Na mwandishi wetu
Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Bw. Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija amesifu ulezi unaofanywa na kituo
chawatoto yatima cha Amani Foundation chenye makao makuu yake Kibugumo wilaya
ya kigamboni, jijini Dar es salaam.
Aidha Ludigija ameahidi kutoa
ushirikiano katika kituo hicho kwani kimethibitisha kuwa hawako kwa ajili ya
maslahi binafsi bali kusaidia watoto kufikia ndoto zao.
Akizungumza jiji Dar es salam
katika tamasha maalum la usiku wa amani Foundation, Ludigija amesema amewahi
kuhudhuria hafla za watoto mayatima nyingi lakini amani foundation wako tofauti
na wengine, wenyewe wanawajali watoto jambo ambalo limesababisha vijana
kuonekana wenye nuru katika nyuso zao.
Ludigija ambaye alionekana mwenye
furaha kuhudhuria hafla hiyo ambayo ilikuwa na dhamira ya kuwafanya watoto wafurahi amesema
ulezi wa amani foundation ni wa kiwango cha juu na ni mfano kwa vituo vingine.
“Nimeambiwa hapa mbali ya kulea
yatima lakini pia mnalea vipaji vya watoto hawa, Kwa muda mchache ambao
nimefika hapa nimegundua mko tofauti na wengine, vijana wenu wameonyesha uwezo
wa hali ya juu katika masuala ya kusifu kupia kaswida zao,
Kunatofauti kubwa kati ya vituo
vingine na chenu, sina maana ya kuviponda vingine hapana ila nazungumza kweli, nyie
mnafanya kazi kubwa na watoto wanaonekana wanafuraha,” alisema Ludigija.
Aidha ametoa wito kwa vituo
vingine kujitahidi kuifanya kazi ya kulea yatima kwa ikhlas, kwani hiyo ni kazi
ya kitume, na inayohitaji kujitoa Zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
kituo cha Amani Foundation, Hajat Zubeida Abdallah amesema kituo chake kina
utaratibu wa kuandaa matamasha ili kukutana na wadau kuona vipaji vya yatima
lakini pia kupata msaada kutoka kwao.
“Sisi huwa tunaendesha matamasha
kama haya kila mwaka, dhamira yetu ni kuwapa furaha watoto, wasione wako
wapweke, tunachagua eneno tunakula nao chakula, wanafurahi basi,” alisema
Aidha akizungumzia historia ya
kituo hicho, kituo chao licha ya kwamba kina umri mdogo lakini kimeweza
kuaminika na jamii kiasi ambacho wapo wadau waliojitolea kuwajengea nyumba.
Amesema kituo kilianza na watoto
4, lakini hadi sasa kina watoto 54 ambao kati yao wapo wanaoishi kituoni na
wengine wanaendelea na masomo katika shule za bweni (Boarding).
Kwa upande wake mmoja wa
wafadhili wa kituo hicho Hajat Safia Abedi Salum Hafsi ameelezea kufurahishwa
kwake na uongozi wa Hajat Zubeida kwani umenyooka na hauna makandokando.
Amesema wao wamekuwa na kituo
hicho kwa muda mrefu sasa hawajaona ubadhirifu wowote kitu ambacho kimewavutia
kuendelea kuwafadhili.
“Mimi ni mdau wa kituo hiki, ni
mmoja wa wafadhili, tuko nao hawa watoto kwa kila hali, hatujawahi kuwaacha
peke yao, tunamuomba Allah atuongoze kufanya heri hizi,” alisema
Aidha ametoa wito kwa umma kufika
katika kituo hicho kujionea vipaji vya watoto, amesisitiza kuwa ukifika kituoni
hapo utajisikia moyo umepoa, watoto wanasoma dua vizuri, hajawahi mtu akasomewa
dua akaondoka anasikitika, ni watoto ambao wanakubuli za ajabu.
Kituo cha amani foundation for
orphanage ni moja ya kituo kikubwa kwa sasa kilichopo kigamboni, kilianza kazi
yake mwaka 2014 kikiwa na watoto 4, sasa hivi wana watoto 54.
No comments:
Post a Comment