Tuesday, November 6, 2018

WABUNGE WALIOHAMIA CCM WALA KIAPO BUNGENI.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akimuapisha Mh. Julius Kalanga Laizer mbunge wa jimbo la Monduli  leo Bungeni jijini Dodoma.
..................................................

Spika wa Bunge la  Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo amewaapisha wabunge wanne ambao walishinda katika chaguzi ndogo zilizofanyika katika Majimbo ya Ukonga, Korogwe,Monduli na Liwale.

Mara Baada ya kufungua kikao cha 13 cha Bunge la 11 Spika Ndugai alianza kwa kumwita Mh Julius Kalanga Laizer wa Monduli,Mh Mwita Mwikwabe Waitara Mbunge wa Ukonga,Mh Timotheo Paul Mnzava Mbunge wa Korogwe Vijijini  na Mh Zuberi Mohamed Kuchauka amabao wote ni kutoka Chama Cha Mapinduzi.

Mara baada ya kumaliza kuwaapisha wabunge hao spika aliendelea na shughuli za bunge kama zilivyopangwa ambapo mapendekezo ya mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020 .

Pia aliomba alimtaka Mwenyekiti wa kamati ya bajeti kutoa taharifa kuhusu mapendekezo ya mipango wa Maendleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na serikali pamoja na mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Mh Spika pia alimwita Msemaji Mkuu wa kambi ya upinzani wa Wizara ya fedha na Mipango kuhusu mapendekezo ya mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na mwongozo wa kuandaa mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa fedha 2019/2020.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akimuapisha Mwita Mwikwabe Waitara mbunge wa jimbo la Ukonga  leo Bungeni jijini Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akimuapisha Mh Timotheo Paul Mnzava mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini  leo Bungeni jijini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akimuapisha Mh Zuberi Mohamed Kuchauka mbunge wa jimbo la Liwale  leo Bungeni jijini Dodoma.

Mbunge wa jimbo la Monduli Mh. Julius Laizer Kalanga akipongezwa na baadhi ya wananchi waliofika bungeni kumpongeza.

Mh Zuberi Mohamed Kuchauka mbunge wa jimbo la Liwale kushoto akiwa na wananchi kutoka Liwale waliofika kumpongeza.

Mh Timotheo Paul Mnzava mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa bungeni jijini Dodoma leo.
Mh. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mh. Mwita Mwikwabe Waitara pamoja na familia yake.


PICHA NA JOHN BUKUKU-BUNGENI JIJINI DODOMA

MBUNGE WA KIBITI AASAIDIA KIDATO CHA NNE JIMBONI KWAKE.

MBUNGE wa Jimbo la Kibiti Mkoa wa Pwani Ally Ungando, akikabidhi misaada hiyo.
...................................................... 
Na Omary Mngindo, Kibiti

MBUNGE wa Jimbo la Kibiti Mkoa wa Pwani Ally Ungando, mwishoni mwa wiki ametoa msaada wa chakula na vifaa mbalimbali vya kielimu, kwa wanafunzi wa kidato cha nne ambao wamefanya mithini yao Jumatatu.

Ungando ametoa msaada huo kwenye shule 11 zilizopo jimboni humo, akiwa kwenye ziara akiambatana na Katibu Mwenezi wilaya Suleimani Ndumbogani, 
Diwani Mteule Salale Ndomondo na viongozi mbalimbali, msaada umewafikia wanafunzi 663 uliogharimu sh. milioni 4.8.

Akizungumza katika shule hizo 11, Ungando alisema kuwa hatua hiyo ni kuwaunga mkono wanafunzi hao, katika mitihani yao iliyolenga kuwaongezea hamasa hatimae kufanya vema katika mitihani yao, na kuingia kidato cha tano msimu ujao wa elimu.

"Serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Dkt. John Magufuli imeweka kipaumbele sekta zote ikiwemo elimu, nami nimeungqna nae katika kusaidia vyakula na vifaa vya kielimu, vyote vinathamani ya sh. milioni 4.8," alisema Ungando.

Kwa upande wake Ndumbogani ameridhishwa kwa hatua hiyo, ambapo alisema inaonedha ni namna gani anavyogushwa na sekta hiyo, huku alisema chama kinaunga mkono kazi zinazoendelea kutekelezwa na mbunge wao.

"Chama kinaziona juhudi za mbunge, tunamuunga mkono katika kazi hizo tupo nyuma yake, kazi anazozifanya kila mtu anaziona kwetu kama chama zinatufariji sana," alisema Ndumbogani.

Kwa upande wake nwalimu Mkuu wa shule ya shule ya Zimbwini Telensio Leonard alisema kuwa msaada huo ni mwendelezo wa mbunge wao, huku alieleza unewafikia wakati mwaka kwani utasaidia kuongeza hamasa kwa wanafunzi.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa shule zote zizopatiwa nsaafa huo, Furaha Nyandika alisema kwamba watafanya vizuri kwenye mitihani yao, ili kuunga mkono juhudi za Ungando.

Shule zilizotembelewa ni Mtanga Delta, Kikale, Rualuke, Nyamidmisati, Wama Nakayama, Mahege, Mjawa, Msafiri Bungu, Mlanzi Mchukwi na Zimbwini Kibiti.
  
MBUNGE wa Jimbo la Kibiti Mkoa wa Pwani Ally Ungando, akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi alipotembelea shule mbalimbali katika jimbo lake.
 


 
MBUNGE wa Jimbo la Kibiti Mkoa wa Pwani Ally Ungando, akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi na viongozi mbalimbali katika jimbo lake wakati alipotembelea shule za jimboni kwake mwishoni mwa wiki iliyopita lengo likiwa ni kuwapa moyo wanafunzi wa kidato cha nne ambao wanaendelea na mtihani wao wa Taifa wa kumaliza elimu ya kidato cha nne.

Picha zote na Omary Mngindo. 

ASHIKILIWA NA POLISI MWANZA KWA KUMUUA MWANAE

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunamshikilia mwanamke mmoja aitwaye RAHEL MATALAKA, miaka 41, mkazi wa kijiji cha lugenge, kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuua mtoto wake wa kiume aitwaye MALIATABU CONSTANTINE, miaka 10, mwanafunza wa darasa la pili shule ya msingi Ikelege.

Tukio hilo la mauaji limetokea tarehe 03.11.2018 majira ya 19:00hrs usiku, hii ni baada ya mama wa marehemu kuletewa malalamiko kuwa mtoto wake alikua akiangusha na kuiba maembe kwa jirani. Ndipo mtuhumiwa alipatwa na hasira na kumpiga mtoto kwa kutumia fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake hali iliyopelekea mtoto kupoteza fahamu na baadae kufariki dunia.

Mtuhumiwa alipoona mtoto amepoteza maisha alimchukua na kumtundika juu ya mwembe kwa kutumia kipande cha khanga ili apoteze ushahidi ili baadae ionekane kuwa amejinyonga. Ndipo majirani walipoona tukio hilo walitoa taarifa kituo cha Polisi.  Aidha baada ya polisi kupata taarifa hizo tulifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.

Polisi tunaendelea na mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani. Mwili wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa  ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

Katika tukio la pili, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tumefanikiwa kukamata gari moja lililoibiwa lenye namba T.233 CDG aina ya Toyota Carina mali ya RENATUS ELIUS, mkazi wa mtaa wa Ghana, likiwa limetelekezwa kando ya barabara huko maeneo ya Kitangiri Wilayani Ilemela.

Gari hilo liliibiwa tarehe 01.11.2018, ndipo mmiliki wa gari alitoa taarifa polisi juu ya kuibiwa kwa gari lake. Polisi baada ya kupata taarifa hizo tulifanya msako mkali kwa kushirikisha vikosi vyetu vya askari wa kufuatilia wezi wa magari na Intelejensia. Ndipo tarehe 04.11.2018 majira ya mchana tulifanikiwa kulikamata gari hilo likiwa limetelekezwa kando ya barabara huko mtaa wa kitangiri huku wezi wakiwa wametoroka.

Aidha baada ya kulikamata gari hilo, tulilifanyia ukaguzi na kugundua baadhi ya vifaa vya gari hilo vimetolewa ambavyo ni betrii ya gari moja, tairi  ya gari moja, jeki moja, radio ya gari, power window na show ya mbele ya gari. Polisi tunaendelea na msako mkali wa kuhakikisha wezi hao wanapatikana.

Katika tukio la tatu, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunamshikilia mwanamke mmoja aitwaye MALAGALITA MATHIAS, miaka 55, mkazi wa kijiji cha Nyatukala, kwa kosa la kupatikana na pombe ya moshi (gongo) kiasi cha lita 20 na dawa za kulevya aina ya mirungi kiasi cha kilo moja, huko maene ya kijiji cha Nyatukala Wilayani Sengerema.

Tukio hilo limetokea tarehe 05/11/2018 majira ya 17:00hrs jioni, hii ni baada ya kupatikana kwa taarifa kwamba katika Vijiji vya Nyamizeze na Nyatukala vilivyopo Wilayani Sengerema wapo watu wanaojihusisha na uuzaji pamoja na utengenezaji wa pombe ya gongo na dawa za kulevya aina ya mirungi.

Aidha baada ya kupatikana kwa taarifa hizo Polisi tulifanya msako mkali katika vijiji hivyo na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa tajwa hapo juu akiwa na kiasi hicho cha pombe ya moshi na mirungi huku wenzake wakifanikiwa kutoroka.

Polisi tunaendelea na mahojiano na mtuhumiwa ili kuweza kubaini wenzake anaoshirikiana nao katika biashara hiyo haramu ya gongo na mirungu, pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Katika tukio la nne, mtoto mmoja wa kike anayekadiriwa kuwa na umri wa siku 2 hadi 3 ameokotwa akiwa hai baada ya kutupwa kichakani kandokando mwa ziwa Victoria na mtu asiyefahamika, huko maeneo ya Bwiru ziwani Wilayani Ilemela.

Tukio hilo limetokea tarehe 01.11.2018 majira ya 14:00hrs, hii ni baada ya watu waliokua wakipita njiani kusikia sauti ya mtoto akilia toka kichakani ndipo walifuatilia na walipoona ni mtoto walitoa taatifa polisi.

Polisi tulifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kukuta mtoto wa kike akiwa ametupwa kichakani hapo akiwa hai huku mwiliwake ukiwa umeviringishwa kwenye mfuko wa sandarusi.

Mtoto amepata matibabu na hali yake inaendelea vizuri amekabidhiwa katika shirika la Forever Angel lililopo Bwiru Wilayani  Ilemela kwa ajili ya hifadhi. Polisi tunaendelea na upelelezi pamoja na msako mkali wa kumtafuta mama wa mtoto huyo.

Katika tukio la tano; Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunamshikilia tapeli/mwizi mmoja aliyefahamika kwa jina la BENEDICTO BAHATI, miaka 29, mkazi wa kiloleli, kwa tuhuma za kujifanya afisa wa TCRA, kitendo ambacho ni kosa la jinai.

Tukio hilo limetokea tarehe 02.11.2018, majira ya 16:30hrs, hii ni baada ya mtuhumiwa kwenda kwa mtumishi wa benki ya CRDB tawi la Nyegezi -Malimbe na kumtapeli kuwa yeye ni afisa wa TCRA Mkoa wa Mwanza, hivyo amefika hapo akidai anazo taarifa zake ambazo zinaonesha amekuwa akifanya mawasiliano yasiyo rasmi.

Hivyo ametumwa na ofisi ya TCRA Mwanza kufuatilia taarifa hizo, na kumtaka atoe fedha kiasi cha laki tano ili aweze kumfichia siri ili asitoe taarifa hizo kwa mamlaka inayohusika yaani TCRA.

Baada ya hapo mlalamikaji alitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ambapo Polisi tulituma askari makachero na wamakosa ya mtandao na badae tulifanikiwa kumtia tapeli huyo nguvuni. 

Polisi tunaendelea na mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.Aidha msako mkali wa kuwatafuta wenzeka anaoshirikiana nao katika uhalifu huo bado unaendelea.

Tukio la sita, Mafanikio ya misako Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tumefanikiwa kukamata gari moja aina ya IST rangi ya Silver lenye namba T.892 DFY/DKY na pikipiki mbili moja inanamba MC.836 ASK aina ya BOXER na nyingine aina ya FEKON lakini haina namba. Gari na pikipiki hizo zimekamatwa baada ya kutumika katika matukio ya kiuhalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji na Mkoa wa Mwanza.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, tunatoa onyo kwa wakazi wa Jiji na Mkoa wa Mwanza tukiwataka waache vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, pindi mtoto anapokosea apewe  kalipio na akanywe na kuonyeshwa madhara ya wizi ili atambue kosa na wala sio vipigo. 

Sambamba na hilo tunawataka vijana waache tabia ya kujihusisha na uhalifu kwani utawagharimu.

AJALI YAUA SITA MSATA BAGAMOYO.

 Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Wankyo Nyigesa, (katkati) akionesha Gari lililopata ajali, kushoto ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya kipolisi Chalinze Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Janeti Magomi.
 .............................................................

WATU sita kati yao akiwemo mtoto mchanga jinsia ya kike ,wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa katika ajali ,iliyotokea kijiji cha Msata, barabara kuu ya Segera /Chalinze mkoani Pwani. 

Akitoa taarifa za awali kuhusu ajali hiyo, kamanda wa polisi mkoani Pwani, Kamishna Mzaidizi wa Polisi (ACP) Wankyo Nyigesa, alisema ajali hiyo ,imetokea novemba 5, majira ya saa moja usiku baada ya gari namba T. 124 DHW aina ya Toyota coaster ikitokea Mkata kwenda Mbezi -Dar es salaam ,kuligonga kwa nyuma bila kuchukua tahadhari ,lori namba KBV 746C/ZE2861 FAW iliyokuwa imeegeshwa barabarani kutokana na kuharibika. 

Aidha alisema, dereva wa Toyota coaster iliyosababisha ajali ambae hajafahamika jina lake, alikimbia baada ya kutokea ajali. 

Kamanda Wankyo alisema, waliopoteza maisha ni wanaume watano wenye umri kati ya miaka 30-40 ambao majina yao bado kufahamika .
Alisema ,watu saba walipata majeraha kwenye maeneo mbalimbali ya mili yao.

“Waliopata majeraha ni pamoja na wanaume wanne na wanawake watatu ambao wote wamepelekwa zahanati ya jeshi Kihangaiko -RTS na kituo cha afya Lugoba kwa matibabu zaidi “alisema Wankyo. 
 
Kamnada Wankyo alisema, miili ya marehemu imehifadhiwa hospital ya wilaya ya Bagamoyo kwa uchunguzi wa daktari. 

Alitaja chanzo cha ajali, ni uzembe wa dereva wa gari namba T. 124 DHW aina ya Toyota coaster kujaribu kulipita bila tahadhari gari jingine lililokuwa limeegeshwa baada ya kuharibika na kwamba wanaendelea kumsaka. 

Kutokana na ajali hiyo kamanda huyo alitoa wito kwa madereva, kutii sheria za usalama barabarani na kuacha tabia za kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi ili kuepuka ajali ambazo chanzo chake ni kukiuka sheria za usalama Barabarani.

Kamanda ACP. Wankyo alisema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya madereva wasiotii sheria za usalama Barabarani ili iwe fundisho kwa wengine. 

Kwa upande wa mashuhuda wa ajali hiyo akiwemo, mwenyekiti wa kitongoji cha Pugini, kijiji cha Msata Siasa James alisema hii ni ajali mbaya ambayo haijawahi kutokea eneo hilo. 

“Tulisikia mshindo, na kuona tukimbilie eneo la tukio ndipo tulipokuta gari ya abiria imelivaa lori kwa nyuma na kisha kukatika upande wa kondakta “alieleza. 

Nae Stephen Hinjo alieleza kwamba, gari ya abiria walikutana nayo ambapo ilipita hata dakika mbili hazijapita walisikia kishindo na kutahamaki waliona limekwenda kujikita nyuma ya lori lililokuwa limepaki pembeni mwa barabara. 

“Kufika eneo la tukio tulikuta abiria upande wa kondakta umebanwa huku vichwa viwili vikiwa vinaning’inia chini, wengine wamekatika mikono na shingo, ni ajali haijawahi tokea, “kikubwa tulichokifanya ni kuopoa miili na polisi walifika eneo la tukio “alifafanua Hinjo.