Wednesday, August 14, 2019

WAZIRI BITEKO ATAKA WANANCHI KULINDA RASILIMALI.

NA HADIJA HASSAN, MTWARA.

WAZIRI wa Madini Dotto Biteko amewataka wananchi kulinda rasilimali ya Madini hapa Nchini ikiwa ni pamoja na kutumia utajili wa Madini uliopo kubadilisha Maisha yao.


WAZIRI Biteko ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na Wananchi wa Kijiji cha Pachani Kata ya Michiga Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu Mkoani Mtwara kuhusu kusitishwa kwa Shughuli ya uchimbaji wa Madini ya Chuma iliyokuwa inaendea Kijiji hapo.


Biteko alisema kuwa kwa miaka mingi utajili wa Madini yaliyopo Nchini yalikuwa yakiwanufaisha wageni huku wenyeji wakiwa bado wanabaki masikini licha ya rasilimali hizo kuwepo kwenye maeneo yao


“Tanzania ni tajili Duniani kwa Madini, hata kwa Afrika mzima sisi ni wanne kwa madini ya dhahabu, wapili kwa madini ya vinto, tunayo Madini mengine mengi ambayo hayapatikani mahali pengine isipokuwa Tanzania nayo ni Tanzanite” alieleza Waziri Biteko


“haiwezekani tunautajili huo halafu watu wetu bado ni masikini ndio maana Rais wetu mnamsikia kila wakati anasema Tanzania sio masikini,


unaweza ukasema kuwa masikini kama uwezo wako wa kufikili hujautumia sawasawa” aliongeza Biteko.


Alisema uwepo wa Madini hayo na madini mengine yanayopatikana Nchini lazima yawe chachu ya kubadilisha Maisha ya Wananchi Hata hivyo waziri Biteko aliongeza kuwa lengo la Serikali la kubadilisha Sheria ya Madini moja wapo ni kutaka kuona rasilimali hiyo inawanufaisha Watanzania

SHEIKH MKUU WA TANZANIA ATEMBELEA MAJERUHI WA AJALI YA MOROGORO.

 Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti, Sheikh, Aboubakar Zubeiry bin Ally, akiongoza  Dua fupi ya kuwaombea majeruhi waliolazwa wodini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutokana na majeraha waliopata katika ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uuguzi wa Muhimbili, Bw. Yassin Munguatosha.

Sheikh Mkuu ametembelea majeruhi wa ajali ya moto na kuwapa pole na kuwaombea Dua ili mwenyezi Mungu awape wepesi wa kupona haraka.

 Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti, Sheikh, Aboubakar Zubeiry bin Ally, akielekea katika wodi walikolazwa majeruhi wa moto katika Hospitali ya Muhimbili.

 Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti, Sheikh, Aboubakar Zubeiry bin Ally, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasaidizi wake pamoja na wataalam wa Muhimbili baada ya kutembelea majeruhi wa ajali ya moto.

WAWEKEZAJI WA MDINI NCHNI WATAKIWA KUWEKA WAZI MAKUBALIANO NA WABIA WAO.

Na Hadija Hassan, Lindi.

Wawekezaji wa Sekta ya Madini Nchini wametakiwa kuweka wazi Serikalini makubaliano wanayowekeana na Wageni wanaoshirikiana nao katika biashara za uchimbaji wa madini katika maeneo mbali mbali hapa Nchini.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Madini Doto Biteko alipotembelea Machimbo ya madini ya Vinto katika kijiji cha Nditi halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi.

Kauli hiyo ya Biteko imekuja baada ya kubaini uwepo wa ubia baina ya Kampuni ya Ngwena ya Hapa Nchini inayofanya shughuli ya uchimbaji wa Madini katika Kijiji hicho cha Nditi na Kampuni ya Indiana ya Nchini Australia ambapo Kampuni ya Indiana hutoa Fedha kwa ajili ya utafiti wa Madini unaoendelea kijijini Nditi lakini Kampuni hiyo (Indiana) haionekani popote katika nyaraka zilizopo Serikalini.

Biteko alisema ili Serikali iweze kufuatilia kwa karibu na kubaini kinachoendelea katika Shughuli zote za uchimbaji wa Madini hapa Nchini ni wajibu kwa kila Mwekezaji katika Sekta hiyo kuweka wazi makubaliano wanayoyafanya na washirika wao katika Wizara ya Madini.

Aliongeza kuwa hata katika Sheria ya madini inaeleza wazi kuwa Mtu yeyote aliyepewa kibali cha uchimbaji hapa Nchini hapaswi kumuingiza muwekezaji wa Nje pasipo Wizara husika kujua amesema kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa Sheria za Nchi.

“....wawekezaji wote wanaojihusisha na uchimbaji wa Madini hapa Nchini ni lazima wajue kwamba wanapoleta Mgeni kutoka Nje ili kushirikiana nao kwenye Mradi basi lazima kuwe na uwazi, na kiasi gani cha fedha kinatumika ikiwa ni pamoja na kuonyesha kwenye mkataba kuwa mradi huo ni wa nani.

La muhimu kwetu Serikali ni kuona kama makubaliano hayo yanakiuka sheria za Nchi kama hayakiuki mtaendelea na makubaliano yenu” alifafanua Bitteko Aliongeza kuwa lengo kubwa la Serikali katika jambo hilo ni kulinda maslahi ya Muwekezaji mzawa dhidi ya mikataba wanayoingia na Wageni akisema kuwa wajibu wa serikali ni kuhakikisha muwekezaji mzawa hawezi kunyonywa na mgeni.

Aidha Waziri Biteko alizidi kusisitiza kwamba serikali haitakubali makubaliano yoyote yatakayoingiwa na Muwekezaji mgeni na kuruhusu mapato yanayotokana na uchimbaji huo zaidi ya asilimia 95 yakaenda kwa mgeni.

Tuesday, August 13, 2019

Majeruhi mwingine ajali ya Morogoro afariki....13 Bado Hawajitambui na Wako ICU


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  (RC) nchini Tanzania, Dk Stephen Kebwe amesema vifo vinavyotokana na ajali ya mlipuko wa moto iliyotokea Jumamosi iliyopita ya Agosti 10, 2019 mkoani humo vimeongezeka na kufikia 76.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Agosti 13,2019 nje ya chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, RC Kebwe amesema idadi hiyo imefikia baada ya majeruhi mmoja aliyelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam kufariki usiku wa kuamkia leo.

Amesema majeruhi waliosafirishwa kwenda Muhimbili wengi walikuwa katika hali mbaya kwa sehemu kubwa ambapo mpaka sasa (asubuhi) wamebakia 38 wakiendelea na matibabu na katika Hospitali ya Rufaa Morogoro wamebaki 16 nao wakiendelea na matibabu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminieli Aligaesha  amesema  Majeruhi 13 kati ya hao  38 walionusurika katika ajali hiyo, waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), hali zao bado ni  mbaya na wamelazwa katika Chumba cha wagonjwa Mahututi (ICU) wakiwa hawajitambui.

“Hadi leo Agosti 13, hiyo ndiyo idadi ya wagonjwa waliolazwa MNH, na wale ambao wamefariki tayari miili yao imepelekwa Morogoro na mmoja umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hapa Muhimbili,” amesema Aligaesha