Tuesday, February 19, 2019

TAMPRO SACCOS YAKABIDHI MADARASA MAWILI KIBAHA VIJIJINI.

 Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini Hamood Abuu Jumaa (katikati) mara baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa madarasa mawili katika kijiji cha Mwembengozi ambayo yamejengwa kwa msaada wa TAMPRO SACCOS ya jijini Dar es Salaam, wanaoshuhudia, wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa TAMPRO SACCOS, Shabani Yasini na kushoto ni Meneja wa TAMPRO SACCOS, Saidi Ngolola.
..................................

Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo kilicho chini ya Jumuiya ya wataalamu wa kiislamu Tanzania, (TAMPRO SACCOS) kimekabidhi madarasa mawili yenye thamani ya shilingi milioni 26 katika kijiji cha Mwembengozi kilichopo kata ya Dutumi Halmashauri ya Kibaha vijijini wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyekiti wa TAMPRO SACCOS, Shabani Yasini amesema ujenzi huo wa madarasa umefanikiwa kwa kushirikiana wanachama wa TAMPRO SACCOS pamoja na wadau wengine ili kuwapunguzia watoto wa kijiji hicho kutembea umbali mrefu kufuata shule.

Alisema wazo la kujenga madarasa hayo ni kutokana na kilio cha muda mrefu kutoka kwa wananchi wa kijiji hicho ambapo shule iliyopo ipo mbali na eneo hilo hali inayopelekea watoto kutembea umbali mrefu kufuata shule.

Aliongeza kwa kusem akuwa, kukamilika kwa ujenzi wa vyumba hivyo viwili kumetokana na ushirikiano kwa wanachama wa TAMPRO SACCOS na wadau wengine mbalimbali.

Alisema ujenzi huo ulianza tarehe 20/11/2018 na kukamilika tarehe 08/02/2019 ambapo mpaka kukamilika madarasa mawili zimetumika shilingi milioni 26.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya tukio la kukabidhi madarasa, Meneja wa TAMPRO SACCOS, Saidi Ngolola amesema hadi sasa TAMPRO SACCOS ina jumla ya wanachama 1800 ambao kati yao wanaume ni 1100 na wanawake ni 700.

Alisema chama kimetoa uhuru kwa wanachama kutoa mawazo yao ili kukiimarisha huku wanachama ndio wafanyaji wa maamuzi katika mambo mbalimbali yanayohitaji kutekelezwa.

Akielezea swala la mikopo kwa wanachama Ngolola alisema chama kina uwezo wa kutoa milioni 60 kila mwezi ambapo mwanachama anatakiwa kurejesha kidogo kidogo bila riba.

Aidha, alisisitiza kuwa, chama hicho Ushirika wa Akiba na Mikopo kinafuata sheria za uislamu katika miamala ya kifedha hivyo kuna mikopo ya aina mbili tu ambayo ni pesa taslimu (mkopo mwema) na pili kukopesha bidhaa (murabaha).

Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini Hamood Abuu Jumaa, aliwataka wananchi wa kijiji cha Mwembengozi kutoa ushirikiano kwa TAMPRO SACCOS ili wapate moyo wa kundelea kuisadia jamii ya kijiji hicho.

Aidha, alitumia nafasi hiyo kuishukuru TAMPRO SACCOS kwa msaada huo wa madarasa mawili ambao ni mkombozi kwa wananchi wa kijiji cha Mwembengozi.

Mbune huyo alimtaka Afisa elimu wa Halmashauri ya Kibaha vijijini kushughulikia swala la usajili wa shule hiyo ambayo mpaka sasa tayari ina madarasa mane ili watoto wapate elimu katika shule hiyo.
  Mwenyekiti wa TAMPRO SACCOS, Shabani Yasini  (kushoto) akimkabidhi Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini, Hamood Abuu Jumaa, funguo za madarasa mawili katika kijiji cha Mwembengozi, anaeshuhudia ni Diwani wa kata ya Dutumi, Mkali Saidi.
 
 Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini, Hamood Abuu Jumaa, akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madarasa mawili yaliyojengwa kwa msaada wa TAMPRO SACCOS ya jijini Dar es Salaam katika kijiji cha Mwembengozi kata ya Dutumi Halmashauri ya Kibaha vijijini Wialaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani.

 
 Meneja wa TAMPRO SACCOS, Saidi Ngolola akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi madarasa mawili yaliyojengwa na
TAMPRO SACCOS ya jijini Dar es Salaam.
    Wananchi wa kijiji cha Mwembengozi kata ya Dutumi Halmashauri ya Kibaha vijijini Wialaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, wakishuhudia makabidhiano ya madarasa mawili yaliyojengwa kijijini hapo na TAMPRO SACCOS ya jijini Dar es Salaam.
 
 Muonekano wa jengo la madarasa mawili yaliyojengwa kijijini hapo na TAMPRO SACCOS ya jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wanachama wa TAMPRO SACCOS wakiwa katika hafla ya kukabidhi madarasa mawili katika kijiji cha Mwembengozi kata ya Dutumi Halmashauri ya Kibaha vijijini Wialaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, wakishuhudia makabidhiano ya madarasa mawili yaliyojengwa kijijini hapo.

CCM YABOMOA NGOME YA CUF RUFIJI.

Na Shushu  Joel,Ikwiriri.
..................................
CHAMA cha mapinduzi (Ccm) wilaya ya  Rufiji  mkoani Pwani kimefanikiwa kuibomoa ngome  ya upinzani katika wilaya hiyo  ilikuwa imeota mizizi.

Akizungumza na viongozi wa  matawi wote wa wilaya hiyo katibu wa chama  hicho Mtua alisema kuwa chama cha cuf  kilikuwa na ngome kubwa  katika wilaya hii  lakini tangu  wannachi  hao waone  utekelezaji wa Ilani ya Ccm chini  ya  mwenyekiti  wa Taifa ambaye pia ni Rais  wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ambaye amekuwa mstali wa mbele katika uletaji wa maendeleo kwa wananchi.

Alisema kuwa awali watu  walishindwa kujiunga na Ccm kutokana na ahadi nyingi kutokamilika kwa wakati lakini kipindi hiki  yote yamefanywa na yanaendelea kufanyika.

"Rufiji ilikuwa ni ngome kuu ya chama cha upinzani cha Cuf lakini kwa  muda  wa miezi michache nilianza kazi hapa kama Katibu nimefanikiwa kuvuna wanachama zaidi ya 1000 hivyo inaonyesha ni jinsi gani ngome hiyo inavyoputikika" Alisema Mtua.

Aidha  aliongeza  kuwa bado  kunanafasi za kutosha kwa wale wanaohitaji kujiunga na Ccm kwani ni chama pekee chenye kuwajali  wananchi pasipo  ubaguzi wa kabila kama ilivyo kwa vyama vingine.

Kwa upande  wake diwani wa kata ya Ikwiriri Ally Ndungutu ambaye awali alikuwa ni diwani kupitia Cuf lakini amejiunga Ccm alisema kuwa kuna kundi zaidi ya elfu 10 wanakuja kujiunga na Ccm sema  tu wanasita sita  lakini watakuja.

Aliongeza kuwa alipokuwa  Cuf kuna  vitu vingi  alikuwa havipati kutokana chama hicho kutokuwa  na vikao vya ushauri na mwelekeo wa maendeleo kwa Taifa.

Hivyo amewataka watanzania  wote nchini kujitathimini kwa yale wanayotendewa  na Rais wa awamu ya tano.

Naye Mwanahasi Geruka mkazi wa Ikwiriri amempongeza katibu wa ccm wilaya hiyo  kwa juhudi zake anazozifanya za uvunjaji wa ngome  ya upinzani  katika wilaya hiyo.

RC NDIKILO ATOA MWEZI MMOJA KIBITI KUANZA MARA MOJA UJENZI WA HOSPITAL YA WILAYA

NA MWAMVUA MWINYI, KIBITI 

MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo ametoa muda wa mwezi mmoja kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Kibiti na mkuu wa wilaya hiyo kuhakikisha ujenzi wa hospital ya wilaya unaanza mara moja.

Amesema haiwezekani fedha kiasi cha sh. bilioni 1.5 zipo, pamoja na eneo lakini cha kushangaza eneo limeachwa badala ya kuanza utekelezaji. 

Akitoa maelekezo hayo wakati alipokwenda kutembelea eneo la ujenzi huo huko Mtawanya, Ndikilo alisisitiza wajipange na kuanza ujenzi mara moja. 

Alisema, baada ya mwezi mmoja atakwenda kuangalia kama maagizo aliyotoa yamefanyiwa kazi. 

“Eneo mnalo haiwezekani liwe jeupe namna hii, pesa ipo nataka watu waingie kazini, “

“Halmashauri ya Kibaha Mjini na Vijijini wameshaanza ujenzi na wanaendelea vizuri, mkurugenzi hapa, Dc kimya, najua ni wachapa kazi, fanyeni vitendo kama tulivyozoea kuwaona “alisisitiza Ndikilo.
 
Hata hivyo ,Ndikilo alifafanua mkoa umepokea bilioni 4.5 kwa ajili ya hospital hizo tatu. 

Alielezea kwamba mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa uzalishaji umeme stigler’s gorge (Stigo)  atatumia barabara ya Kibiti -Mloka hivyo idadi kubwa itatumia hospital hiyo, ambapo itakuwa mkombozi kwa wananchi walio wengi. 

Pia aliipongeza halmashauri ya wilaya ya Kibiti ,kwa kuanza ujenzi wa ofisi ili kumuondolea kero mkurugenzi ya kupangisha kwenye  ofisi za watu binafsi kwa ajili ya watumishi wa halmashauri ambao hurundikana kwenye ofisi hizo. 

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibiti, Alvera Ndabagoye alisema wamejipanga kuanza ujenzi wa hospital ya wilaya. 

Mkuu wa wilaya ya Kibiti, Gulam Kifu alibainisha wamepokea maelekezo waliyopatiwa na mkuu wa mkoa huyo na ameahidi kuyafanyia kazi.

CHALINZE YAPITISHA BAJETI YA BILIONI 50.6 MWAKA 2019/2020.

Image may contain: 2 people, people sitting, screen and indoor
Baraza la Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze limekaa na kupitisha bajeti ya Mapato na matumizi ya jumla ya Fedha za kitanzania bilioni 50.6 kwa mwaka wa Fedha 2019/2020.Mapendekezo ya bajeti hiyo yamefanyika katika kikao maalumu cha baraza hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa shule ya Sekondari ya Lugoba jana.


Akiwasilisha bajeti hiyo Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Bwana Shabani Millao alitoa ufafanuzi wa bajeti na kueleza mawanda ya bajeti(scopes of budget)hiyo kuwa,Mapato ya ndani bilioni 6.1,michango ya Jamii bilioni 1.8,ada za shule za Sekondari milioni 84.6,mishahara bilioni 31.7,miradi ya maendeleo serikali kuu bilioni 5.8,ruzuku ya matumizi ya kawaida bilioni 3.9,wahisani bilioni 1.2.


Hivyo kutokana na ufafanuzi huo bajeti ya halmashauri ya Wilaya ya Chalinze inakuwa na bajeti yenye jumla ya Fedha za kitanzania bilioni 50.6.


Katika mapendekezo ya bajeti baraza la Madiwani lilipitia kwa kina kamati kwa kamati na kuona vipaumbele ambavyo vinatatua kero za wananchi kama huduma za afya,elimu Maji na usafi wa mazingira na wajumbe walishauri baadhi miradi iondolewe kwa sasa ili huduma za Jamii zitolewe moja kwa moja,katika mabadiliko ya miradi waliyopendekeza wajumbe ni kuondoa mradi wa ujenzi wa nyumba za wakuu wa idara na kukamilisha vituo vya afya ,zahanati na vyumba vya madarasa ambavyo ni kipaumbele kwa sasa.





Naye Diwani wa viti maalum CCM Maria Moreto aliwaomba Madiwani kumuunga mkono hoja ya kuondoa mradi wa ujenzi wa nyumba za wakuu wa idara kwa sasa ili kukamilisha miradi ya wananchi na wananchi waanze kupata huduma, mradi wa ujenzi wa nyumba za wakuu wa idara ufanyike bajeti ijayo.




Mwenyekiti Wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mhe Saidi Zikatimu alitoa mchango wake wa mawazo kwa kueleza umuhimu wa miradi katika halmashauri na kuwataka wajumbe kuamua kwa kuzingatia miongozo ya bajeti na si vinginevyo kwani tunapanga bajeti kwa miongozo iliyotolewa na serikali.


Kwa upande wake Diwani wa kata ya Miono ambaye pia ni makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mheshimwa Juma Mpwimbwi aliwapongeza wataalamu kwa maandalizi mazuri ya bajeti na kwa ufafanuzi mzuri wa mawanda ya bajeti Iliyofafanuliwa na Kaimu Mkurugenzi, "Ni bajeti inayogusa Maisha ya wananchi na inayotatua kero za wananchi katika halmashauri yetu,bajeti hii itatekelezeka kama tutakusanya Mapato yetu kwa umakini na kufikia malengo tuliyojiwekea." Mpwimbwi alisema.


Naye Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Bwana Shabani Millao aliwashukuru wajumbe wa baraza la Madiwani kwa kupitia kwa kina bajeti pendekezwa na kueleza kuwa bajeti hii imeandaliwa kwa kuzingatia miongozo ya serikali na kila kinachosomeka ni kipaumbele kwani mwongozo ndiyo uliotumika katika kuandaa kazi hii. "Ushauri mlioutoa ni wa kujenga na pale itakapowezekana kulingana na ukomo wa bajeti tutatekeleza na ikishindikana kwa mwaka huu tutatekeleza kwa bajeti ijayo“ Millao alisema.



Hata hivyo baada ya mjadala wa muda mrefu kwa pamoja Madiwani waliridhia kupitisha bajeti ya halmashauri yenye thamani ya Fedha za kitanzania bilioni 50.6.

Monday, February 18, 2019

MAHAKAMA KUU YAFUTA BODI ZA WADHAMINI ZA CUF

Mahakama Kuu Nchini Tanzania  imetoa uamuzi wa kuzifuta bodi za wadhamini za pande mbili zinazovutana katika chama cha CUF, kati ya upande wa Mwenyekiti wa chama hicho Ibrahim Lipumba na mwingine wa Katibu Mkuu Maalim Seif.

Wakati huohuo Mahakama ya rufani jijini  Dar es Salaam Tanzania imeomba muda zaidi wa kusikiliza hoja za pande mbili kuhusiana na kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama  cha upinzani cha CHADEMA Freeman Mbowe na mbunge wa jimbo la Tarime mjini , juu ya ikiwa kesi yao inastahili kuendeshwa katika mahakama kuu au mahakama ya rufani.