Sunday, September 8, 2019

NAIBU WAZIRI KANYASU AWATAKA WASOMI WAZIHUDUMIE JAMII ZAO



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na wahitimu wa vyuo vikuu wanaoishi karibu na Hifadhi ambao wametoka familia duni waliosomeshwa na Asasi isiyo ya Kiserikali ya Africa Foundation, And Beyond katika hafla iliyofanyika jijini Arusha ya kuwapongeza baada ya kuhitimu elimu yao.
.......................................

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewataka wahitimu waliomaliza Vyuo vikuu waliosomeshwa kupitia mradi wa kuzisaidia familia duni katika vijiji vinavyopakana na maeneo ya Hifadhi wakumbuke kurudi katika vijiji vyao ili wakawahudumie wananchi wa maeneo hayo.

Pia, Amewataka wahitimu hao wakawe mabalozi wazuri wa kutoa elimu kwa jamii zao juu ya umuhimu wa kulinda Hifadhi kwa vile wao miongoni mwa wanufaika wa shughuli za Uhifadhi nchini.



Akizungumza kwenye hafla ya kuwapongeza wahitimu 50 katika ngazi ya Astashahada na Shadada katika kozi tofauti iliyofanyika Jana usiku mkoani Arusha, Mhe.Kanyasu ameitaja Asasi isiyo ya Kiserikali ya Africa Foundation kupitia kuwa ni moja ya wadau muhimu wa Uhifadhi ambao ni mfano wa kuigwa katika kuzisaidia familia masikini.

Africa Foundationi ni Asasi inayotekeleza mradi wake kwa kusaidia kulipa ada kwa wanafunzi kutoka familia duni zinazoishi karibu na Hifadhi kujiunga na vyuo vikuu nchini kama inavyofanya Bodi ya Mikopo ya Vyuo Vikuu ( HESLB).

Asasi hiyo inayoendesha baadhi ya Hoteli za kitalii ndani ya Hifadhi za Taifa nchini na imekuwa ikisaidia familia duni kwa kuwalipia ada wanafunzi hao ikiwa kurudisha kwa jamii kile walichopata kupitia Hoteli hizo.


Mkopo huo ni tofauti na ule wa HESLB ambapo mara baada ya kusomeshwa na Africa Foundation wanafunzi hao hulipa mkopo huo kwa kuihudumia jamii alikotoka kulingana na kozi aliyoisomea badala ya kurudisha pesa.

Naye, Waziri wa Habari, Utalii na Mambokale, Mhe.Mahamoud amewataka wahitimu hao wakaitumie elimu hiyo kwa kuwasaidia vijana wengine waweze kutambua thamani ya elimu katika maisha yao

” Nendeni huko mkaibadilishe jamii yenu ianze kutambua umuhimu wa kutunza maliasili tulizonazo, alisisitiza Mhe, Waziri Kombo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa mkoa Arusha, Jerry Muro amewataka wanafunzi hao wakaitumie vizuri elimu yao kwa kuanza kuzibadili kifikra familia zao pamoja na jamii kuhusu umuhimu wa kutunza Hifadhi na kuachana na vitendo vya ujangili ili watalii waendelee kuja nchini

” Elimu yenu ikawe silaha kwa wale wote wanajihusisha na vitendo vya ujangili” alisisitiza Mhe.Muro.

Naye Mkurugenzi wa Africa Foundation kwa nchi za Africa Mashariki, Dkt. Mkomeni Mgonho amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuzifanya familia hizo kuthamini na kuona thamani ya shughuli za Uhifadhi.

Aidha, Amesema kuwa pia ni mchango wao wanaourudisha katika jamii kwa kile wanachopata kupitia Hoteli za kitalii.

Mbarouk Salum ambaye ni mhitimu wa fani ya Udaktari katika Chuo Kikuu kishiriki cha Muhimbili amesema kitendo cha Asasi hiyo kuwasaidia kwa kuwalipia ada ni moja ya alama kubwa za matumaini kwa familia hizo ambapo zitaweza kubadili maisha kwa kuandaa kizazi bora kitakachopenda na kuthamini shughuli za Uhifadhi.

Africa Foundation imesaidia kuwalipia ada wanafunzi 45 wa Kitanzania pamoja wanafunzi wa 5 wa kutoka nchini Kenya wote wakiwa wanaishi kwenye vijiji vinavyopakana na Hifadhi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (wa pili kulia) akiwa na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya kale wa Zanzibar, Mhe. Mahamoud Kombo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mhitimu wa Chuo Kikuu mara baada ya kukabidhiwa cheti chake.

Baadhi ya wahitimu wa vyuo vikuu wanaoishi karibu na Hifadhi ambao wametoka katika familia duni waliosomeshwa na Asasi isiyo ya Kiserikali ya Africa Foundation, And Beyond wakiwa wamesimama wakati Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa anawasili ukumbini katika hafla iliyofanyika jijini Arusha ya kuwapongeza baada ya kuhitimu elimu yao.

Monday, September 2, 2019

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MAAFISA WATENDAJI WA KATA WA NCHI NZIMA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. George Mkuchika, Rais wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo, Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurian Ndumbaro,Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Nyamhanga na Naibu Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Francis Michael katika picha ya pamoja na Maafisa Watendaji wa Kata baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata chakula cha mchana na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima wakati wa chakula cha mchana baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. George
Mkuchika, Rais wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo,Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Utumishi Dkt.Laurian Ndumbaro, Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Nyamhanga na Naibu Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Francis Michael katika picha ya pamoja na Maafisa Watendaji wa Kata wa Mkoa wa Lindi baada ya mkutano wao Ikulu ijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019


DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.


Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) wakati akifungua kikao kazi kilichowakutanisha wanasayansi wa hali ya hewa (meteorologists) ili kujadili rasimu ya utabiri/mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli Oktoba hadi Desemba 2019 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tanzania.





Matukio mbalimbali katika picha wakati kikao kazi kilichowakutanisha wanasayansi wa hali ya hewa (meteorologists) ili kujadili rasimu ya utabiri/mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli Oktoba hadi Desemba 2019 kikiendelea. Kikao kazi kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tanzania.


‘Kupitia kikao hiki natarajia kiwango cha usahihi wa utabiri wa msimu huu wa VULI kitakuwa juu zaidi ya misimu yote’, alisema Dkt. Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) .

Alisema hayo wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha wanasayansi wa hali ya hewa (meteorologists) ili kujadili rasimu ya utabiri/mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli Oktoba hadi Desemba 2019 .

Aidha, Dkt. Agnes Kijazi alisisitiza kwa kuwajulisha washiriki hao kuwa TMA inategemea kuzinduliwa rasmi kutoka ‘Agency’ kwenda ‘Authority’ tarehe 05 Septemba mwaka huu, hivyo ni vyema wakatambua kwamba wanapaswa kufanyakazi kwa bidii ili kukidhi mategemeo ya wadau. Alisema, kazi kubwa waliyonayo kwasasa ni kuhakikisha mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli 2019 unakuwa wenye manufaa na tija kwa watumiaji kwa kwa na usahihi na usambazaji wa viwango vya juu zaidi. 

TMA imewakutanisha wanasayansi kutoka vituo vyake mbalimbali nchini ikiwa ni mwendelezo wa utamaduni wake wa utendaji kazi wa pamoja. Mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli 2019 utatolewa rasmi  tarehe 03 Septemba 2019.

WADAU MBALIMBALI WATAKIWA KUCHOCHEA MATUMIZI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KATIKA UCHUMI WA VIWANDA.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma Saidizi Bi. Mariam Is-haaq akimkaribisha Mgeni rasmi kwa ajili ya ufunguzi wa warsha ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za vuli (Oktoba - Desemba 2019) unaotarajiwa kutolewa rasmi tarehe 03 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.
Bw. Wilberforce Kikwasi akichangia mada kwenye warsha ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za vuli (Oktoba - Desemba 2019) unaotarajiwa kutolewa rasmi tarehe 03 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.
Bw. Aloyce Swenya akiwasilisha mada kwenye warsha ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za vuli (Oktoba - Desemba 2019) unaotarajiwa kutolewa rasmi tarehe 03 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.
Bi. Sabiha Mukubwa akiwasilisha mada kwenye warsha ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za vuli (Oktoba - Desemba 2019) unaotarajiwa kutolewa rasmi tarehe 03 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.

Wadau mbalimbali wakichangia mada katika warsha ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za vuli (Oktoba - Desemba 2019) unaotarajiwa kutolewa rasmi tarehe 03 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.

Wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi kwenye warsha ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za vuli (Oktoba - Desemba 2019) unaotarajiwa kutolewa rasmi tarehe 03 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.


By TMA

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kupitia programu ya Huduma za Hali ya Hewa ya kidunia (Global Framework for Climate Services (GFCS)) iliyo chini ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), imekutana na wadau wa sekta mbalimbali ili kujadili na kupata maoni yao jinsi watakavyoutumia utabiri wa msimu wa mvua za vuli (Oktoba hadi Disemba, 2019) unaotarajiwa kutolewa rasmi tarehe 03 Septemba 2019.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa WMO, Dkt. Agnes Kijazi aliwakumbusha washiriki kutambua mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto kubwa katika sekta mbalimbali hivi sasa, hivyo aliwataka washiriki kufanya juhudi za pamoja ili kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinatumika ipasavyo na kuleta maendeleo endelevu hasa kuchochea uchumi wa viwanda katika Taifa letu kwa kuzalisha malighafi zitakazohitajika viwandani.

“Ni matumaini yangu baada ya kikao hiki TMA kwa kushirikiana na ninyi wadau kutoka katika sekta mbalimbali tutahakikisha watanzania wanapata taarifa za hali ya hewa kwa wakati na wanazitumia ipasavyo katika sekta mbali mbali ili kuleta maendeleo endelevu hasa kuchochea uchumi wa viwanda katika Taifa letu kwa kuzalisha malighafi zitakazohitajika viwandani ikiwemo mali ghafi kutoka sekta ya kilimo”, alifafanua Dkt. Kijazi

Aidha Dkt.Kijazi  alisisitiza wadau kupanga mipango ya sekta zao kulingana na utabiri wa hali ya hewa utakaotolewa hapo baadae wenye kujumuisha maoni yao, ikiwa ni moja ya utekelezaji wa maelekezo kutoka Shirika la hali ya hewa Duniani la kutaka taasisi za hali ya hewa kuwahusisha zaidi wadau ambao ndiyo watumiaji wa taarifa za hali ya hewa.

Washiriki wa mkutano huo ulijumuisha sekta ya afya, nishati, maafa, wanahabari, kilimo, uchukuzi, uvuvi, mifugo, NGO, na wataalamu wa lugha (BAKITA).

Sunday, September 1, 2019

Programu Ya Kitalu Nyumba Yawapa Hamasa Vijana Kushiriki Kwenye Sekta Ya Kilimo


Na; Mwandishi Wetu
Programu ya ukuzaji ujuzi kwa vijana kupitia teknolojia ya Kitalu nyumba (Green house) inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imewapa hamasa vijana kushiriki kwa wingi kwenye sekta ya kilimo ikiwa ni chanzo cha kimoja wapo cha ajira nchini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa Ziara yake ya kukagua maendeleo ya mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba, Mkoani Iringa.

Waziri Mhagama alieleza kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu iliamua kuanzisha programu hiyo kwa lengo la kuwawezesha vijana kushiriki kwa wingi kwenye masuala ya kilimo ili waweze kujiajiri wao wenyewe na kuajiri vijana wenzao kupitia teknolojia hiyo.

“Mradi huu unatekelezwa kwenye Halmashauri 185 nchini katika awamu hii ya kwanza ikiwa na lengo la kuwawezesha vijana kuwa na ujuzi pamoja na stadi za kilimo cha kisasa kupitia kitalu nyumba ambacho kina tija katika kuwapatia mazao bora na mengi yatokanayo kwenye eneo dogo,” alieleza Mhagama

Alieleza kuwa Serikali imeendelea kuwawezesha na kuwajengea uwezo vijana wa masuala ya ukuzaji ujuzi ili waweze kuongeza tija kwenye shughuli wanazozifanya na zitakazo wakwamua kiuchumi.

“Vijana wanaweza kupata ajira bora katika kilimo endapo watawekewa mazingira bora kama kuimarisha teknolojia na mbinu za kilimo,” alisema Mhagama.

Hata hivyo aliwasihii vijana kuhakikisha wanatunza vitalu nyumba hivyo kwa kuwa watanufaika navyo na vitawasaidia kufanilisha malengo yao sambamba na kuleta maendeleo endelevu katika sekta ya kilimo.

Aidha alitoa wito kwa wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhakiksha wanawasilisha njia bora zaidi za kuwapata vijana stadi zitakazo wajengea uwezo kupata teknolojia za kisasa zitumikazo katika kilimo pamoja na kuwapatia mitaji ambayo itawawezesha kujenga vitalu nyumba vyao binafsi.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Venerose Mtenga alisema kuwa Ofisi hiyo inatekeleza programu mbalimbali zitakazo wawezesha vijana kupata ujuzi na stadi stahiki zitakazo wasaidia kuondokana na changamoto ya ajira.

Naye Mratibu wa Mradi huo katika Halmashauri ya Iringa Vijijini Bw. Daniel Mlay alisema kuwa jumla ya vitalu nyumba vinne vimejengwa na vijana 431 wameweza kunufaika na mafunzo hayo.

“Tutaendelea kuwahamasisha vijana washiriki kwa kikamilifu katika mradi huu kwa kuwa una manufaa mazuri kwao,” alisema Mlay  

Pia mmoja wa vijana walionufaika kupitia Mradi huo Bw. Ramadhani Haule alieleza kuwa mradi huo wa Kitalu Nyumba umewasaidia kupata elimu bora ya kilimo na umesaidia vijana kuondoka kwenye makundi ya wasiokua na ajira.

“Tunaishukuru Serikali kwa kutuamini na kutupatia ujuzi huu, tunaahidi tutaendelea kushirikiana vijana wengi ili kujikwamua kiuchumi,” alisema

Katika ziara hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alitembelea Vitalu Nyumba vilivyopo katika eneo la Ihemi na Halmashauri ya Mafinga.

Wakazi wa Nyakasangwe na Nakalekwa kupewa hati za viwanja na kurasimishwa rasmi jijini Dar.


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo ametangaza neema kwa wakazi wa Nyakasangwe na Nakalekwa kwa kuwapatia hati za viwanja na kurasmishwa rasmi.

Mh. Chongolo ametangaza amesema hayo wakati alipozungumza na waandishi wa habari habari hiyo njema kwa wananchi hao wa Nyakasangwe na Nakalekwa  eneo ambalo lipo katika Wilaya ya Kinondoni kata ya Wazo jimbo la Kawe.

”Ninachokitangaza rasmi leo ni kwamba, tumefungua zoezi la ugawaji ama utowaji hati kwa wakazi wa maeneo hayo.”Amesema Mh. Daniel Chongolo.

Aidha ameongeza kuwa eneo hilo lilikuwa na mgogoro wa muda mrefu wa zaidi ya miaka 12, na mgogoro huu umeweza kugharimu maisha ya baadhi ya ndugu zetu na pia kusababisha uhasama wa kimakundi.

”Sasa tunatoa fursa na nafasi kwa wananchi wale ambao wapo kwenye yale maeneo na walitambuliwa wakati wa zoezi la utambuzi tunawarasimisha kwa kuwapatia hati, jana nimefanya mkutano huko na wananchi na tumekubaliana yafuatayo”

”Kuanzia Jumanne tunafungua dawati la maafisa wa Wizara, Nida, Halmashauri pamoja na Wataalamu waliyohusika katika zoezi la upimaji na urasimishaji wa eneo la Nyakasangwe na Nakalekwa watakuwepo hapo kwa siku 10. Lengo ni kurahisishwa mchakato wa wananchi wanaohitaji kumilikishwa hati ya ardhi rasmi, kupata haki hiyo bila usumbu”


Friday, August 30, 2019

MICHEZO YA WATOTO HUCHANGIA KATIKA UKUAJI WAO.

Na HADIJA HASSAN, LINDI.

Zaidi ya asilimia 75% ya Watoto wanaolelewa kwenye mazingira ya upweke, (geti kali) na wanaokosa vifaa vya kuchezea katika mazingira wanayoishi huchelewa kufikia hatua za ukuwaji kwa haraka.

Hayo yameelezwa na Mtaalamu wa Lishe wa Manispaa ya Lindi, Mwenda Gellah alipokuwa anazungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG ofisini kwake.

Mwenda alisema kitendo cha baadhi ya wazazi ama walezi kuwalea watoto wao kwenye mazingira ya upweke, kunawanyima watoto hao kutofikia hatua za ukuwaji kwa haraka kutokana na kushindwa kujifunza kutoka kwa watoto wengine.

Alisema hali ya Mtoto kujichanganya katika michezo na watoto wengine ni namna bora ya kupata uchangamshi ambao unamuwezesha mtoto kujenga uwezo wake wa kukuwa kiakili hata kimwili.

Kwa upande wake Muuguzi mkunga wa Kituo cha Afya mji Manspaa ya Lindi Victoria Mlope alisema kuwa kitendo hicho cha wazazi kuwafungia Watoto ndani licha ya kutofikia hatua za ukuwaji kwa haraka lakini pia kitendo hicho kinawafanya watoto hao kushindwa kupata mahusiano ya kijamii na watoto wenzao.

Hata hivyo Mlope aliongeza kuwa michezo kwa mtoto humsaidia kuongeza uwezo wa kujifunza kwa kuujenga ubongo wake ambapo alisisitiza kuwa ni vizuri wazazi wakatenga muda wa kuwaacha watoto wakachanganyika na watoto wezao katika michezo mbali mbali ili waweze kujifunza.

Akizungumzia juu ya Baadhi ya Wazazi/walezi kuwalea Watoto wao kwa geti kali Mkazi wa Manispaa ya Lindi Othumani Mzee alisema kuwa baadhi ya wazazi wanaowalea watoto wao kwa namna hiyo mara nyingi wanahofia tabia ovu kutoka kwa watu wanaowazunguka huku akisema kuwa hiyo ni dhana potofu

“Mtoto anaweza kuwa na tabia ovu hata asipochangamana na watoto wenzake wa Mtaani msingi wa kumlea mtoto unatokana na wazai wenyewe kumfungia mtoto sio suluhisho tunatakiwa kuwafundisha watoto kwa kuwaelewesha lipi zuri na lipi baya bila hata kuwafungia ndani” alisema Chilewa