Sunday, September 8, 2019

NAIBU WAZIRI KANYASU AWATAKA WASOMI WAZIHUDUMIE JAMII ZAO



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na wahitimu wa vyuo vikuu wanaoishi karibu na Hifadhi ambao wametoka familia duni waliosomeshwa na Asasi isiyo ya Kiserikali ya Africa Foundation, And Beyond katika hafla iliyofanyika jijini Arusha ya kuwapongeza baada ya kuhitimu elimu yao.
.......................................

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewataka wahitimu waliomaliza Vyuo vikuu waliosomeshwa kupitia mradi wa kuzisaidia familia duni katika vijiji vinavyopakana na maeneo ya Hifadhi wakumbuke kurudi katika vijiji vyao ili wakawahudumie wananchi wa maeneo hayo.

Pia, Amewataka wahitimu hao wakawe mabalozi wazuri wa kutoa elimu kwa jamii zao juu ya umuhimu wa kulinda Hifadhi kwa vile wao miongoni mwa wanufaika wa shughuli za Uhifadhi nchini.



Akizungumza kwenye hafla ya kuwapongeza wahitimu 50 katika ngazi ya Astashahada na Shadada katika kozi tofauti iliyofanyika Jana usiku mkoani Arusha, Mhe.Kanyasu ameitaja Asasi isiyo ya Kiserikali ya Africa Foundation kupitia kuwa ni moja ya wadau muhimu wa Uhifadhi ambao ni mfano wa kuigwa katika kuzisaidia familia masikini.

Africa Foundationi ni Asasi inayotekeleza mradi wake kwa kusaidia kulipa ada kwa wanafunzi kutoka familia duni zinazoishi karibu na Hifadhi kujiunga na vyuo vikuu nchini kama inavyofanya Bodi ya Mikopo ya Vyuo Vikuu ( HESLB).

Asasi hiyo inayoendesha baadhi ya Hoteli za kitalii ndani ya Hifadhi za Taifa nchini na imekuwa ikisaidia familia duni kwa kuwalipia ada wanafunzi hao ikiwa kurudisha kwa jamii kile walichopata kupitia Hoteli hizo.


Mkopo huo ni tofauti na ule wa HESLB ambapo mara baada ya kusomeshwa na Africa Foundation wanafunzi hao hulipa mkopo huo kwa kuihudumia jamii alikotoka kulingana na kozi aliyoisomea badala ya kurudisha pesa.

Naye, Waziri wa Habari, Utalii na Mambokale, Mhe.Mahamoud amewataka wahitimu hao wakaitumie elimu hiyo kwa kuwasaidia vijana wengine waweze kutambua thamani ya elimu katika maisha yao

” Nendeni huko mkaibadilishe jamii yenu ianze kutambua umuhimu wa kutunza maliasili tulizonazo, alisisitiza Mhe, Waziri Kombo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa mkoa Arusha, Jerry Muro amewataka wanafunzi hao wakaitumie vizuri elimu yao kwa kuanza kuzibadili kifikra familia zao pamoja na jamii kuhusu umuhimu wa kutunza Hifadhi na kuachana na vitendo vya ujangili ili watalii waendelee kuja nchini

” Elimu yenu ikawe silaha kwa wale wote wanajihusisha na vitendo vya ujangili” alisisitiza Mhe.Muro.

Naye Mkurugenzi wa Africa Foundation kwa nchi za Africa Mashariki, Dkt. Mkomeni Mgonho amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuzifanya familia hizo kuthamini na kuona thamani ya shughuli za Uhifadhi.

Aidha, Amesema kuwa pia ni mchango wao wanaourudisha katika jamii kwa kile wanachopata kupitia Hoteli za kitalii.

Mbarouk Salum ambaye ni mhitimu wa fani ya Udaktari katika Chuo Kikuu kishiriki cha Muhimbili amesema kitendo cha Asasi hiyo kuwasaidia kwa kuwalipia ada ni moja ya alama kubwa za matumaini kwa familia hizo ambapo zitaweza kubadili maisha kwa kuandaa kizazi bora kitakachopenda na kuthamini shughuli za Uhifadhi.

Africa Foundation imesaidia kuwalipia ada wanafunzi 45 wa Kitanzania pamoja wanafunzi wa 5 wa kutoka nchini Kenya wote wakiwa wanaishi kwenye vijiji vinavyopakana na Hifadhi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (wa pili kulia) akiwa na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya kale wa Zanzibar, Mhe. Mahamoud Kombo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mhitimu wa Chuo Kikuu mara baada ya kukabidhiwa cheti chake.

Baadhi ya wahitimu wa vyuo vikuu wanaoishi karibu na Hifadhi ambao wametoka katika familia duni waliosomeshwa na Asasi isiyo ya Kiserikali ya Africa Foundation, And Beyond wakiwa wamesimama wakati Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa anawasili ukumbini katika hafla iliyofanyika jijini Arusha ya kuwapongeza baada ya kuhitimu elimu yao.

Monday, September 2, 2019

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MAAFISA WATENDAJI WA KATA WA NCHI NZIMA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. George Mkuchika, Rais wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo, Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurian Ndumbaro,Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Nyamhanga na Naibu Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Francis Michael katika picha ya pamoja na Maafisa Watendaji wa Kata baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata chakula cha mchana na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima wakati wa chakula cha mchana baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. George
Mkuchika, Rais wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo,Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Utumishi Dkt.Laurian Ndumbaro, Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Nyamhanga na Naibu Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Francis Michael katika picha ya pamoja na Maafisa Watendaji wa Kata wa Mkoa wa Lindi baada ya mkutano wao Ikulu ijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019