Tuesday, January 14, 2020

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI WA ALGERIA, UJERUMANI NA QATAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo jioni Jumanne Januari 14, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani nchini Mhe. Regina Hess kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo jioni Jumanne Januari 14, 2020
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule Taifa la Qatar nchini Mhe. Hussein Bin Ahmed Mohamed Ibrahim Al-Homaid katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo jioni Jumanne Januari 14,2020 

PICHA NA IKULU



Monday, January 13, 2020

WAZIRI MKUU AMTAKA AITAKA TAKUKURU KUKAMILISHA UCHUNGUZI WA KASORO ZILIZOIBULIWA NA MBIO ZA MWENGE MKOANI LINDI.

NA HADIJA HASSAN, LINDI.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzua na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo kukamilishe mapema uchunguzi dhidi ya kasoro zilizoibuliwa katika mbio za Mwenge wa Uhuru 2019.

Pamoja na wizi uliofanywa na viongozi wa AMCOS kwa wakulima wa zao la ufuta na korosho msimu uliopota 2018/2019 Majaliwa ameyasema hayo leo wakati akizindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.


Amesema pamoja na kazi nzuri waliyoifanya na inayoendelea kufanyika na Taasisi hiyo kupitia uchunguzi na ufuatiliaji wa madai ya malipo ya wakulima wa zao la ufuta na korosho lakini inapaswa kukamilisha uchunguzi huo mapema ili hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wote waliohusika Majaliwa.

Alisema rushwa ni miongoni mwa mambo yanayoathiri utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kutokana na ukweli huo, Serikali ya Awamu ya Tano imetoa msukumo wa pekee katika kushughulikia vitendo vya rushwa na ufisadi.

Msukumo huo, umechangia kwa kiasi kikubwa hususan katika kipindi hiki, utekelezaji wa miradi mikubwa na ya kimkakati kwa ufanisi na kwa wakati.

"Kwa mfano, upo Mradi mkubwa wa kihistoria wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha Megawati 2115; Kwa uwekezaji huu pamoja na miradi inayoendelea ya kuimarisha upatikanaji wa umeme kutumia gesi asilia na usambazaji umeme vijijini, wastani wa upatikanaji wa Umeme vijijini umepanda kutoka chini ya asilimia 46 mwaka 2015 hadi zaidi ya asilimia 65 mwaka 2019." Alisema Majaliwa.

Hata hivyo, Majaliwa alisema tafiti za hivi karibuni zilizofanywa na wadau wa mapambano dhidi ya rushwa na Utawala Bora kama vile Transparency International (TI), MO Ibrahim na Afrobarometer zinaonesha kuwa kwa miaka mitatu mfululizo, yaani 2016 hadi 2018 Tanzania imeendelea kufanya vyema katika mapambano dhidi ya rushwa na utawala bora.

Amesema mafanikio hayo ya kujivunia ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kusimamia kwa dhati mapambano dhidi ya rushwa kwa usimamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambayo ndicho chombo kilichopewa dhamana kisheria.

Akizungumzia kuhusu jengo alilolizindua amesema muhimu sana kwa taasisi nyeti kama ya TAKUKURU kumiliki majengo yake yenyewe.

Kuhusu hali ya majengo ya ofisi za TAKUKURU katika ngazi ya mikoa na hata wilaya, Awali kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana a Rushwa (TAKUKURU), Brigedia Jenerali John Mbungo amesema mradi wa jengo hilo umegharimu kiasi cha milioni 142,857,142.86.”  ambapo lilianza kujengwa 11/06/2018 na umekamilika 25/01/2019.

Akizungumzia kuhusu uchunguzi Mbungo alisema kwa kipindi cha mwaka 2019 TAKUKURU imefanya uchunguzi kwenye tuhuma kubwa hasa ikiwemo wa upotevu wa fedha za wakulima wa ufuta wa Mkoa wa Lindi Mbungo alisema Kupitia uchunguzi huo , walibaini kwamba zaidi ya vyama 30 vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) vya Mkoani humo viliwadhulumu wakulima wa zao la ufuta kiasi cha zaidi ya sh.Bilioni sh. 1.23.

Mbungo aliongeza kuwa Kupitia uchunguzi huo waliweza kuwakamata na kuwahoji zaidi ya viongozi 300 wa AMCOS zilizokuwa zinahusika katika dhuluma hii.
Pamoja na kuokoa zaidi ya sh. bilioni 1.042. Ambazo zilikuwa ni mali ya wakulima wa ufuta ambao walidhulumiwa fedha hiyo na Viongozi wa Vyama vya AMCOS.

Nae Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt Mary Mwanjelwa alitumia Fursa hiyo kuwaasa watendaji wa Taasisi hiyo ya TAKUKURU kuyaishi yale wanayoyasema kwa wananchi kuepuka kuomba na kupokea Rushwa ili wananchi wanaowahudumia waendelee kuwa na imani nao

Sunday, January 12, 2020

WAJAWAZITO WASHAURIWA KULA VYAKULA VYENYE VIRUTUBISHO.

NA HADIJA HASSAN, LINDI.

Kina mama wajawazito wameshauriwa Kula vyakula vya aina mbali mbali vyenye Kuzingatia lishe bora vitakavyomsaidia mtoto tumboni kuendelea kukua vizuri.

Ushauri huo umetolewa na Muuguzi Mkunga wa kituo cha Afya cha Mji cha Manspaa ya Lindi Mkoani humo Victoria Mrope hivi karibuni alipokuwa anazungumza na Bagamoyo kwanza Blog.

Mrope alisema mwili wa mama mjamzito unahitaji mlo kamili unaotokana na vyakula vya aina mbali mbali vitakavyomsaidia kupata nguvu na virutubisho vya kutosha.

Aliongeza kuwa miongoni mwa faida ya kula vyakula vyenye lishe kwa mama mjamzito ni kuongeza uzito angalau kilo 12 wakati wa ujauzito kwa wastani wa kilo 1 kila mwezi, kuboresha ukuaji wa mtoto alietumboni kimwili na kiakili, kuzuia upungufu wa Damu.

Alizitaja faida zingine kuwa ni Kuutayarisha mwili kwa ajili ya kunyonyesha kwa kuwa mahitaji ya chakula na virutubisho ni mkubwa unaponyonyesha kuliko unapokuwa mjamzito, kupunguza uwezekano wa kupata mtoto mwenye uzito pungufu pamoja na kujifungua kabla ya wakati au kupata mtoto mfu.

Hata hivyo Mrope pia alisisitiza kuwa mama mjamzito anapaswa kula walau milo 3 iliyokamilika na asusa (vitafunwa ) walau mara 2 kwa siku kwa Kuzingatia makundi ya vyakula.

Nae Mratibu wa Afya ya Uzaji katika kituo hicho cha Mji Faida Saidi alitoa tahadhari kwa kinamama wajawazito kuepuka kula samaki au nyama mbichi au nyama isiyoiva vizuri ili kujiepusha na uwezekano wa kula bakteria na vijidudu vingine hatari kwa Afya ya Mtoto alietumboni.

Tahadhari nyingine ni Mjamzito kutoruhusiwi kula soseji  au sandwich za nyama na vyakula vingine vilivyotengenezwa kwa nyama, kwa kuwa nyama zinazoandaliwa kwa ajili ya kutengeneza vyakula kama hivyo huwa vimewekewa vihifadhi vyakula ambavyo vinaweza Visiwe vizuri kwa mtoto alie tumboni Ulaji wa mayai mabichi au vyakula vilivyochanganywa na mayai mabichi haruhusiwi kuliwa kwani Kuna baadhi ya 'Ice Cream ' na Mayonaizi hutengenezwa kwa kuchanganywa na mayai mabichi pia mjamzito hapaswi Kula kwa ajili ya kulinda Afya ya Mtoto alie tumboni Pia alisema wajawazito wanashahuliwa kutokula samaki wenyekiasi kikubwa cha madini ya zebaki.

Ulaji wa zebaki kwa mama mjamzito umehusishwa na uzaaji wa watoto mataahira huku akieleza mfano wa samaki hao ni pamoja na Papa, Chuchunge na Dagaa wakubwa Ulaji wa maini pia umeelezwa kuwa sio salama kwa mama mjamzito kwa kuwa kuna kiwango kikubwa cha madini ya aina ya chuma na vitamini A ambacho vinaweza kuwa na madhara kwa mtoto alie tumboni endapo kiwango hicho kitazidi Ulaji wa Maziwa mabichi pia yameelezwa kuwa ni hatari kwa mtoto alietumboni kutokana na uwezekano wa kuwepo kwa bakteria aina ya 'Listeria' ambae huweza kusababisha kuharibika kwa mimba.