Tuesday, May 7, 2019

TECNO YADHAMINI WANAFUNZI MLIMANI.







Kampuni ya simu nchini, TECNO imedhamini mashindano ya wanafunzi wanaojifunza lugha na tamaduni za kichina katika chuo kikuu cha mlimani kwa kushirikiana na taasisi ya Confucius iliyopo chuoni hapo.


Mashindano hayo yamefanyika katika ukumbi wa chuo uliopo katika jingo jipya la library iliyojengwa kwa udhamini wa watu wa china, yalishirikisha    takribani washiriki  kumi na mbili ambapo wote walikua ni wanafunzi  wa chuo kikuu cha mliman.

Akizungumza wakati wa mashindano hayo meneja mahusiano, bwana Eric Mkomoye alisema kua  TECNO imesaidia kuwapa nafsi vijana  wa ktanzania  wanaotamni kutimiza ndoto zao kupitia kujifunza tamaduni za nchi nyingine  hasa katika kukuza  taaluma zao pia kuweza kuwasiliano na watu wa mataifa mbalimbali, aliendelea kwa kusema  kampuni yao  pamoja na  taasis ya Confucius wametoa zawadi mbalimbali ikiwemo  simu aina ya spark 3 pia safari ya kwenda nchii china kujifunza zaidi kw awashiriki washindi wawili.

 
Mashindano ya kuongea kichina katika chuo kikuu cha mlimani hua yanfanyika kwa usimamizi mkubwa wa taasisi ya Confucius iliyoanzishwa mwaka 2013 kwa makubaliano kati ya chuo kikuu cha mlimani na makao makuu ya taasisi ya Confucius yaliyopo Hanban na Zhejiang yakihudhuriwa na makamu wa chuo kikuu cha mlimani  Prof. Rutinwa , mkuu wa utamaduni kutoka  ubalozi wa China bwana Gao Wei.

Mwaka jana na mwka huu TECNO mobile imedhamini mashindano haya  na kuyaboresha kwa kuongeza zawadi kwa washindi, washiriki na hata wahudhuriaji  kwa njia  ya bahati nasibu,

Kampuni ya TECNO kwa sasa inayotangaza simu yake mpya  aina ya TECNO Spark 3  imeeendlea kudhamini matukio mbalimbali yanayohusu  jamii  hasa katika kukuza vipaji vya vijana wa kitanzania na kufanikisha ndoto zao kupitia majukwaa mbalimbali ikiwemo ile maarufu ya kua shujaa wangu.

Monday, May 6, 2019

WAZEE CHALINZE WAMFAGILIA NJIA KIKWETE.

 
Na Shushu Joel.


WAZEE wa Halmashauri ya chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wamemtabilia Mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete kuwa kuna siku anaweza akaja kuwa kiongozi mkubwa wa nchi hii.


Utabili huo wa wazee hao unatokana na jinsi Mbunge huyo anavyojituma katika utendaji wake wa kuwaletea wananchi wa jimbo hilo maendeleo makubwa waliyokuwa wakiyahitaji.


Wakizungumza mara baada ya kikao cha kujadili maendeleo ya jimbo hilo wazee hao walisema kuwa nguzo kubwa ya kiongozi bora ni unyenyekevu, upendo, mshikamano na utii ambapo wamesema hizo zote Ridhiwani Kikwete  anazo hivyo ni lazima atafika mbali.


Kwa upande wake Shehe Lukatili ambaye ni kiongozi wa msikiti kata ya Miono alisema kuwa Ridhiwani amekuwa msaada mkubwa kwao kutokana na vile utekelezaji wake wa miradi ya maendeleo anavyoufanikisha kwa wananchi.


"Mie kwa niaba ya wazee wenzangu wa kata ya Miono tunamuombea Mbunge wetu Ridhiwani Kikwete aweze kuishi maisha marefu yenye baraka ili baadae aje kuwa kiongozi mkubwa katika taifa hili "alisema.


Aliongeza kuwa siku zote nyota njema uonekana asubui hivyo nyota ya kijana huyu imeanza kuonekana na sie kama wazee tunamtakia kila la heri katika kuwatumikia watanzania.


Naye Muhammed Mzimba alisema kuwa Ridhiwani amekuwa kiongozi wa kuigwa na vijana wengi hapa nchini kutokana na ujasiri wake wa kusimamia jambo na kulifanikisha ili umma unufaike.


Aidha aliongeza kuwa ufanikishaji wa miradi mikubwa kwenye jimbo lake la chalinze kuna pelekea wazee na watu wengine jimboni kuona kuwa Ridhiwani ni mkombozi wa Chalinze.


Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete alisema kuwa yeye hana pingamizi lolote kwani wazee wanaona jinsi ninavyowapambania jimboni na pia ni haki yao kumuombea kwa Mungu ili awafanikishie zaidi ya hapo.


Aliongeza kuwa anaipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa juhudi zake inazozifanya kwa kuhakikisha chalinze inakuwa ni jimbo lenye maendeleo ya kutosha.


"Kwa kweli nakumbuka kipindi ambacho tulikuwa tukiomba kura mh Rais Dkt John Pombe Magufuli alituambia wanachalinze watasahau shida na sasa yanaonekana kwani serikali inaleta miradi mingi ya maendeleo chalinze ikiwemo umeme, huduma za afya, miundombinu na sasa inapambana kumaliza changamoto za maji kwa jimbo zima"Alisema Kikwete.


Aidha amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Dkt Magufuli kwani ni kiongozi mwenye kupenda wanyonge.

AJERUHIWA NA SIMBA NA KULAZWA HOSPITALI.

NA HADIJA HASSAN, LINDI.

KIZITO Mathey Mgogo (59) Mkazi wa Kata ya Rutamba, Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi amelazwa katika Hospitali ya Mkoa huo, Sokoine, akiugulia majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na Simba nyakati za usiku.


Hayo yameelezwa na mdogo wake Michael Mathei alipokuwa akizungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG Jana Mei 05, 2019, ilipotembelea Hospitalini hapo.


Michael akizungumzia mkasa huo, alisema kaka yake anayekabiliwa na tatizo la akili, alipatwa na mkasa huo Aprili 26/2019, kati ya Saa 5:00 na 6:00 usiku akiwa amejilaza kwenye Kibanda kinachotumiwa na wajasiliamali wadogo wa kuuza Chakula.


Alisema siku hiyo Kizito akiwa anarejea Nyumbani kutoka katika mihangaiko yake, alipofika eneo la Namatili ndipo alikuta Kibanda hicho, kilichokuwa kimejengwa kwa kuzungushia Fito maeneo ya Pembeni bila ya kukandikwa kwa udogo, aliamua kuingia na kujilaza.


Michael aliendelea kuseama kuwa,  kaka yake akiwa kwenye usingizi  Simba wawili waliokuwa kwenye mawindo yao, waalikuwa wakikimbiza Mbwa waliokuwa maeneo ya Simba hao bila mafanikio, na walifika Kibandani hapo wakasimama na kuangalia kilicho ndani.


Alisema baada ya Simba hao kubaini ndani ya Kibanda kile kuna kitu na kukosa eneo la kupita, ndipo mmoja wa wao aliamua kupitisha mkono wake kupitia matundu ya Fito, ambapo kucha za Simba huyo zilifikia kati ya tumbo na Kifua cha Kaka yake, ambae alishtuka na kupiga kelele kuashiria kuomba msaada kutoka kwa majirani.


Michael alisema kutokana na kelele hizo Simba wale waliamua kuondoka huku wakimuacha Kizito akiendelea kuvuja Damu zilizotokana na kubanwa kucha za mnyama huyo.


Alisema wasamalia walipofika eneo la Kibanda hicho walimkuta tayari ameshajeruhiwa ambapo walimchukuwa hadi Kituo kidogo cha Polisi Kata ya Rutamba na kupatiwa Fomu namba tatu (PF3) na kumkimbiza Kituo cha Afya cha Rondo.


Hata hivyo kutokana na ukubwa wa tatizo hilo, Mganga wa Kituo hicho aliamuru apelekwe Hospitali ya Sokoine kwaajili ya matibabu.


Mmoja wa watumishi wa Hospitali hiyo, Dkt. Ernest Muhando, amesema wamempokea Majeruhi Kizito akiwa na majeraha kati ya kifua na tumboni, yaliyosababishwa na kushambuliwa na kucha za Simba.


Alisema mara baada ya kufikishwa Hospitalini hapo waliweza kumuanzishia Matibabu kwa haraka na kwamba sasa hali yake inaendelea vizuri.


BAGAMOYO KWANZA BLOG ilimtafuta Afisa Mali asili wa Wilaya ya Lindi, Victor Shau, ili kuzungumzia tukio hilo ambae amewaomba wananchi wanaoishi maeneo yanayokaribiana na Msitu wa Tarafa ya Rondo, kuchukuwa tahadhari ikiwa ni pamoja na kutotembea hovyo nyakati za usiku, kutoka Kijiji kimoja kwenda kingine ili kulinda usalama wa maisha yao.

TUCHANGAMKIE FURSA YA VIFUNGASHIO - MGALU

WANANCHI katika vijiji vinavyounda halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wametakiwa kuchangamkia fursa ya kufungiwa kwa mifuko ya plastiki, kwa kutengeneza vikapu vya asili, vitakavyochukua nafasi ya mifuko ya plastik.


Kufungiwa kwa mifuko hiyo kunakoelezwa ni hatua ya kupambana na uchafuzi wa mazingira, kunatokana na mifuko hiyo kutooza haraka iwapo ardhini, licha ya kuwa msaada kwa wananchi katika kubebea vitu mbalimbali.


Ushauri huo umetolewa na Mbunge wa viti maalum, mkoa wa Pwani, Subira Mgalu, alipozungumza na wajasiriamali katika vijiji vilivyopo Kata za Talawanda na Kiwangwa, ambao wamekopeshwa fedha za asilimia zilizotolewa na halmashauri ya Chalinze, wilayani hapa.


Alisema kwamba serikali iliyopo madarakani kupitia wizara husika ya mazingira, imefanya utafiti wa kina hivyo kubaini uwepo wa uchafuzi wa mazingira, na kufika hatua ya kufungia mifuko hiyo, inayolenga kupambana na hali hiyo.


"Tuchangamkie fursa ya kutengeneza vikapu vyetu vya asili, ukiangalia kwa haraka unaweza kusema kufungiwa kwa mifuko kutatuathiri katika uchukuzi, hii imeturejeshea fursa ya kibiashara ya kutengeneza vikapu, ambavyo wazee wetu walikuwa wanavitengeneza," alisema Mgalu.


"Miyaa, ukindu na rangi vyote tunavyo, kilichobaki sasa ni kuitumia fursa hii kutengeneza vikapu kwa wingi, kisha tuvipeleke katika maeneo mbalimbali ninaimani kubwa kwamba hatua hii imeleta neema kwetu," alisema.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Said Zikatimu alisema kwamba, wanaendelea na ukopeshaji wa vikundi vya ujasiriamali, ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali kuvikopesha vikundi mikopo isiyokuwa na riba.


"Katika halmashauri yetu fedha sio tatizo, tunazo za kutosha, tunachokiomba kutoka kwenu ni kuanziasha vikundi, kuvisajili kisha kuwasilisha kwenye ofisi ya Maendeleo ya Jamii ili muweze kunufaika na mikopo hiyo isiyo na riba," alisema Zikatimu.

KIZIMBANI KWA KUBAKA MTOTO CHINI YA MIAKA 10.

NA HADIJA HASSAN, LINDI.

MKULIMA wa Kijiji na Kata ya Rutamba, Halmashauri ya Wilaya Lindi Mkoa wa Lindi, Issa Seif Puyaye (51) amefikishwa mahakamani akikabiliwa na Shitaka la kubaka Mtoto mwenye umri chini ya miaka kumi (Jina linahifadhiwa).


Puyaye amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Lindi na kusomewa Shitaka lake mbele ya Hakimu Faudhia Jemedari, na mwanasheria wa Serikali Godfrey Mramba. 


Akimsomea Shitaka lake, Mramba alidai kuwa Aprili 14 mwaka huu, Mshitakiwa alikamatwa na askari wa Jeshi la Polisi, kufuatia wazazi wa Mtoto huyo kutoa taarifa kwenye chombo hicho. 


Mramba alidai Mahakamani hapo kuwa wazazi wa Mtoto huyo anayesoma Darasa la Pili katika Shule ya Msingi Mpilipili iliyopo Manispaa ya Lindi,walichukuwa uwamuzi huo baada ya kupewa taarifa na walipomkagua waliweza kubaini kufanyiwa kitendo hicho cha kinyama. 


Alidai kwamba kutokana na kitendo hicho mshitakiwa amefanya kosa kwa mujibu wa kifungu 130 (1) (2) (e) na 131 (1) Sheria na kanuni ya adhabu ya makosa sura ya 16/2002. 


Mwanasheria huyo aliiambia Mahakama hiyo kwamba mshiatkiwa alipata nafasi ya kumfanyia unyama huo, kutokana na Mtoto huyo kwenda likizo kwa ndugu zake wengine. 


Hata hivyo mshitakiwa amekana kosa na kesi hiyo namba 34/2019, imepangwa kusikilizwa tena Mahakamani hapo Mei 13 mwaka huu, na mshitakiwa amepelekwa rumande baada ya kukosa wadhamni.