Thursday, June 13, 2019

BODI YA KOROSHO YATOA MAFUNZO YA VIUATILIFU LINDI.

NA HADIJA HASSAN- LINDI

KUTOKANA na matumizi madogo ya viuwatilifu vya zao la korosho uliojitokeza katika Msimu wa mwaka 2018/2019 Bodi ya korosho Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya utafiti wa Kilimo Naliendele pamoja na TPRI imeanda mafunzo ya matumizi sahii ya viuwatilifu hivyo katika Mikoa yote inayolima zao hilo Hapa Nchini

Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Francis Alfred alipokuwa akitoa salamu za bodi hiyo katika uzinduzi wa mafunzo ya Matumizi ya Viuwatilifu yaliyofanyika katika kata ya Maumbika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani Humo

Alisema matumizi hayo madogo ya viuwatilifu yamechangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa uzalishaji wa zao hilo kutoka tani laki 313,000 za mwaka 2017/2018 hadi tani laki 214000 kwa mwaka 2018/2019.

Alisema mafunzo hayo hasa yanalenga makundi matatu ambayo ni wakulima wa zao la korosho, wapuliziaji wa viuwatilifu pamoja na maafisa ugani ambao baada ya mafunzo hayo watatakiwa kuwafundisha watu wengine katika makundi yao ambao hawakupata fursa ya kushiriki katika mafunzo hayo.

Alfred aliongeza kuwa Bodi ya korosho kwa kutambua uhaba wa maafisa ugani iliona njia sahihi ya kuwafikia wakulima hao kwa wingi na haraka zaidi ni kuyakutanisha makundi hayo na kuyapa mafuzo kwani wamekuwa wakipokea malalamiko mengi kutoka kwa wakulima kutokujua kiwatilifu sahihi kwa ugonjwa sahihi

Nae kaimu mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya utafiti wa Kilimo Naliendele DKT, Fortunus Kapinga alisema katika mafunzo hayo washiriki watapata fulsa ya kujifunza njia na namna bora ya kutumia viuwatilifu, namna ya utunzaji bora wa viuwatilifu pamoja na jinsi ya kujilinda na viwatilifu hivyo ili usipatwe na madhara wakati wa kuvitumia

Hata hivyo DKT Kapinga alitumia fulsa hiyo pia kuishauri Bodi ya korosho kuendelea na utaratibu wa kuwa na mafunzo maalumu kwa maafisa ugani kila mwaka ili kukabiliana na magonjwa mbali mbali yanayoweza kuibuka katika misimu ya zao hilo

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Godfrey Zambi alisema pamoja na mafunzo wanayotakiwa kupatiwa washiriki hao pia wawafundishe jinsi ya kutunza Mazingira ikiwa pamoja na Namna ya kuteketeza vifungashio ambavyo vilitumika kuwekea viuwatilifu huku akiwataka watumiaji wa viwatilifu hiyo kutotumia vifungashio hivyo kwa matumizi ya nyumbani

“viuwatilifu vingi vinavifungashio, kunamifuko ya viuwatilifu vya unga, kunachupa kubwa na ndago, tunajiuliza baada ya kupuliza tunatupa wapi? Yapo mashamba ukizunguka unakutata na chupa zimetupwa hovyo, unakutana na mifuko tena mbaya zaidi hii mifuko tukimaliza kupulizia tunaiyosha alafu tunatiliamaindi tunaenda kusaga wengine wakimaliza kupuliza chupa anaosha anaweka chuvi au sukari.

Naomba tusaidiane baada ya kuwa tumetumia viuwatilifu vifungashio hivi tunavitupa wapi?” alieleza Ndemanga

Hata hivyo Ndemanga alitumia fulsa hiyo kuzitaka mamlaka zinazohusika na usambazaji wa viuwatilifu kufanya udhibiti wa uuzwaji holela wa viuwatilifu pamoja na maeneo yanayotumika kuuzia viuwatilifu ili kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza

Nae ibrahimu Ngalondola akizungumza kwa niaba ya wakulima wengine alisema kuwa miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo katika zao hilo ni bei kubwa ya viuwatilifu jambo ambalo huchangia kwa kiasi kikubwa kwa wakilima hao kushindwa kuandaa mashamba yao kwa wakati

SERIKALI KUENDELEA KUTUMIA LUGHAA MBILI ZA KUFUNDISHIA.

Image may contain: 1 person, sitting
Wazari wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema suala la lugha ya kufundishia na kujifunzia ni la kisera kama iliyotamkwa katika Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.


Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo Bungeni ambapo amesema Sera hiyo imebainisha matumizi ya lugha mbili za Kiswahili na Kiingereza ambapo lugha ya Kiswahili inatumika kufundishia katika ngazi ya Elimu ya Awali na Msingi, Vyuo vya Ualimu ngazi ya Cheti na Vyuo vya Ufundi Stadi wakati lugha ya Kiingereza inatumika katika ngazi za Elimu ya Sekondari, Vyuo vya Kati ba Vyuo Vikuu.


"Hii ni kwa sababu ya umuhimu wa lugha hiyo katika masuala ya Kitafa, Kikanda na Kimataifa kwa mawasiliano na biashara ili kuwajengea wanafunzi ufahamu na umahiri ktk lugha hiyo," amesisitiza Prof. Ndalichako.


Waziri Ndalichako amesema Kutokana na umuhimu wa lugha ya Kiingereza serikali itaendelea kutumia lugha mbili katika kufundishia pamoja na kuimarisha matumizi ya lugha ya kiswahili ili Watanzania wengi zaidi kunufaika na fursa zinazojitokeza nje ya nchi.


Aidha, amesisitiza kuwa Serikali itaangalia utaratibu wa kutumia Vyuo vilivyopo kuandaa walimu wanaofundisha shule za English Media nakuendelea kukitangaza kiswahili ikiwa ni pamoja na kutumika ktk mikutano ya Afrika mashariki na kufundishwa nje ya nchi.


Tuesday, June 4, 2019

JELA MIAKA 30 KWA KUKUTWA NA BANGI.

NA HADIJA HASSAN, LINDI.

MKAZI wa Kijiji cha Majengo, Kata na Tarafa ya Mtama, Wilaya ya Lindi, Ramadhani Haji Juma {23} amehukumiwa kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka {30}, baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na Madawa ya kulevya aina ya Bangi yenye uzito wa Kilo 7.8 kinyume cha Sheria.


Hukumu hiyo imetolewa juzi na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Lindi, Liliani Rugalabamo, baada ya Mshitakiwa kukiri kosa lililomkabiri bila ya kulazimishwa.


Baada ya Mshitakiwa kukiri kosa, Hakimu Rugalabamo alimuuliza mshitakiwa kama anazo sababu zitakazoishawishi Mahakama isimpe adhabu kali, ambapo Ramadhani Haji Juma aliomba asipewe adhabu kali, akidai ni mkosaji wa mara ya kwanza na alilazimika kujiingiza kwenye Biashara hiyo kwa lengo la kujipatia riziki ya kila siku.


“Mh. Hakimu naiomba Mahakama yako tukufu inisamehe na sitarudia kufanya kosa la aina hii tena kushiriki kazi hii ”Alisema Ramadhani.


Kufuatia utetezi huo, Hakimu Rugalabamo alirejea kwa Mwanasheria wa Serikali, Yahaya Gumbo iwapo anazo kumbukumbu za Makosa ya zamani kwa mshitakiwa na kujibu hana, huku akiiomba Mahakama impatie adhabu kali ili iwe fundisho kwake na wengine walio na tabia ya aina hiyo.


Hakimu Rugalabamo akimpatia mshitakiwa adhabu Stahiki katika kesi hiyo Namba 41/2019, alipinga utetezi huo kwa kusema hauna mashiko, kwani zipo njia nyingi za halali kama vile kuitumia Aridhi iliyopo kuzalisha Mali, yakiwemo Mazao ya Chakula na Biashara ili kuondokana na umasikini.


Akimpatia adhabu kwa mshitakiwa huyo kupitia kifungu cha 15 (A) kifungu kidogo cha kanuni ya kuzuia matumizi ya Madawa ya kulevya 2015 kilichofanyiwa Marejeo na Act 15/2017, Rugalabamo alimuhukumu kwenda Gerezani miaka (30).


Mwanzoni ilidaiwa Mahakamani hapo na Mwanasheria wa Serikali yahaya Gumbo, kuwa mshitakiwa alikamatwa eneo la Mitwero katika Manispaa ya Lindi na Askari WP 7203 D/C Kibibi, Mei 14 mwaka huu, kufuatia Gari namba T.540 DQJ alilokuwa akisafiria Mtuhumiwa huyo kufanyiwa ukaguzi.


Gumbo alidai kwamba katika ukaguzi huo, ndipo Askari Kibibi aliweza kubaini Madawa hayo ya kulevya aina ya Bangi yenye ujazo wa Kilo 7.8, yakiwa yamefungwa ndani ya mfuko wa Plastiki na kuwekwa kwenye Begi alilokuwa amewekea Nguo.

Monday, June 3, 2019

TFS BAGAMOYO YAKAMATA MKAA WA MAGENDO.

Wakala wa huduma za misitu nchini (TFS) wilaya ya Bagamoyo wamekamata mkaa magunia zaidi ya mia mbili yaliyokuwa yanapitishwa kwa njia za magendo.


Mkuu wa kikosi cha doria kutoka Wakala wa Huduma za Misitu TFS wilaya ya Bagamoyo, Yusuf Haruna amesema mkaa huo wameukamata kufuatia taarifa za wasamaria wema.


Amesema mkaa huo ulipakiwa kwenye Jahazi na kufichwa kwenye mkondo wa Bahari ya hindi unounganishwa na mto Ruvu wakisubiri kusafiri kuelekea Zanzibar.


Aliongeza kuwa, mara baada ya kupata taarifa hizo kikosi cha doria kilifika eneo la tukio ambapo kimekuta Jahazi hilo likiwa na mzigo huo huku mmiliki wa mkaa huo akiwa amekimbia.


Alisema utoroshaji wa mazao ya misitu ni makosa kwa mujibu wa sheria hivyo mzigo unaokamatwa unataifishwa kwa mujibu wa sheria huku chombo kilichobebwa hupigwa faini.


Akizungumzia hali ya utoroshaji wa mazao ya misitu kwa wilaya ya Bagamoyo, Mkuu huyo wa kikosi cha doria wilaya ya Bagamoyo, alisema bado kuna hali ya utoroshaji wa mazao ya misitu lakini kikosi chake kimejipanga kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa wilaya hiyo wandhibiti mianya yote inayotumika.


Na Meneja msadizi wa kanda maalum ya Saadan wilaya ya Bagamoyo, Hadija Msuya ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mazao ya misitu katika wilayani humo kufuata sheria za uvunaji na usafirishaji wa mazao ya misitu.


Alisema ni vyema wafanyabiashara hao wakafuata sheria katika kuvuna na kusafirisha ili kuepuka usumbufu unaoweza kuwapata.


Alisema TFS wilaya ya Bagamoyo imejipanga kuhakikisha inadhibiti vitendo vyote vinavyokiuka sheria za uvunaji na usafirishaji wa mazao ya misitu.


Aliwataka wananchi kutoa ushirikiano ili kubaini vitendo vya kiharifu ili kunusuru misitu katika wilaya hiyo.
    
Kikosi cha doria kutoka Wakala wa Huduma za Misitu TFS wilaya ya Bagamoyomara baada ya kukamata jahazi lililobeba mkaa na kufanikiwa kulifikisha bandari ya Bagamoyo na kutaifisha mkaa huku jahazi hilo likiwa chini ya ulinzi.

 

Jahazi likiwa limebeba mkaa wa magendo baada ya kukamatwa kama linavyoonekana likiwa katika bandari ya Bagamoyo.

WANANCHI LINDI WASHAURIWA KUTUMIA KIFAA CHA UMETA ILI KUPATA NAFUU YA KUUNGANISHIWA UMEME.

NA HADIJA HASSANI, LINDI.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa Nishati vijijini Rea Mhandisi Amos Maganga amewashauri wananchi wa Mkoa wa Lindi kutumia kifaa cha umeme tayari UMETA Kuunganisha umeme katika Nyumba zao ili kuondokana na gharama za kuweka mfumo wa umeme.

Mhandisi Maganga ameyasema hayo leo Juni 03, 2019 mara baada ya kukagua Maendeleo ya Mradi wa usambazaji wa umeme vijijiji REA katika Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi alipokuwa ameongozana na Wataalamu wa Bodi hiyo.

Maganga alisema huenda idadi ndogo ya wateja waliounganishwa kwa ajili ya kupata huduma ya Umeme inatokana na gharama kubwa ya kuweka mifumo ya umeme katika nyumba zao hivyo kupitia kifaa hicho wananchi wataweza kuunganishiwa huduma hiyo pasipo kuweka mifumo hiyo.

Alisema serikali kwa kutambua kuwa umeme huo wa Rea unaenda vijijini tena kwa wananchi walio wengi ilionelea kuwaletea kifaa hicho cha UMETA ili waweze kupata huduma hiyo ya Umeme kwa gharama nafuu zaidi.

Alisema vifaa hiyo vimetolewa 250 kwa kila mkoa ambavyo vinapaswa kuunganishwa bure kwa wateja wapya wa awali wa mradi huo wa Umeme vijijini.

Nae Msimamizi wa miradi ya Umeme Vijijini Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Lameck Njambo alisema kifaa hicho cha Umeme tayari UMETA hakina tofauti na mfumo wa kawaida wa umeme.
Alisema kifaa hicho huwa kina uwezo wa kuwasha taa, kutumia jiko la umeme, Tv, feni, friji pasi na vifaa vingine vya umeme kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Lindi Felisian Makota alisema kuwa kati ya wateja 5000 wanaotarajiwa kuunganishiwa umeme kupitia Mradi huo wa umeme vijijini Rea ni wateja 290 Peke ndio waliounganishiwa kwa sasa.