ya afya (bilioni 15.2), sekta ya elimu (bilioni 38.7), miundombinu ya barabara (bilioni 2.4), usambazaji wa umeme vijijini (bilioni 42.6), miradi ya maji (bilioni 20.4) na mradi wa kusaidia kaya masikini unaotekelezwa na TASAF (bilioni 5.6).

Pamoja na hilo, Msigwa amehabarisha kuwa fedha hizo zitaendeleza ujenzi wa Stendi za Nyamhongolo na Nyegezi, Soko la Kisasa la Mjini, Jengo la Abiria pale kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza,  ujenzi wa MV Mwanza yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 400 za mizigo, na Daraja la Kigongo – Busisi lenye urefu wa kilometa 3.2.

“Tumeleta shilingi Bilioni 8.3 kwa ajili ya kujenga hospitali tatu za Wilaya ya Sengerema, Kwimba na Misungwi, kumalizia hospitali mbili za Wilaya ya Buchosa na Ilemela, kujenga vituo vya afya vitano na zahanati 21 na kukarabati na kujenga vituo vya huduma 48, aidha tumeleta shilingi Bilioni 6.4 kwa ajili ya kununua dawa,” amefahamisha Msigwa.

Akifafanua kuhusu shilingi bilioni 38.7 zilizoelekezwa kwenye sekta ya elimu mkoani Mwanza, Msigwa ameeleza kuwa shilingi bilioni 11 zinaimarisha miundombinu ya elimu kwenye shule za msingi na sekondari huku shilingi bilioni nane zikigharamia mradi wa elimu bila malipo.

“Na tunatarajia kuleta shilingi bilioni 19.7 kwa ajili ya kujenga madarasa 985, hizi ni zile fedha za Mpango wa Ustawi wa Jamii tulizopata kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF),” amedokeza Msemaji Mkuu wa Serikali. 

No description available.

Baadhi ya waandishi wa habari wakipokea vyeti ikiwa ni pongezi kutoka Klabu ya Waandishi  wa Mkoa wa Mwanza, baada ya kushinda Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) kwa mwaka 2020

Tuesday, August 3, 2021

Udugu Social Help welfare yawafariji mayatima Mbagala

 







Na Mwandishi wetu





Taasisi ya Udugu Social Help Welfare yenye Makao Makuu yake Buguruni Jijini Dar es Salaam imefanikisha nia yake ya kuwafariji mayatima wa kituo cha Al-Azim kilichopo Mbagala kwa kujumuika nao na kupata chakula cha pamoja.

Aidha Taasisi hiyo imetoa wito kwa wadau kuendelea kuwakumbuka na kuwajali mayatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu popote pale walipo kwani bado wanazo changamoto nyingi zinazohitaji ufumbuzi.

Akizungumza mara baada ya kupata chakula cha mchana na mayatima, mratibu wa kundi hilo lenye wanachama Zaidi ya 20, Hajat Neema Maumba amesema kilichowasukuma kushiriki chakula pamoja na mayatima ni kuwafariji, wasijione wapweke katika maisha yao.

Amesema ni utaratibu wao wa kila mwaka kushiriki chakula na watoto yatima na wamekuwa wakifanya hivyo katika maeneno mbalimbali katika jiji la Dar es salaam.

Amesema taasisi yao ya Udugu Social Help welfare sio ya kidini na lakini wengi wao ni waislam, wanasaidia watu mbalimbali bila kujali dini zao.

 

“Sisi tunaitwa Udugu Social Help welfare, Makao makuu yetu yapo Buguruni Malapa, tuko wakina mama 20, tulianza kazi mwaka 2009, tumefanya kazi sehemu nyingi na bado tunaendelea,” alisema

Tumesikia majonzi mengi baada ya watoto kueleza changamoto zao, tunamuomba mwenyezi Mungu atuafikishe sisi na wengine tuweze kusaidiana, yatima sio mtoto wa mtu mmoja, ni watoto wetu, kama alivyosema Mtume wetu Muhammad (saw) kwamba katika nyumba yenye yatima wakalala njaa na nyumba nyingine wakala basi watu wote katika mtaa huo wanapata dhambi,” aliongeza

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa taasisi ya kulelea watoto yatima na wenye mazingira hatarishi cha Al-Azam Orphanage center Sheikh Musa Chele ametoa wito kwa wafadhili kuacha kuwatumia watu wa kati kufikisha sadaka zao katika makao ya watoto yuatima.

Amesema kwa muda mrefu watu hao wa kati (agent) wamekuwa wakitumia fursa hiyo vibaya kwa kujinufaisha wao wenyewe badala ya watoto mayatima.

Ametoa mfano katika kituo chake pekee jumla ya milioni 80 zimeliwa na watu wa kati jambo ambalo lina muudhi sana na kuamua kulitolea ufafanuzi.

Aidha akielezea historia ya kituo chao, Sheikh Musaa alisema Kituo chao kimeanzishwa mwaka 2009 kikiwa na watoto 10, wavulana 5 na wasichana 5, hadi kufika mwaka 2021, walikuwa na watoto 60, kati yao wanawake 35 na wanaume 25, aidha kati ya watoto 60, 45 wanaishi katika kituo na wengine wanalelewa wakiwa majumbani mwao.

Amesema Kituo kinakabiliwa na changamoto nyingi, lakini kubwa ni huduma za afya, watoto wengi hawana bima za afya ili kuwasaidia kupata matibabu bila hofu.

Pia amesema kuna changamoto ya rasilimali fedha za kulipa pango la nyumba, ada za wanafunzi, na chakula,  kwa mwezi wanalipa shilingi 300,000 fedha ambazo ni nyingi kwa uwezo wao.

Aidha kwenye upande wa mafanikio kituo kimeweza kununua kiwanja na kuwaomba wadau kuwajengea nyumba ili watoto wakaishi huko na kuepukana na adha ya kupanga.


 

DC Ilala asifu kituo cha yatima cha Amani Foundation Kigamboni

 


Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Bw. Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija akizungumza na waandishi wa habari katika Tamasha la usiku wa Amani lililofanyika katika ukumbi wa Lamada Hotel Ilala Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa kituo hicho Hajat Zubeda Abdallah





Na mwandishi wetu

Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Bw. Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija amesifu ulezi unaofanywa na kituo chawatoto yatima cha Amani Foundation chenye makao makuu yake Kibugumo wilaya ya kigamboni, jijini Dar es salaam.

Aidha Ludigija ameahidi kutoa ushirikiano katika kituo hicho kwani kimethibitisha kuwa hawako kwa ajili ya maslahi binafsi bali kusaidia watoto kufikia ndoto zao.

Akizungumza jiji Dar es salam katika tamasha maalum la usiku wa amani Foundation, Ludigija amesema amewahi kuhudhuria hafla za watoto mayatima nyingi lakini amani foundation wako tofauti na wengine, wenyewe wanawajali watoto jambo ambalo limesababisha vijana kuonekana wenye nuru katika nyuso zao.

Ludigija ambaye alionekana mwenye furaha kuhudhuria hafla hiyo ambayo ilikuwa na  dhamira ya kuwafanya watoto wafurahi amesema ulezi wa amani foundation ni wa kiwango cha juu na ni mfano kwa vituo vingine.

“Nimeambiwa hapa mbali ya kulea yatima lakini pia mnalea vipaji vya watoto hawa, Kwa muda mchache ambao nimefika hapa nimegundua mko tofauti na wengine, vijana wenu wameonyesha uwezo wa hali ya juu katika masuala ya kusifu kupia kaswida zao,

Kunatofauti kubwa kati ya vituo vingine na chenu, sina maana ya kuviponda vingine hapana ila nazungumza kweli, nyie mnafanya kazi kubwa na watoto wanaonekana wanafuraha,” alisema Ludigija.

Aidha ametoa wito kwa vituo vingine kujitahidi kuifanya kazi ya kulea yatima kwa ikhlas, kwani hiyo ni kazi ya kitume, na inayohitaji kujitoa Zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha Amani Foundation, Hajat Zubeida Abdallah amesema kituo chake kina utaratibu wa kuandaa matamasha ili kukutana na wadau kuona vipaji vya yatima lakini pia kupata msaada kutoka kwao.

“Sisi huwa tunaendesha matamasha kama haya kila mwaka, dhamira yetu ni kuwapa furaha watoto, wasione wako wapweke, tunachagua eneno tunakula nao chakula, wanafurahi basi,” alisema

Aidha akizungumzia historia ya kituo hicho, kituo chao licha ya kwamba kina umri mdogo lakini kimeweza kuaminika na jamii kiasi ambacho wapo wadau waliojitolea kuwajengea nyumba.

Amesema kituo kilianza na watoto 4, lakini hadi sasa kina watoto 54 ambao kati yao wapo wanaoishi kituoni na wengine wanaendelea na masomo katika shule za bweni (Boarding).

Kwa upande wake mmoja wa wafadhili wa kituo hicho Hajat Safia Abedi Salum Hafsi ameelezea kufurahishwa kwake na uongozi wa Hajat Zubeida kwani umenyooka na hauna makandokando.

Amesema wao wamekuwa na kituo hicho kwa muda mrefu sasa hawajaona ubadhirifu wowote kitu ambacho kimewavutia kuendelea kuwafadhili.

“Mimi ni mdau wa kituo hiki, ni mmoja wa wafadhili, tuko nao hawa watoto kwa kila hali, hatujawahi kuwaacha peke yao, tunamuomba Allah atuongoze kufanya heri hizi,” alisema

Aidha ametoa wito kwa umma kufika katika kituo hicho kujionea vipaji vya watoto, amesisitiza kuwa ukifika kituoni hapo utajisikia moyo umepoa, watoto wanasoma dua vizuri, hajawahi mtu akasomewa dua akaondoka anasikitika, ni watoto ambao wanakubuli za ajabu.

Kituo cha amani foundation for orphanage ni moja ya kituo kikubwa kwa sasa kilichopo kigamboni, kilianza kazi yake mwaka 2014 kikiwa na watoto 4, sasa hivi wana watoto 54.