Sunday, February 10, 2019

WAKULIMA WA MPUNGA JICA BAGAMOYO WALIA NA MKANDARASI

Image may contain: 6 people, people smiling, people standing, sky, cloud and outdoor
Wakulima wa mpunga wapatao 28 wanachama wa skimu ya Umwagiliaji BIDP maarufu kama Skimu ya Jitegemee iliyopo Kata ya Magomeni Wilayani Bagamoyo, wamemlalamikia Mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa barabara na mifereji ya maji katika skimu hiyo kwa kuwatia hasara kwa kusua sua kwa utekelezaji wa mradi huo.


Mkandarasi huyo toka kampuni ya musons engineers alianza kutekeleza mradi huo Mwezi April 2018 na alitarajiwa kukamilisha mradi mwishoni mwa Mwezi Novemba, 2018 lakini hadi sasa hajakamilisha mradi huo na anaendelea kuutekeleza akiwa katika kipindi cha adhabu ambacho pia kinakwisha ifikapo tarehe 18 Februari, 2019.


Wakulima hao 28, waliwasilisha malalamiko yao kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Waheshimiwa madiwani ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Hapsa Kilingo ambaye aliongoza wajumbe wa kamati hiyo waliofuatana na Wataalam wa Halmashauri kuutembelea na kuukagua mradi huo wa ujenzi wa mifereji na barabara katika Skimu ya Umwagiliaji ya Tegemeo mapema jana.


Akizungumza kwa niaba ya wakulima wenzake wa skimu ya Tegemeo, mmoja wa wakulima (jina limehifadhiwa) anayefanya shughuli zake za kilimo katika Skimu hiyo kwenye kitalu GH amesema, yeye na wakulima wenzake wa kitalu GH ndio wahanga wakubwa zaidi, kwani tangu msimu wa pili wa kilimo uanze hawajafanikiwa kabisa kupata maji katika mashamba yao, kutokana na mkandarasi kushindwa kukamilisha mradi kwa wakati, hususani ujenzi wa mifereji ya kupeleka maji katika kitalu hicho, hali iliyopelekea wakulima 28 wa kitalu GH kupata hasara kubwa ya kuunguliwa na mazao yao.


“Wakati wenzetu wakikaribia kuvuna mpunga katika mashamba yao, sisi hatuna kabisa matarajio hayo ya kupata chakula katika msimu huu, ni maumivu makubwa sana kwa mkulima kulima kisha akakosa mavuno kwa sababu za uzembe tu wa mkandarasi aliyeamua kufanya kazi bila kuzingatia mahitaji halisi ya wakulima lakini pia kwa kusua sua sana hivyo kupelekea mradi kutokamilika kwa wakati, niwaombe viongozi watusaidie kuhakikisha mradi huu unakamilika ili tuondokane na changamoto hizi” Anaongeza Mkulima huyo.


Nae diwani wa Kata ya Magomeni unakotekelezwa mradi huo Mhe. Mwanaharusi Jarufu akizungumza katika Ziara hiyo ameonesha kutoridhishwa na kiwango cha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa mifereji na barabara katika Skimu hiyo, na kueleza kwamba mradi umetekelezwa chini ya kiwango na ni vyema Mamlaka zinazohusika kufika katika mradi huo na kuukagua kuona kama mradi umetekelezwa katika kiwango kinachotakiwa, kwani hayuko tayari kuona fedha za Serikali zinapelekwa katika Kata anayoiongoza na kisha fedha hizo zisifanye kile kilichotarajiwa na Serikali.


Akizungumza na Wakulima hao mara baada ya kukagua mradi huo na kusikiliza kero za wakulima wa skimu hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Mhe. Kilingo amewaasa wakulima hao kuwa watulivu na wavumilivu wakati kamati yake na Ofisi ya Mkurugenzi ikiendelea kushughulikia suala lao kwa haraka kwa kufanya mazungumzo na mkandarasi ili akamilishe mradi huo mapema iwezekanavyo.


Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira jana imefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ya Sekta za Kilimo na Ufugaji ikiwa ni katika utaratibu wake wa kawaida wa kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo kila robo.
 Image may contain: 3 people, people standing, sky, outdoor and nature 
Wakulima wa mpunga wapatao 28 wanachama wa skimu ya Umwagiliaji BIDP maarufu kama Skimu ya Jitegemee iliyopo Kata ya Magomeni Wilayani Bagamoyo wakilalamikia mbele ya Madiwanai, kukosa maji kwenye mashamba yao baada ya mkandarasi anaetengeneza barabara na mifereji ya maji kuchelewa kukamilisha kazi yake.
Image may contain: 4 people, including Nuru Tamimu, people standing, outdoor and nature
 Mmoja wa wakulima hao akiwaonyesha Madiwani namna mifereji ilivyoharibika na kupelekea kukosa maji ya kumwagilia mashamba yao, hiyo ni baada ya mkandarasi aliyepewa kazi kuchelewa kukamilisha kazi yake, mwenye mtandio mweupe ni Diwani wa kata ya Magomeni Mwanaharusi Jarufu.

Image may contain: 5 people, people standing and outdoor
Image may contain: 3 people, people smiling, people standing, wedding, outdoor and nature
 kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, ya Halamashauri ya Bagamoyo wakitembelea mashamba ya mpunga ambayo yamekosa maji kutokana na Mkandarasi kuharibu mifereji ya maji na kuchelewa kukamilisha kazi yake ya ukarabati.
Image may contain: plant, outdoor and nature 
Image may contain: sky, grass, plant, outdoor and nature 
 Muonekano wa mifereji ya maji ya kumwagilia kwenye mashamba ya mpunga kama inavyoonekana ikiwa imeharibika mara tu baada ya kutengezwa ambapo kampuni inayofanya kazi hiyo baado inaendelea na kazi huku wakulima wakilalamika kukosa maji ya kumwagilia kwenye mashamba yao.
Image may contain: 4 people, people smiling, outdoor
 Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Mwambao Shumina Rashidi, akiandika baadhi ya hoja zilizotolewa na wakulima wa mpunga katika shamba hilo wakati kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, ya Halamashauri ya Bagamoyo.
Image may contain: 2 people, people standing and outdoor 
 Mwenyekiti wa kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Hapsa  Kilingo (katikati) akimsikiliza mmoja wa wakulima akiwaonyesha mifereji ya maji ilivyoharibika hali inayopelekea wakulima kukosa maji kwenye mashamba yao, kushoto ni Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Mwambao Shumina Rashidi.
Image may contain: plant, grass, sky, outdoor and nature

 Muonekano wa shamba ambalo limekosa maji na mpunga kunyongea na Ardhi yake kupasuka kama inavyoonekana.

Thursday, February 7, 2019

AHUKUMIWA JELA MIAKA 20 KWA KUMDHALILISHA MTOTO WA MIAKA MITATU.

Na Hadija Hassan, Lindi.

Mahakama ya wilaya ya Lindi, Mkoani Lindi, imemuhukumu mkazi wa Kijiji cha Milola,‘B’ Salum Kunyuma (26) kifungo cha miaka (20) Gerezani,baada ya kupatikana na hatia ya kumdhalilisha kimapenzi Mtoto mwenye umri wa miaka mitatu Jina limehifadhiwa.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo, Franco Kiswaga, kufuatia mshitakiwa kukiri kosa aliloshitakiwa nalo bila ya kulazimishwa.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Hakimu Kiswaga alimpa mshitakiwa nafasi ya kujitetea ambapo aliiomba Mahakama hiyo isimpe adhabu kali kwa maelezo alilazimika kutenda kosa hilo,baada ya kukaa muda mrefu bila ya kukutana kimapenzi na mwanamke yeyote.

Baada ya utetezi huo,Kiswaga alimuuliza Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Godfrey Michael Mramba, kama ana kumbukumbu ya makosa ya zamani kwa Mshitakiwa na kujibu hana, lakini aliiomba mahakama kumpa adhabu kali, kwani kitendo alichokifanya ni cha kinyama dhidi ya Mtoto mdogo asiye na hatia.

Hakimu Kiswaga akitoa hukumu katika kesi hiyo namba 12/2019, kupitia vifungu vya Sheria 138 (C) kifungu cha (1) na (2) (b) kanuni ya adhabu sura ya 16,alisema hakubaliani na utetezi huo kwani wapo wanawake walio sawa na lika lake, hivyo akamuhukumu kifungo cha miaka (20) Gerezani.

“Sikubaliani na huo utetezi kwani wanawake walio na umri wako na zaidi yao wapo wengi,hivyo Mahakama inakuhukumu kwenda Jela miaka (20)”.

Awali ilidaiwa Mahakamani hapo na Mwanasheria wa Serikali, Mramba aliiambia Mahakama hiyo kwamba Januari 28 mwaka huu,Mshitakiwa akijua anachokifanya ni kosa,alikutwa amempaka Mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitatu,kasha kuchukuwa uume wake na kuuchuwa Mapajani mwa Mtoto huyo.

Aidha,Mwanasheria huyo alieleza kuwa Mshitakiwa alipata mwanya wa kufanya kosa hilo kufuatia mama wa Mtoto huyo,jina limehifadhiwa kumuomba kijana huyo kumuangalizia mtoto  wake wake ,wakati yeye akiwa ameenda Bombani kuteka Maji kwa ajili ya Matumizi ya Nyumbani.

Mwanasheria huyo aliiambia Mahakama hiyo kwamba mshitakiwa baada ya kukutwa amempakata huku akiendelea kujichua juu ya mapaja ya Mtoto wake aliomba msaada wa majirani,na walipofika walimkuta Mtoto yule akiwa na mbegu za kiume zilizotokana na mwili wa Kunyumu.

PWANI YAPOKEA BILIONI 4.5 KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITAL TATU ZA WILAYA -RC NDIKILO

NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA

KATIKA  kukabiliana na changamoto ya utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi,  serikali ya awamu ya tano inajenga hospitali za wilaya tatu za kisasa , halmashauri ya Kibaha Mjini, Kibaha Vijijini na Kibiti mkoani Pwani ambazo zitagharimu kiasi cha sh. bilioni 4.5.


Akizungumza wakati alipotembelea ujenzi wa hospital ya halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Lulanzi kata ya Pichandege, kwenye ziara yake inayoendelea kukagua miradi ya maendeleo, mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo alisema kukamilika kwa hospital hizo, kutaondoa kero ya kutembea umbali mrefu kufuata matibabu.


“Kila hospital inatarajiwa kugharimu bilioni 1.5 ,matarajio yetu ni kuona ujenzi unakamilika na sio kuanza mradi na kisha kusuasua “alieleza Ndikilo.


Aidha ameelezea, fedha zote zinazoelekezwa katika miradi hiyo muhimu zitumike kwa wakati na kwa matumizi lengwa bila kuziacha kubaki viporo.


Hata hivyo Ndikilo, aliwaasa wahandisi wa halmashauri ya Kibaha Mji na wa serikali ya mkoa huo kujiwekea utaratibu wa kutoka maofisi kwenda kutembelea miradi pasipo kusubiria ziara ama kiongozi kutembelea ndipo nao watoke maofisini.


Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama alitoa rai kwa jamii kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu na kujitolea kwenye miradi ya kimaendeleo.


Diwani wa kata ya Picha ya ndege Robert Machumbe alieleza,  nia ya serikali ni kuwaletea wananchi  mabadiliko chanya ya kimaendeleo ambapo amefafanua kwamba,  eneo hilo linalojengwa hospital lina ukubwa wa hekari 25 lipo eneo linalojengwa shule ya sekondari Lulanzi lenye ukubwa wa hekari 11.7 .

BARAZA LA ARDHI LINDI LAKOSA MWENYEKITI WA KUDUMU KWA MIAKA MITATU.

Na Hadija Hassan, Lindi

Baraza la Aridhi Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi linakabiliwa na changamoto ya kukosa Mwenyekiti wa kudumu kwa  zaidi ya miaka mitatu hali inayopelekea kuchelewa kumaliza mashauri kwa wakati

Hayo yameelezwa na kaimu mwenyekiti wa Baraza hilo Saidi  Wambili jana  alipokuwa anazungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG  wakati maazimisho ya wiki ya sheria Nchini yaliyofanyika katika viwanja vya Ilulu Manispaa ya Lindi Mkoani humo

Wambili alisema changamotokubwa inayoikabili Baraza hilo kwa sasa ni kukosekana kwa mwenyekiti wa kudumu hali inayopelekea kuchelewa kumalizika kwa baadhi ya mashauri yanayofika katika baraza hilo

“baraza la Aridhi Lindi kwa kipindi cha miaka mitatu halina mwenyekiti wa kudumu mimi ni mwenyekiti wa baraza la Aridhi la mtwara hivyo nalazimika kufanya kazi kwa maeneo yote mawili hiyo wakati mwingine namna ya kujigawa inakuwa ni vigumu  hivyo hiyo  changamoto ni kubwa na ninyeti sana”  alieleza Wambili

Aliongezakuwa licha ya baraza hilo kukosa mwenyekiti wa kudumu pia baraza hilo linakabiliwa na changamoto ya watumishi  5 kwani aliyopo kwa sasa ni mtumishi mmoja  wa kada ya ukalani pekee

Alisema hali hiyo pia inamfanya kalani huyo kufanya kazi nyingine ambazo sio za kwake kama vile kupokea na kupeleka mashauri mahakamani, kupokea Ada za mahakama pamoja na shughuli za kiutawala

Alisema ili kuwe na mgawanyo mzuri wa kazi  kwa mujibu wa ikama ya watumishi  Baraza hilo lilikuwa linahitaji watumishi 6

Wambili aliongeza Baraza hilo kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo limekuwa likipokea mashauri yasiyopungua 160 yanayohusu Rufaa, Maombi madogo  mashauri ya kutekelezakwa hukumu,