Wednesday, February 27, 2019

MAJALIWA AKABIDHI JENERETA KITUO CHA AFYA MKOWE WILAYANI LUANGWA.

NA HADIJA HASSAN, LINDI.

Waziri Mkuu kasimu Majaliwa Akabidhi Jeneleta katika Kituo cha afya Mkowe kilichopo  katika kata ya Mkowe Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi litakalosaidi kufua Umeme wa Dharua kituoni hapo

Akizungumza na wananchi pamoja na wauguzi kituoni hapo  kwa Niaba ya Waziri Mkuu  Kasimu Majaliwa , wakati wa ghafla ya makabidhiano hayo Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Alisema amefurahishwa na maboresho yaliyofanyika katika kituo hiko kwa kuweza kufanya Upasuaji kwa akinamama Wajawazito. 

Alisema hali  hiyo inaonyesha  ni kwa namna gani dhamira ya uwekezaji huo umeweza kuleta tija katika kituo hicho.

Hata hivyo pamoja na mambo mengine Mgalu alilitaka shirika la Umeme (TANESCO) Mkoa wa Lindi kuendelea na uboreshaji wa upatikanaji wa umeme katika mkoa huo.

Awali akitoa taarifa ya kituo Mganga Mfawidhi wa  Kituo hicho Paulo Mbinga alisema kuwa kituo cha  Afya Mkowe ni miongoni mwa vituo vya Afya vilivyonufaika na mpango wa Serikali wa kuimarisha Miundombinu ya vituo vya Afya Nchini unaolenga kuviwezesha vituo vya Afya  kutoa huduma za Dharula kwa akina Mama Wajawazito   

Alisema Kituo hicho kwa sasa kinahudumia jumala ya Wananchi 5,224 wa Kata ya Mkowe pamoja na zile za jirani kama Chienjele, Nandagala, Likunja,Namalolo na  Mnacho ambapo jumla ya wagonjwa 74 hufika Kituoni hapo kwa siku kwa ajili ya kupatiwa Matibabu.

Mbinga aliongeza kuwa  kituo hicho kilipoanzishwa kilikuwa kinatoa huduma za nje OPD,  kulaza wagonjwa, kliniki kwa akina Mama wajawazito na Watoto, huduma za Uzazi wa Mpango pamoja na kujifungua akina Mama

Alisema kutokana na maboresho yaliyofanyika  hivi karibuni  kituo hicho kwa sasa kimeongeza  Huduma  za Damu salama, pamoja na Upasuaji kwa akina Mama  wajawazito.

Aidha, DKT Mbinga  alimshukuru Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa ambae pia ni Mbunge wa Jimbo hilo la Ruangwa kwa kuwasaidia jenereta katika Kituo hicho ambalo kwa kiasi kikubwa  litasaidia utoaji wa Huduma  kwa Wagonjwa Pindi umeme utakapokatika.

Hata hivyo DKT Mbinga alisema kuwa pamoja na kusaidia utowaji wa huduma pia jenereta hiyo litasaidia kuimarisha usalama wa Huduma za upasuaji katika Kituo


AFISA UTUMISHI MKURANGA AONYWA KUTUMIA CHEO CHAKE VIBAYA.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza uadilifu kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, wakati wa kikao kazi na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
............................


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amemuonya Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Bw. Valintine Mbai ambaye ni Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa Halmashauri hiyo kuacha tabia mbaya  ya kutumia cheo chake kuomba rushwa ya ngono kwa Watendaji wa Vijiji katika Halmashauri hiyo na kumtaka afisa huyo kubadili mwenendo wake haraka iwezekanavyo.


Onyo hilo amelitoa wilayani Mkuranga, wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kabla ya kuanza kutembelea wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri hiyo ili kujiridhisha na utekelezaji wake.


Akizungumza na watumishi hao, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, ni aibu kwa afisa huyo mwenye dhamana ya kusimamia maadili ya kiutumishi kutumia madaraka yake vibaya kwa kuomba rushwa ya ngono toka kwa Watendaji wa Vijiji jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya kiutendaji katika utumishi wa umma.


Amemtaka afisa huyo kuacha tabia hiyo na kujirekebisha maramoja ili awe mfano bora kwa watumishi anaowasimamia kimaadili.


Pi amemtaka, afisa huyo kuwa na heshima kwa wakuu wake wa kazi akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ili kutengeneza mazingira mazuri ya kiutendaji.


Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa ametoa angalizo kwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Juma Abeid kutowatetea watumishi wasio waadilifu na badala yake awachukulie hatua za kinidhamu hata kama ni marafiki zake.


Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ameendelea kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma nchini akiwa wilayani Mkuranga na kutoa wito kwa watumishi wote wa umma kuhakikisha wazingatia Kanuni za Maadili ya Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza hoja mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, wakati wa kikao kazi na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji


TUMIENI UMEME WA REA KUONGEZA UFAULU SHUELNI- SUBIRA MGALU.

Image may contain: Subira Mgalu, standing and outdoor
NA HADIJA HASSAN, LINDI

Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu amezitaka Shule Zote Nchini zinazowekewa miundo mbinu ya Umeme kupitia mradi wa umeme Vijijini (REA) , kuutumia umeme huo  kuongeza ufaulu katika Shule zao.

Mgalu ameyasema hayo jana alipokuwa anazungumza na baadhi ya wanafunzi na walimu katika shule ya Sekondari Mnacho kijiji cha Luchelegwa Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi wakati wa hafla fupi ya kuwasha umeme katika shule hiyo.

Mgalu amesema ili umeme huo uweze kuleta tija ni wajibu kwa walimu kuongeza kasi ya kufundisha  na wanafunzi kujisomea kwa kutumia muda wa ziada hata nyakati za jioni

“Serikali inapoamua kufanya maboresho katika maeneo haya ina nia ya makusudi ya kutaka kuona mabadiliko maana sasa hamtakuwa na kisingizio tena cha kufanya vibaya ” alisema Mgalu.

Pamoja na mambo mengine Mgalu alitumia fursa hiyo kuwaasa  wanafunzi wa shule hiyo  kusoma kwa bidii ili kupata matokeo mazuri , pamoja na kuwataka wanafunzi wa kike kuepuka vishawishi kwa vijana wa kiume

“Nawaomba msome watoto wangu hasa watoto wa kike, mshika mawili moja humponyoka ni aibu sana tukionekana mikoa ya kusini na ukanda huu kwamba sisi wanafunzi wetu wengi wanafeli kwa sababu ya kupata ujauzito wakati tupo sisi wenzenu wa mfano tumetoka kusini na tulivumilia hizo mimba tulikuja kuzipata baadae baada ya kuanza maisha yetu” alisema Mgalu

kwa upande wake mkuu wa Shule hiyo David Mwakalobo alisema kuwa kabla ya kuwekwa kwa umeme huo shule hiyo ilikuwa inatumia umeme wa jua ambao ulikuwa haukidhi mahitaji kwani walikuwa walikuwa wanalazimika kutumia kompyuta tano tu kati ya ishirini walizonazo wakati wa kufundishia  kutokana na uwezo mdogo wa nishati iliyokuwa inatumika

Mwakalobo Alisema umeme huo Licha ya kuutumia katika masomo hayo ya kompyuta pia wanatarajia kununua shajala itakayoweza kudurufu Mitihani  hali ambayo itawarahisishia Wanafunzi kutotumia muda mwingi kuandika Mtihani kwenye Makaratasi pamoja na Walimu kuweka  kwa usiri wa mitihani hiyo huku ikiwarahisishia Walimu kutoandika kwa chaki ubaoni wakati wa Mitihani hiyo.

Aliongeza kuwa wanaishukuru Serikali kwa kuwawekea umeme katika shule yao kwani utaweza kuongeza kiwango cha ufaulu kwa kuongeza ubunifu wa ufundishaji kwa walimu

Kufuatia hatua hiyo ya kuwasha umeme katiaka Shule ya Sekondari Mnacho Mkandarasi anaetekeleza mradi huo wa kusambaza umeme vijijini (REA) STATE GRID amehaidi kuweka mfumo wa umeme katika shule hiyo.

MAGAZETI YA LEO FEBRUARY 27, 2019.

Tuesday, February 26, 2019

CUF YA MAALIM SEIF YAOMBA HUKUMU ZISOMWE...WASEMA KESI ZINAWACHOSHA




Mbunge wa malindi Mhe Ally Saleh Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wabunge wa chama hicho, Magomeni jijini Dar es Salaamna, KULIA ni mbunge wa jimbo la mchinga Mhe Hamidu Bobali. wameiomba mahakama kutolea huku shauri lao.
 Na Selemani Magali
"Kwa heshima na taadhima tunamuomba Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi waliangalie suala hili kwa umuhimu na uzito maalumu kwa sababu kuchelewa kwake kunakiathiri chama chetu kwa kiasi kikubwa," ni Kauli ya  Mbunge wa Malindi Bw. Ally Saleh wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuiomba Mahakama kutoa hukumu ya shauri lao namba 23/2016 linalohusu uhalali wa uenyekiti wa Profesa Ibrahim Lipumba kwa chama CUF.
Ally amesema kuna athari kubwa wanazipata toka kesi hiyo kufikishwa mahakamani na kwamba waathirika wakubwa ni wabunge lakini pia inawagharimu rasilimali fedha, muda na kuibiwa ruzuku zaidi ya Sh1.5 bilioni na uharibifu wa mali za chama zikiwamo magari na majengo. .
"Chama kinashindwa kuendesha shughuli kwa utulivu na kujiandaa na chaguzi za ndani na za kiserikali kwa mwaka huu 2019 na uchaguzi mkuu 2020" amesema Saleh.
Naye Bobali amesema athari anazopata ni kubwa ikiwamo kutofanya siasa kwa kipindi chote tangu mgogoro huo ulipoanza.
Bobali ambaye pia ni mwenyekiti wa vijana wa chama hicho amesema mgogoro huo unawatoa kwenye ushindani wa kisiasa kwa sababu unawaweka mbali na wanachama wao na majimbo yao kwa ujumla.
"Tunashindwa kufanya siasa, kwa sababu baadhi ya maeneo wenyeviti wa chama kwa eneo husika wanakuwa upande wa Lipumba na sisi tupo upande halali wa Maalim Seif, huu mkanganyiko unatusukuma kuiomba mahakama kutoa hukumu ya kesi hiyo ili tuendelee na majukumu yetu angalau kwa kipindi hiki kifupi kabla ya uchaguzi mkuu 2020," amelalama Bobali.
Februari 22, 2019 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilisogeza mbele utoaji  hukumu ya mgogoro wa uongozi ndani ya CUF na sasa hukumu hiyo itatolewa Machi 17, 2019.